WAPC yailaumu serikali kwa kutishia kufunga magazeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WAPC yailaumu serikali kwa kutishia kufunga magazeti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Njowepo, Oct 28, 2010.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Na Richard Makore
  28th October 2010
  Umoja wa Mabaraza ya Habari Duniani (WAPC), umelaani vitisho vilivyotolewa na Serikali ya Tanzania vya kutaka kufungia magazeti ya Mwananchi na Mwanahalisi pamoja na kukionya Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa).

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa WAPC, Chris Conybeare na nakala yake kupatikana nchini kupitia Baraza la Habari Tanzania (MCT), iliitaka Serikali kuhimiza na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kutoa maoni nchini.

  Conybeare alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa WAPC uliofanyika Kathmandu nchini Nepal ambapo aliitaka Serikali kusimamia kwa dhati uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kutoa maoni badala ya kuukandamiza.

  Aidha, WAPC umeelezea kusikitishwa kwake kutokana na kudorora kwa juhudi za kubadilisha sheria mbaya zinazokandamiza uhuru wa vyombo vya habari na kuopngeza kuwa ni vyema juhudi hizo ambazo zimechukua takribani miaka minne zikamilike.

  WAPC imetaka kupitishwa haraka kwa sheria ya haki ya kupata habari na ile ya huduma za vyombo vya habari hapa nchini.

  Nakala ya taarifa hiyo ya WAPC ambayo ilipatikana jijini Dar es Salaam jana ilisainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa MCT, Pili Mtambalike, ambapo pia ilisisitiza umuhimu wa kuwa na sheria inayolinda vyombo vya habari badala ya hii ya sasa ambayo inavikandamiza.
  CHANZO: NIPASHE
  MY TAKE
  Labda wazungu wakiongea watawaelewa
   
Loading...