Elections 2010 Wapeni Wapiga kura haki yao sasa!

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Ni hatari sana kumnyima mpiga kura haki yake. Kama tume ya uchaguzi ingeamua kuwapa wapiga kura haki yao kwa kutangaza matokeo kwa muda muafaka bila kuchelewesha kungesaidia kupunguza hasara ambazo zinajitokeza sasa hivi. Tusianze kuwataka wananchi waanze kuwa na hasira. Mimi naamini kuwa ucheleweshaji huu ni kwa maslahi ya upande fulani na wapiga kura wanaelewa sio wale wa hewala bwana wa miaka iliyopita. Wengi kama utaona ni vijana wenye elimu ingawa ya kuunga na hivi wanataka wanachoamini kuwa ni haki yao. Ni kwa nini watu hawa wasiondolewe tashwishi kuamini kuwa kuna wizi unatendeka. Mimi nawashauri tume ya uchaguzi waache uzandiki wao na watangaze matokeo haraka kuepusha hasara zaidi.

Amani Tanzania inawezekana!
 
Back
Top Bottom