Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Ni mwanzo wa mapambano na wahafidhina wa CCM,hivi ndivyo inavyotakiwa ifanywe kwa wale ambao wapo mstari wa mbele katika kuona haki haifuati mkondo wake ,ikiwa Sheha amepewa mamlaka ya kutoa barua na anawanyima wakazi barua hizo au anazitoa kwa ubaguzi kutokana na shinikizo la CCM basi sasa dawa yao ndio hio imeanza kuchemka ,itabidi wazifahamu na sauti badala ya sura ,kuwa sauti hii ni ya mwanachama wa CCM hivyo tumpe barua ya kupata kadi ya Uraia na hii ni sauti ya mtu asieitakia mema CCM. Ila kitu kimoja kikumbukwe kuwa baadhi ya mikakati hii hufanywa na CCM wenyewe (Badboys) ili kuipaka matope CUF ,kuna yale yaliotokea siku za miaka ya nyuma,ulipuaji wa mabomu Unguja ,wachunguzi walitoka makao makuu ya upelelezi Dar mpaka leo hawakutoa jawabu la waliohusika,alielipukiwa na bomu kisiwani Pemba katika matayarisho ni CCM ,hakuulizwa kitu alipelekwa Dar kutibiwa ,waliokuwa wakitia vinyesi katika visima Pemba walijulikana kuwa ni CCM na wakikusanya vinyesi kwenye magereza hawakufanywa kitu ,wala hakuna hatua yeyote waliochukuliwa ,hivyo hata na hili linawezekana kabisa ni la CCM ,ili kuvipa nguvu vyombo vya dola kufanya maovu na kuonyesha kuwa Pemba kuna matatizo,ni katika mbinu za kuwafanya iwe rahisi kukwiba kura na kuwatisha watu kwa kutumia vyombo hivyo,kwa ilikwisha chunguzwa kuwa hakuna haja ya kupeleka majeshi na mapolisi kwa wingi ,ili kurudisha upotofu imewabidi wafanye lolote lile litakalowawezesha kuendelea kuweka vyombo vya dola ili kurahisisha wizi wao. Ila itakavyopigwa ndivyo hivyo itakavyochezwa ,Wenyewe wanasema Pemba peremba.
SHEHA wa Shehia ya Ole Muhogoni Mkoa wa Kaskazini Pemba Mussa Ali Kombo amemwagiwa tindikali usoni na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.
Kamanda wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi amethibitisha kutokea tukio hilo majira ya saa mbili usiku na kuahidi kuwatafuta wote waliohusika na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Alisema jeshi la polisi bado linafanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ili kuweza kujua zaidi chanzo cha tukio hilo pamoja na kuwatia mikononi watu waliofanya kitendo hicho cha kikatili.
Chanzo cha tukio hilo inasadikiwa ni kufuatia zoezi la daftari la uendelezaji kastika daftari la kudumu la wapiga kura katika kisiwa cha Pemba,ambalo linaratibu wapiga kura wapya na wale wa zamani kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani.
Chama cha mapinduzi Mkoa wa Mjini Magharibi kimetoa taarifa kwa vyombo vya habari leo hii mjini Unguja huku kikilaani kutokea kwa tukio hilo linalotishia amani
Aidha CCM Katibu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ramadhan Abdallah Ali imeelezea kusikitishwa kwake na tukio hilo kupitia taarifa hiyo kwa vyombo vya habari
Akizungumza na gazeti hili Sheha wa Shehia ya Ole Muhogoni, Mussa Ali Kombo amesema majira ya saa mbili uziku amekutwa na mkasa huo wakati akirudi dukani kununua sirgireti baada ya kurejea msikitiki kusali sala ya ishaa ndipo alipowaona vijana mbele yake na kumwagia kitu alichokuwa hajakifahamu lakini alihisi maumivu makali kama ya kuchinjwa na kisu mwilini.
Zoezi la uandikishaji kwa wapiga kura wapiya lilianza Kisiwani Pemba katika wilaya ya Micheweni ambapo zoezi hilo mwezi uliopita.
Katika salamu za masikitiko Katibu wa huyo wa CCM alisema CCM imesikitishwa na kitendo hicho ambacho wamekiita ni cha kikatili chenye lengo la kujenga chuki na kuvuruga zoezi la daftari la kudumu la wapiga kura.
Ali alitoa amekitupia lawama chama cha wananchi CUF akidai tangu kuanza kwa daftari la kudumu la wapiga kura kimekuwa kikilalamika kwamba wafuasi wake hawaandikishwi.
'Tumepokea taarifa za kutiwa tindikali sheha wa Ole kwa masikitiko makubwa...tunaitaka serikali kuchukuwa hatua kali za kisheria pamoja na kuwapatia ulinzi masheha wote 'ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari,katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Seif Shariff Hamad alielezea kutoridhishwa na zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea katika kisiwa cha Pemba ambapo wafuasi wengi wa CU inadaiwa wamekataliwa ikiwemo pamoja na kupewa kitambulisho cha ukaazi.
Hamad alisema hadi sasa katika majimbo matano ya wilaya ya Kaskazini A Unguja watu 12,363 wameripoti katika idara ya vitambulisho kudai vitambulisho vyao, watu 2584 wamenyimwa kupewa vitambulisho ambapo katika jimbo la Konde watu 1559 wamekataliwa kuandikishwa wakati katika jimbo la Mgogoni ni watu 1237 wamewekwa kando katika zoezi hilo.
Wajumbe wa Baraza la wawakilisji wa CUF kwa nyakati tofauti waliitahadharisha serikali wakati wakichangia bajeti mbalimbali za SMZ na kuitaka kuwa makini kutokana na idadi kubwa ya wananchi kunyimwa nafasi za kujiandikisha.
Chama cha CUF kimetoa wito na kuutaka Umoja wa Mataifa kusimamia uchaguzi mkuu ujao mwaka 2010 na pia wakilitaka shirika la umoja huo la UNDP kuijiaondoa katika ufadhili wa zoezi hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ Suleiman Othman Nyanga alisema hakuna mtu atakayenyimwa haki ya kuandikishwa na kila mtu anatakiwa kufuata sheria.
Vituko vya uvunjaji wa amani katika kisiwa cha Pwemba aghalab hutokea wakati huu kuelekea katika uchaguzi mkuu wa nchi ambapo mwaka 1995 Afisa mmoja wa CCM Ali Mwinyi Msuko pia alimwagiwa tindikali.
MWISHO