Wapendwa yule mtabiri wa asili wa neema na balaa maarufu Kakakuona yuko wapi siku hizu?

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,720
2,070
Heri ya mwaka mpya 2022.
Tunashukuru Mungu kufika na hata kuweza kuinuka na kutembea.
Kwenye mada.
Inaweza pita mwaka wa tano au zaidi sijamsikia huyu kiumbe au mnyama wa ajabu sijui yuko kwenye kundi gani la wanyama.
Kiumbe huyu KAKAKUONA mara nyingi kwenye misimu ya hali ya hewa yenye mgogoro kama huu wa 2021-2022 kiumbe huyu ndio ilikuwa nafasi yake kujitokeza na kutupa ahueni kuwa mwaka huu utakuwaje.
Sijui tumekosea wapi kiasi kwamba kiumbe huyu amesusa na kutokomea kusikojulikana kwa sababu hadi sasa matokeo ni bila bila.
Enzi za mababu zetu kiumbe huyu alikuwa akijitokeza mara kwa mara na kutupa matokeo.Wataalamu wa mambo ya asili kama mpo hebu mtusaidie.
Watu wa mali asili inakuwaje kushindwa kumtunza kiumbe adimu kama huyu kama mlivyowatunza wale vyura wa Kihansi na tumbiri wa Udzungwa? Sasa tumebaki njia panda hatuoni mbele kukoje msimu haueleweki sayansi nayo imeshindwa kututabiria msimu utakuwaje wanatupa tu matokeo ya mda mfupi ya vipindi virefu vya jua na pepo zitazovuma kutoka mashariki kuelekea magharibi, lkn kiumbe huyu alikuwa akitupa full matokeo ya msimu mzima bila kupepesa macho.
Asanteni nisiwachoshe nawatakia mwaka mpya mwema usiotabirika kwa wakulima.
 
Back
Top Bottom