Wapendwa nimfanyaje huyu X husband

Kyeli Lula

Member
Mar 7, 2011
65
6
Wapendwa, Salaam poleni na majukumu, tatizo langu ni kwamba nimeachana na mume wangu takribani miaka sita sasa, mtoto wangu wa kawnza ndio alimaliza darasa la saba mwaka huu, katika kuhangaika kumtafutia shule ili ajiunge na kidato cha kwanza nilimchukulia fomu Marian Boys ya Bagamoyo.

Kwenye fomu niliandika jina la baba na namba ya simu kwa kutambua kwamba ni baba wa mtoto, alifanya mtihani na akafaulu, tatizo illilonisikitisha sana ni kitendo cha huyu baba mtu pindi alipopigiwa simu ili atambue hilo aliwajibu kwamba, huyo mtoto yupo kwa mama yake mimi hanihusu hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine.

Nilipata maelezo hayo baada ya kupiga simu shuleni ili nijue utaratibu unakuaje na kuambiwa nafasi yake ilishatolewa baada ya baba mtu kuwajibu vile. Je baba kama huyu nimfanyaje kwa hili, mtoto amejua na amekosa amani, naombeni ushauri wenu sijawahi kuumia kama nilivyoumia kwa hili.

Asanteni nakaribisha ushauri wenu
 
Pole sana kwa matatizo dada yangu..
Nyote naona mmechangia kwenye hili tatizo.
kwanza ulitakuwa kumjulisha ex mumeo kuwa umejaza namba zake kwenye form za shule ya mtoto.kwa kufanya hivyo msingefikia hapo.
Pia hata kama mmeachana mlitakiwa kukaa chini na kujipanga namna ya kulea watoto...ina kwa kuendekeza ugomvi wenu mmemuumiza mtoto na kakosa fursa ya kwenda shule...nyie mna akili gani...nadhani utakuwa umemweleza mwanao ukweli ndio maana umesema amejua ana amekosa amani...sio yote twawaeleza watoto..
Fanyeni yote ila watoto wasiwe wahanga na 'utoto' wenu.
Tafakari chukua hatua...
 
pole sana. Tumia hilo kama fundisho, wakati mwingine usiandike namba ya huyo baba mtoto. andika details zako mwenyewe
 
  • Thanks
Reactions: EMT
huyo baba ana akili za viatu,sasa hapo anafikiri anamkomoa nani na wewe mama sio kila jambo la kumueleza mtoto tena kwenye umri huo.
inaonyesha hamna mawasiliano mazuri na mwenzako hata kama mmeachana jaribuni kuwa mnawasiliana kwa ishu muhimu kwa maendeleo ya watoto wenu,haina maana kuharibu future za watoto wenu kwa ugomvi/chuki zinazohusu wazazi.
 
Pole sana kwa matatizo dada yangu..
Nyote naona mmechangia kwenye hili tatizo.
kwanza ulitakuwa kumjulisha ex mumeo kuwa umejaza namba zake kwenye form za shule ya mtoto.kwa kufanya hivyo msingefikia hapo.
Pia hata kama mmeachana mlitakiwa kukaa chini na kujipanga namna ya kulea watoto...ina kwa kuendekeza ugomvi wenu mmemuumiza mtoto na kakosa fursa ya kwenda shule...nyie mna akili gani...nadhani utakuwa umemweleza mwanao ukweli ndio maana umesema amejua ana amekosa amani...sio yote twawaeleza watoto..
Fanyeni yote ila watoto wasiwe wahanga na 'utoto' wenu.
Tafakari chukua hatua...
Vin D, Baba alikuwa anaelewa kila kitu, hata mtoto alipofaulu nilimweleza, ila nadhani yeye ndio anaamua kumwumiza mwanae kupitia mimi akijua ananikomoa mimi, suala la mtoto kujua alifatilia mwenyewe pale msimbazi na kuambiwa hivyo baada ya kuona mimi namchenga kumwambia ukweli, tatizo hapo sio utoto tunatofautiana uelewa
 
upo sahihi mkuu.
 
Kama tatizo sio utoto ila ni kutafautiana kwa uelewa then jitahidi kutumia uelewa wako kumlinda mtoto wako dhidi ya baba huyu asiejua majukumu yake....si wajua tena mbwa ukimjua jina lake hakusumbui kabisa...
 
dah nimeisikia hii nikabaki kushangaa tu,pole sana dada yangu.mwachie mungu tu madingi wa hivi huwa wanakuja kuipata fresh fainali,sasa hivi haoni faida ya mwanae kwenda kusoma
 
Pole sana kwa yaliyokukuta. Ila samahani swali langu kwako ni:
JE HUYO BABA ANAMLEA MTOTO WAKE KWA NAMNA YOYOTE ILE KIASI KWAMBA IKABIDI UWEKE DETAILS ZAKE KWA FORM???

Nimejikuta naandika ukurasa hapa imebidi nifute maana hata hujanijibu hilo swali. Kuna majitu mabichwa maji kweliiii ngoja nisiendelee.
 
Muulize atayakubalimafanikio ya mtoto baadae?akatae kwa maadnsihi na uweke katika kumbukumbu komaa na somesha mwanao
 
Pole sana kwa yaliyokukuta. Ila samahani swali langu kwako ni:
JE HUYO BABA ANAMLEA MTOTO WAKE KWA NAMNA YOYOTE ILE KIASI KWAMBA IKABIDI UWEKE DETAILS ZAKE KWA FORM???

Nimejikuta naandika ukurasa hapa imebidi nifute maana hata hujanijibu hilo swali. Kuna majitu mabichwa maji kweliiii ngoja nisiendelee.
MamaTuli Dada we acha maana nikisema niandike kila kitu watu watamaliza kusoma kesho, yaani ni mwanaume msumbufu, mtesaji mnyanyasaji sijawi kuonaona, huwa atoa hela kwa kusumbuana kwanza utadhani sio mwanae
 
dah nimeisikia hii nikabaki kushangaa tu,pole sana dada yangu.mwachie mungu tu madingi wa hivi huwa wanakuja kuipata fresh fainali,sasa hivi haoni faida ya mwanae kwenda kusoma
Yaani Kaka yangu wewe acha tu roho imeniuma sana asante kwa kunipa moyo
 
Kwangu mimi huyo baba alifanya vibaya.

Sasa suala la wewe umfanye nini, nadhani ni kumuacha tu matatizo ya wazazi kuachana ni mengi tu tena hilo lako dogo. Kuna wazazi wakiachana wanaenda kutorosha watoto shuleni na kuwahamishia shule nyingine.

Mie pia yalinikuta kama hayo kwa namna tofauti. Tulipotengana na wife (miaka 6 kama wewe) watoto walikuwa wanasoma St mathews. Muhula ulipotimu walikuwa kwake hivyo akawapeleka. Wakati wa kuandikisha watakaojulishwa wakati wa ajali akamuandika bwana anayeishi nae (wakati tuko pamoja alijenga, tulipotengana akahamia huko, AKAOA). Nikanyamaza mpaka leo. Watoto wameenda vyuoni, nilipomuuliza mmoja wao amepewa shilingi ngapi na mama, akasema 5,000 (mama ana uwezo kidogo wa kunywa bia na kuchagua kiburudisho cha siku).

Hivyo kimsingi vumilia. Ni-pm tuliwazane.
 
Funga safari nenda kwa yule father wala hana neno....lol sipati picha ingekuwa mimi, baba gani asiyekuwa mstaarabu shule ile inawindwa na watu kibao embu fikiria watoto 6000 tanzania nzima wamefanya wamechaguliwa 120 tu huwezi kuwa proud na mtoto wako???pole sana maskini ka kwangu pia kamepata
 
Kabla sijakupa pole ni heri nikushauri kuwa;

Kwa sasa tulia kabisa yaani achana na wazo la kwamba umfanyeje huyo jamaa. Pata muda wako mzuri wa kumtafutia mahali pengine, sio big issue ki vile, tulia kabisa ukishampatia dogo shule na ukishalipa, mtafute either direct au kwa kupitia ndugu ili adi-declare kwa maandishi kuwa hamtaki huyo mtoto kisha itunze hio document uje umuonyeshe mtoto the moment baba atakapokuja kumhitaji......

Naamini siku moja atakuja kumhitaji tu na ndio hapo na wewe utamkumbusha haya kabla ya kumsamehe, bytheway, umchukulie kama chizi fulani tu na sio ajabu ukute yupo humuhumu ndani.....pole Sissy
 
Unajua nimejiuliza kitu, kwenye ile form kuna kuweka namba mbili ya mama na pia baba ina maana hata hawakujaribu yako? na walibandika majibu pale msimbazi jtatu hukwenda?
 
Kabla sijakupa pole ni heri nikushauri kuwa;

Kwa sasa tulia kabisa yaani achana na wazo la kwamba umfanyeje huyo jamaa. Pata muda wako mzuri wa kumtafutia mahali pengine, sio big issue ki vile, tulia kabisa ukishampatia dogo shule na ukishalipa, mtafute either direct au kwa kupitia ndugu ili adi-declare kwa maandishi kuwa hamtaki huyo mtoto kisha itunze hio document uje umuonyeshe mtoto the moment baba atakapokuja kumhitaji......

Naamini siku moja atakuja kumhitaji tu na ndio hapo na wewe utamkumbusha haya kabla ya kumsamehe, bytheway, umchukulie kama chizi fulani tu na sio ajabu ukute yupo humuhumu ndani.....pole Sissy

Elli tatizo shule karibu zote bab kubwa zinakuwa zimejaa, na mtoto kichwa namna hiyo akikosa shule zenye challenge yaan wakutane vichwa watupu atapoteza kipaji chake
 
Back
Top Bottom