Wapendekeza matokeo ya Urais yapingwe Mahakamani

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
WADAU wa siasa wametoa maoni kuhusu uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuridhia pendekezo la kikosi kazi cha kuratibu demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Miongoni mwa mambo hayo ni matokeo ya urais kupingwa mahakamani.

Wadau hao ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ambacho mapendekezo 12 ikiwamo kuruhusu matokeo ya urais kupingwa iwapo miko ya msingi na kuruhusu mgombea binafsi, kwa ajili ya kuimarisha demokrasia ya vyama vya siasa nchini.

Mapendekezo yalitolewa Dar es Salaam, jana na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Anna Henga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kimetoa mahakamani kutakuwa na malalamiko hayo, mambo ya kipaumbele ya LHRC wamefuatilia.

Alisema uwasilishwaji wa ripoti ya Kikosi Kazi hicho kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuamua kutoa mapendekezo ambayo kikosi hicho ni vyema kikayazingatia wakati wa ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wadau.

“Tunapendekeza kuruhusu matokeo ya kiti cha urais kupingwa mahakamani ikiwa kuna malalamiko ya msingi, kwani tunachukulia kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Haki za Binadamu na Watu katika kesi ya Jebra Kambole dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na. 018/2018," alisema Henga.

Alifafanua kuwa, mahakama hiyo iliamua kuwa Ibara ya 41 (7) ya kutopinga matokeo ya urais ni kinyume cha Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu wa mwaka 1981.

Kuhusu suala la mgombea binafsi, alisema hatua hiyo itakwenda sawa na uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu ya Watu, katika kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na. 011/2011.

"Hatua hiyo ya kuwapo kwa mgombea binafsi, itasaidia kupunguza urasimu wa vyama vya siasa ambavyo hutumia sifa za uanachama dhidi ya wagombea, ikitokea kutoelewana kati ya pande mbili,” alisema.

Alisema, LHRC pia inapendekeza kuwapo mfumo wa 50+1 kuwa kigezo cha ushindi wa uchaguzi mkuu, na kuwe na uwakilishi sawa wa jinsia wa 50/50 kwa kuweka kipengele mahsusi kitakachoweka sharti kwa sera au sheria yoyote kuzingatia usawa wa kijinsia.

Mapendekezo mengin ni Jeshi la Polisi kutoingilia shughuli za vyama vya siasa wakati, kabla na baada ya kampeni kinyume cha sheria, na kushauri tume ya uchaguzi kuwa na watumishi wake, ili wakurugenzi wa halmashaauri wasiwe wasimamizi wa uchaguzi katika ngazi ya jimbo.

"Lakini wa uchaguzi, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na makamishna wapatikane kwa kuomba kazi ambazo zinatangazwa hadharani na uteuzi wa wajumbe wa tume ya uchaguzi uzingatie uwakilishi wa vyama vikubwa vya siasa, asasi pia mkurugenzi za kiraia, taasisi za kidini na wanataaluma," alisema.

Henga alisema, LHRC ina shauri kigezo cha kupita bila kupingwa kiondolewe, hata kama mtu atapita bila kupingwa kuwe na kura ya ndiyo au hapana, na pia kuwe na mfumo wa kielektroniki wa kupiga kura.

Aidha, kisheria kwa vyama vya siasa kuzingatia usawa wa kijinsia na watu wenye ulemavu wakati wa mchakato wa uteuzi.

"Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ifanyike kwa usawa kwa vyama vyote, na pia nafasi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iwe ya kutangazwa hadharani kwa vigezo vitakavyoanishwa na kamati kuajiri," alisema.

Pia, Sheria ya Vyama vya Siasa ifanyiwe marekebisho na kuondoa yale yaliyofanyika mwaka 2019 ambayo kwa kiasi kikubwa yalirudisha nyuma ustawi wa demokrasia ya vyama vingi.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom