Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,607
- 4,264
Uchaguzi umemalizika sasa na matokeo yameshatangazwa. Ma-Rais waliochaguliwa wameshatangazwa, mmoja alishaapishwa, mwingine bado ni mteule naye ataapishwa muda si mrefu (kama bado). Wabunge nao wataapishwa mara baada ya Rais kuapishwa na wote waliopewa dhamana wataingia kazini.
Sitaki kuzungumzia mchakato wa uchaguzi na mema na mabaya yake mwaka huu maana mengi yameshasemwa na yataendelea kusemwa. Yaliyotokea wote tumeyasikia, kuyaona au hata kuyashiriki.
Matokeo ya uchaguzi mwaka huu yameonyesha sura tofauti ya kukua kwa uelewa wa wananchi katika masuala ya demokrasia kuelekea uchaguzi mkuu. Hapa naongelea kwa wale waliojitokeza kupiga kura, japo ni asilimia ndogo ya waliostahili kupiga kura. Imeonyesha kuwa watu wanaelewa kuwa katika demokrasia haitoshi tu kuwepo pale kama kisiki kisichotikisika kutokana na mizizi yako ya muda mrefu. Siku ikifika watu wanaweza kuja na sururu, shoka, hata tingatinga na kukung'oa. Tuliona kwenye kura za maoni na tumeona hayo katika uchaguzi mkuu.
Kwa muda mrefu sasa, katika chaguzi zote CCM imekuwa ikifaidi mtaji mkubwa utokanao na 'ujinga' wa watanzania walio wengi. Kutokana na CCM kuwa 'chaguo-msingi' (default party) hasa kwa sababu kimeendeleza utawala wa enzi za chama kimoja, kilipata faida ya kuwa na misingi tangu kwenye mashina na matawi. Watu wengi waliendelea kuchukulia uongozi wa mitaa, kata n.k kama sehemu ya CCM hata baada ya chama na serikali kutenganishwa. Ikawa sasa ni jukumu la vyama shindani kupeleka sera zake kwa hawa watu kwamba sasa hivi si CCM pekee iliyopo Tanzania, jaribuni na vyama vingine. Ni zoezi gumu lakini baadhi ya vyama maendeleo yake ni mazuri katika hili.
Suala ninalotaka kuzungumzia ni kuwa CCM imetumia uelewa mdogo w raia wengi juu ya siasa za vyama vingi kuendelea kuwa na 'support' mahali pengi hasa vijijini. Matokeo ya mwaka huu yanaonyesha hali inaanza kubadilika. Vuguvugu lililoanzia kwa wasomi na wale wa mijini linaelekea kuendelea hadi vijijini na hii imepelekea CCM kupoteza viti vingi vya ubunge na udiwani ikilinganishwa na chaguzi zilizopita. Hata ushindi wa Rais umekuwa mdogo sana ikilinganishwa na JK 2005. CCm ilipanga ushindi wa kishindo lakini wakati namsilikiliza Kinana akitoa tathmini ya uchaguzi, alisema CCM imepata ushindi 'mzuri' si wa 'kishindo' tena.
CCM inatakiwa ifahamu kuwa ujinga si kilema cha kudumu. Mtu mwenye akili zake ila asiyeelewa jambo fulani, akieleweshwa vizuri ataelewa tu na ujinga utamtoka. Hili ndo tunaloliona. Kama CCM itaendelea kuwahadaa watu na kutowatimizia ahadi ambazo imemwaga wakati wa kampeni; kama CCM itaendelea kukumbatia mafisadi ambao wanelekea kukiendesha chama; Kama mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Tanzania ataendelea kuufanya uenyekiti na u-Rais kuwa wa ubia na wa ki-familia; kama JK ataendelea kudanganywa na wafuasi wake, na kuendelea kudanganya wananchi akishadanganywa...(na mengineyo) na vyama-shindani vikaendeleza elimu ya uraia na haki ya mwananchi na mpiga kura wakati wa miaka mitano, na mitano tena ijayo basi inawezekana CCM hawatasema wamepata ushindi 'mzuri' tena maana watakuwa wameshindwa hata kabla ya uchaguzi.
Ujumbe hapa ni kuwa watanzania si wajinga tena na wale ambao uelewa haujawafikia, watabadilika muda si mrefu.
Ni jukumu la wapenda CCM kama kweli wapo kufanya tathmini na kujua nini wafanye ili watanzania wawaamini tena. Wasipange mbinu za kubadilisha matakwa ya wananchi kwa uchakachuaji. Waelewe kuwa enzi za kutembea gizani zimepita na hawatakiwi tena kutembea uchi wakijidanganya kwa kufumba macho wakiamini kuwa kama wao hawawaoni watu njiani (kwani wamefumba macho) basi na wtu hawawaoni...Watu wako macho sasa na wanaona.
Kazi kwenu CCM, mi yangu macho!