Wapemba wamtaka Maalim Seif apumzike kugombea urais

wagagagigi

JF-Expert Member
Dec 9, 2014
890
983
Salaam wana JF.

Muelekeo wa kisiasa Zanzibar sasa unaelekea kugeuka. Pamoja na kwamba Maalim Seif bado anapendwa na kuheshimiwa na Wazanzibari walio wengi, wengi wa Wazanzibari wanaona kwamba Maalim Seif kwa hulka yake ya 'kujawa na uislamu' kunarejesha nyuma, kunachelewesha au kuzorotesha harakati za kuingo'a CCM.

 
Sio kugomea tu maalim afunguliwe mashtaka kwa kuhamasisha maandamano yaliuwa wapemba wengi

It was suicidal protest .Mungu atamchomq moto mkali kawa wa kuyeyushia vyuma

State agent
 
Kifupi Mama anasema wamechoka na uvumilivu wa Sefu, amejaa uislamu maana yake amajaa roho nzuri ya kusamehe kuliko mapambano

Ina maana watu wapo tayari kwa lolote tatizo ni Sefu na huruma yake dhidi ya CCM.

Raia wako tayari kwa kila kitu ila Sefu inafika wakati Imani inamzidi anaona kama ni maswala ya kawaida.

Huu ujumbe ni Mzito sana Kwa Sefu.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maalim Seif hajajibu hoja ya huyo mama. Hapo Bi Mkubwa anamwambia wewe mwaka hadi mwaka tunapoporwa ushindi unakazi ya kutuambia subirini subirini subirini! Maana yake mama alitaka
Seif Shari atoe amri ya kukinukisha
Mbona Maalim kamjibu kuwa vurugu zitasababisha watu kuumia
Maalim anajua fika kuwa ccm wanapenda ajiingize kwenye vurugu halafu waseme Maalim anafuga Magaidi tazama mashekhe wa uamsho wanavyoteswa
Mbinu pekee ni kuwashinda tena ccm kwenye boksi la kura safari hii dunia mzima inaangalia
Mwisho ccm wataachia tu mamlaka ya visiwani
 
Kifupi Mama anasema wamechoka na uvumilivu wa Sefu, amejaa uislamu maana yake amajaa roho nzuri ya kusamehe kuliko mapambano

Ina maana watu wapo tayari kwa lolote tatizo ni Sefu na huruma yake dhidi ya CCM.

Raia wako tayari kwa kila kitu ila Sefu inafika wakati Imani inamzidi anaona kama ni maswala ya kawaida.

Huu ujumbe ni Mzito sana Kwa Sefu.!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huu ujumbe wa mama hauna uzito sana kwa Maalim Seifu, huu ni ujumbe mzito kwa watawala. Hawa watu wa kisiwa hiki ndio wale waliopitia madhila ambayo hata Rais wa awamu ya tatu ameandika kwenye kitabu chake kwamba ni miongoni mwa mambo yanayomuuma sana akiyakumbuka. Wapemba walipigwa, wanawake wao wakabakwa, watu kadhaa wakauliwa na wengine kukimbilia uhamishoni Shimoni Kenya hadi Somalia!

Huyo mama kwa umri wake huwezi kutarajia kuyasema aliyoyasema. Ni hatari sana kumbana mtu mpaka afikie hatua ya kusema "potelea mbali". Nahisi bi mkubwa hapo anawakilisha hasira zilizojificha za wana wa Pemba.

Natamani na nawaomba viongozo wetu wenye busara na hekima waliangalie hili na ikiwezekana walete meza ya maridhiano ili vinyongo viondoke
 
Mbona Maalim kamjibu kuwa vurugu zitasababisha watu kuumia
Ni kweli mkuu Maalim amemjibu hivyo lakini mama alikua na hoja kuu kwamba kama miaka mingi Maalim anataka watu watulie kitu ambacho mimi nakikubali kabisa, lakini sasa akae pembeni ili watu wengine wagombee hiyo nafasi kwani Maalim hana tena njia nyingine mbadala ya kuhakikisha maoni na sauti za watu kwenye sanduku la kura zinasikilizwa na kuheshimiwa, na wala sio lazima kufanya fujo au kuleta machafuko, zipo njia nyingi za kushinikiza ajenda yao
 
Back
Top Bottom