WAPEMBA KARAFUU NA MAFUTA-Waomba kujitenga UN

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Wapemba wataka kujitenga kama Kosovo,waiomba Marekani iwasaidie
* Wasema wamechoka kutengwa

Na Salma Said, Pemba
BAADHI ya wazee wa visiwa vya Pemba wameiomba Serikali ya Marekani kufanikisha visiwa hivyo vijitenge na Muungano wa Tanzania, kwa sababu ya kutetereka kwa mwafaka wa kisiasa Zanzibar. Ombi hilo walilitoa jana asubuhi kwa Balozi wa Marekani nchini, Mark Green walipozungumza naye kabla ya balozi huyo kukutana na wabunge na wawakilishi katika Hoteli ya Treasure kisiwani hapa.
Walimtaka Rais Bush kuwasaidia kujitenga kama alivyofanikisha Kosovo kujitenga na kuwa taifa huru.Wazee hao walisema mazungumzo ya Mwafaka yaliyochukua miezi 14, yakiwashirikisha wajumbe kutoka CCM na CUF na hayakuleta matumaini yoyote na kwamba, hoja ya kupigia kura ya maoni serikali ya mseto, inaonyesha kuwa CCM hawana lengo zuri juu ya wananchi wa Pemba.
"Kwa kuwa mazungumzo hayakuleta faida na hakuna Wapemba katika Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano nayo imeshindwa kutekeleza maombi yetu na sisi wananchi wa Pemba ndio tunaoumia, basi sisi tunakutuma utupelekee salamu zetu kwa Rais Bush kwamba tunataka kujitenga kama walivyofanya Kosovo hatuna haja na kuendelea kukaa na watu wasiotutaka," alisema Bakari Mohammed.Wazee hao Bakari Mohammed kutoka Micheweni na Juma Kombo kutoka Wete ambao waliwawakilisha wazee wengine waliojazana nje ya hoteli hiyo, walimweleza Balozi Green kwamba, wanashindwa kuwadhibiti vijana wao kutokana na hasira walizonazo tokea kutolewa tamko la Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Butiama mkoani Mara wiki iliyopita.Balozi huyo alilazimika kuzungumza na baadhi ya wazee wachache, baada ya wananchi wengi waliojitokeza katika hoteli hiyo kutaka kuzungumza naye.Wazee hao walisema wamesikitishwa na kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kutetea maamuzi ya Butiama, wakati walikuwa wakimtarajia yeye kumaliza mpasuko kama alivyoahidi.Wamesema ikiwa kutakuwa na kura ya maoni juu ya kuwepo kwa serikali ya mseto, basi pia serikali ipitishe kura ya maoni juu ya wananchi wa Pemba, kama wanataka kujitenga na kisiwa chao au laa kwa kuwa mambo mengi yanafanyika bila ya kuulizwa wananchi na kwamba, wananchi wa Pemba wamekuwa wakinyimwa fursa ya kuwemo ndani ya Serikali kwa muda mrefu hali ya kuwa Unguja na Pemba ni nchi moja.
Wazee hao wamesema vijana wengi wamechanganyikiwa na wana hasira kubwa juu ya mwenendo unavyokwenda hasa pale baada ya kupokea vikaratasi vikiwataka wapemba wahame Unguja na kwenda kwao, hivyo vijana wamesema inaonyesha dhahiri nia mbaya na ya kuwabagua Wapemba inaendelezwa na watawala wa Zanzibar.
"Hatuna utamaduni wa kuulizana katika mambo ya maamuzi wakubwa wanajiamulia wenyewe, na kama kuna kura ya maoni basi tuulizwe sisi kama tunataka kuendelea na mazungumzo au tunataka tujitoe maana imekuwa kawaida kuonewa sisi Wapemba," alisema Mohammed.
"Kama jumuiya ya kimataifa itapuuza kilio cha Wapemba kutaka washirikishwe ndani ya serikali yao ya Zanzibar tutajua Marekani nayo haina nia njema na wananchi wa Pemba," alisema Mariam Juma.
Wazee hao wamesema iwapo juhudi za Rais Kikwete zimeshindwa kabisa katika kufanikisha suala la mwafaka basi kura ya maoni iwe chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa na Zanzibar.
Kwa upande wao wabunge na wawakilishi, walimwelezea Balozi huyo wa Marekani kwamba,tangu kusita kwa mazungumzo hayo wananchi wamekata tamaa na wanashindwa kuwazuia kutokana na hasira walizonazo.Wabunge hao pia walisema pamoja na misaada inayotolewa na serikali ya Marekani katika Kisiwa cha Pemba, ya kuhakikisha kinapata maendeleo lakini hakuna maendeleo bila ya kuwapo demokrasia nchini.Akizungumza na wabunge na wawakilishi, Balozi Green aliwaahidi kufuatilia suala la mazungumzo kati ya CUF na CCM katika ngazi mbalimbali, ikiwamo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Jumuiya za Kimataifa.
Aliwahakikishia wabunge na wawakilishi kwamba, suala la mwafaka atalifuatilia kwa karibu na pia kufikisha salamu za wazee kwa Rais Bush, huku akiwataka kuendelea kuwa wavumilivu wakati masuala hayo yakiendelea kujadiliwa katika ngazi za juu.Balozi Green alisema, Marekani imekuwa ikifuatilia mazungumzo kati ya CCM na CUF na itahakikisha yanamalizika bila ya kuathiri hali ya amani.
Baada ya kikao hicho Kiongozi wa Upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano,Hamad Rashid Mohammed alisema iwapo serikali mambo hayo hayatashughulikiwa, basi hali ya kuwepo mpasuko wa kweli itajitokeza katika kipindi hiki ambacho wananchi wengi wamekata tamaa.
"Hali ni mbaya sana hivi sasa, wananchi wetu wamekata tamaa na serikali zao zotembili, wameona jinsi mambo yao yanavyoshindwa kushughulikiwa sasa kama hatutakuwa makini basi mpasuko wa kweli unakuja na ni hatari sana hali hii" alisema Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Wawi.
Katika hatua nyingine, watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana, wamesambaza vikaratasi vyenye ujumbe wa kuwataka wananchi wa asili ya visiwa vya Pemba, wanaoishi Unguja kuondoka mara moja na kurudi kwao katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa, vinginevyo watakiona cha moto.
Katika mitaa ya Unguja vikaratasi hivyo vimezagaa maeneo mbalimbali, likiwamo eneo la Mkoa wa Mjini Magharibi na ambako kuna wafanyabiashara na wengi wanaofanya shughuli zao, wakati kwa upande wa Pemba vikaratasi hivyo vimezagaa katika maeneo ya Chake Chake na Wete.
Ingawa vikaratasi hivyo havina saini wala jina la aliyeandika, tangu asubuhi jana wananchi wa viswani walikuwa wakivisoma na kuzua mjadala mzito mitaani.
"Ilani kutoka Mzimu Butiama Wapemba hamna fadhila na hamfadhiliki tumechoka nanyi, tunawapeni mwezi mmoja mujiandae kurudi kwenu mkaendeleze fitina zenu kwenu," sehemu ya ujumbe uliopo katika vikaratasi hivyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban hakupatikana kwa njia ya simu alipotakiwa kuthibitisha kuwapo kwa vikaratasi hivyo vinavyohatarisha amani.
 
Kwa Kawaida Mtu Asiyejua Chochote Kuhusu Nchi Yake Hawezi Kusema Chochote Kikakubaliwa Au Kueleweka Sawa Na Hao Wazee ,hao Wazee Wamezaliwa Wakakuta Muungano Upo Na Utaendelea Kuwepo Hata Wao Wakiondoka Na Hawajui Chochote Kuhusu Muungano Zaidi Ya Kukaa Kucheza Bao Na Kuvalishwa Vilemba Vya Ukoka
 
waandishi msiwe mnaandika habari za uchonganishi kama hizi bila kuweka bayana majina ya wazee hao ili sheria ichukuwe mkondo wake
 
waandishi msiwe mnaandika habari za uchonganishi kama hizi bila kuweka bayana majina ya wazee hao ili sheria ichukuwe mkondo wake

Ah! Ndugu yangu Uandishi huko umezongwa na ushabiki. Watu wanandika kama wanatoa beti za mipasho. Bi Salma Said tokea lini akawa Mwandishi. Hiyo ndio Zenj.
 
Peleka kura ya maoni Pemba, kama Wapemba wanataka kujitenga wawe nchi yao wape uhuru.

Kesho Unguja nao wakitaka kujitenga sawa.

Keshokutwa Mafia wakitaka kujitenga poaa tu.

Baadaye dry dock Kahama wakitaka kuchukua dhahabu zao wawe nchi nao poa tu.

Kigoma wakiona tunawayeyusha hawapati huduma wanataka kuwa ki nci nao poa tu.

As long as ni wananchi wenyewe ndio wanataka, after all isn't democracy supposed to be the rule of the people by the people and for the people? Then how come the people wants a referendum and the bigger heads can't have that.Is that democratic?
 
Back
Top Bottom