comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Kitengo cha ujasusi nchini Korea Kusini kinaamini kwamba washukiwa wanne wa Korea Kaskazini wanaohusishwa na kifo cha Kim Jong nam ni wapelelezi.
Ndugu huyo wa kambo wa rais wa Korea Kaskazini aliwekewa sumu katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur kulingana na maafisa wa polisi wa Malaysia.
Wanne kati ya washukiwa saba waliotajwa na serikali ya Malaysia wanafanya kazi katika wizara ya usalama ,na ujasusi kulingana na wabunge mjini Seoul.
Haijulikani ni akina nani kati yao wanaotafutwa na serikali ya Malaysia.
Bwana Kim alifariki wiki mbili baada ya wanawake wawili kumfuata katika uwanja huo wa ndege.
Wanasema walidhani walikuwa wanahusishwa kufanya filamu ya mzaha.
Bwana Kim alipakwa sumu kali ya kuua neva kwa jina VX na kufariki akiwa na uchungu mkali kati ya dakika 15-20, alisema waziri wa afya wa Malaysia siku ya Jumapili.
Maafisa wa polisi wa Malaysia walimkamata raia mmoja wa Korea Kaskazini kwa jina Ri Jong Chol siku chache baada ya mauaji hayo.
Watu wengine 6 kutoka Korea Kaskazini wametajwa kuwa washukiwa na wanasakwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo.
BBC SWAHILI