Wapare hawaruhusiwi kuoa Makabila mawili; Washana na la pili ni lipi?

Bongo.Com

Member
May 17, 2015
52
20
Kabla ya yote tunaomba kujua hilo kabila la pili ni lipi? Japo Kabila hilo nimelisahau ila nakumbuka niliambiwa linapatikana Tanga.

Baada ya kulifahamu kabila hilo, naomba kujua kihistoria au ni sababu zipi zilizosababisha Wapare tusioe makabila hayo mawili, kwani tunaishia tu kuambiwa na mabibi na mababu zetu kuwa "Haturuhusiwi kuoa Washana na.......?

Badala ya kutupa sababu kwanini iwe hivyo, wanaishia kutuambia madhara endapo utakaidi!

Tuambieni tujue nini sababu za kauli hii..
 
Kwanza Washana sio kabila bali ni ukoo ndani ya kabila la Wapare. And for your information, Washana ndio ukoo tajiri kuliko koo zote za kabila la Wapare. Source ya utajiri wao ni biashara ya chuma waliokuwa wakifanya kabla ya kuja kwa Wakoloni. Kwa mfumo wa 'Barter Trade' waliwauzia Wachagga, Wamasai, Wasambaa, Wakamba na Wataita zana za chuma kama Mikuki, mishale, visu, mapanga na kadhalika. In return, walipata ngo'mbe, mbuzi, kondoo, vyakula(hasa wakati wa njaa) na kadhalika. Hali hii imewafanya Washana kuongoza katika kabila la Wapare kwa mifugo mingi na uwezo mkubwa wa kibiashara hadi hivi leo.

Kihistoria, koo zingine za kipare zilishindwa kuoa mabinti wa Kishana kwa sababu tayari mabinti hao walishazoea maisha fulani ya class ya juu tokea wakiwa kwao na wazazi wao hali iliyosababisha vijana wa koo zingine za Kipare kushindwa kuhimili mahitaji ya mabinti wa Kishana hasa ikizingatiwa kwamba koo hizi za kipare hazikuwa na uwezo mkubwa wa mali kama wa koo ya Washana. Hali hii ilisababisha vijana wa koo zingine za Kipare waliooa mabinti wa Kishana kushindwa kukuza uwezo wao wa kumiliki mali kwa sababu ya kutumia akiba kubwa ya mali yao kuwalea wake zao wa kishana.

Kwasababu hiyo, simulizi zimeendelea hadi leo hii kuwa Wanawake wa Kishana ni Mlango wa nane! Ikumbukwe kuwa, kasumba hii ni ya kawaida kwa binadamu.... Mwanaume yeyote yule asingependa kuoa mwanamke mwenye matumizi makubwa kuliko uwezo wa mwanaume kumlisha. Nijuavyo mimi hili ni jambo la zamani ila kwa maisha ya zama hizi hali-apply tena. Kwahiyo, washana wanaolewa tu kama kawaida siku hizi na waliowaoa wana maisha mazuri tu.

Kwa upande wa Tanga, Wabondei ndio wanaojulikana kama mlango wa nane. Kasumba hii ya kuwaita Wabondei mlango wa nane ilienezwa na Wasambaa kwasababu wanawake wa Kibondei ni Wavivu na wanajua sana kutumia kuliko kutafuta hali inayosababisha mwanaume kutumia nguvu nyingi kumlea.

Hadi hivi leo Wasambaa hawaruhusiwi kuoa wanawake wa kibondei na wanaowaoa hufanya hivyo ki-ubishi tu. Imani hii dhidi ya Wabondei ilienea hadi kwa Wapare, Wachagga, Wazigua na Wadigo tokea long time.

Likewise, hizi ni simulizi za kale, and by now hazina nafasi kabisa, wanawake wa Kibondei wanaolewa tu kama kawaida siku hizi na waliowaoa wana maisha mazuri tu.
 
Mimi niliambiwa na wapare washana wana laana fulani ukiwa binti toka ukoo wa mshana anaweza kukuua au ukiwa na mali atafanya mpango wa kuziamishia kwao.Ukoo wa mshana ni hatari umejaa mikosi na mabala.

NB Mimi si Mpare ila nimepewa simulizi na wapare wenyewe. Wana Ukoo wa mshana siku hizi wengi wamebadilisha majina ya Ukoo ili kukwepa kuzodolewa na Koo nyingine.Mfano Ukoo wa Masumai asili yake ni Ukoo wa Mshana baada ya kuona mabinti zao wanakimbiwa hawapati ndoa wazee wakaketi chini na kubadilisha jina la Ukoo ili kuondokana na laana za washana.
 
Mimi niliambiwa na wapare washana wana laana fulani ukiwa binti toka ukoo wa mshana anaweza kukuua au ukiwa na mali atafanya mpango wa kuziamishia kwao.Ukoo wa mshana ni hatari umejaa mikosi na mabala.

NB Mimi si Mpare ila nimepewa simulizi na wapare wenyewe.Wana Ukoo wa mshana siku hizi wengi wamebadilisha majini ya Ukoo ili kukwepa kuzodolewa na Koo nyingine.Mfano Ukoo wa Masumai asili yake ni Ukoo wa Mshana baada ya kuona mabinti zao wanakimbiwa hawapati ndoa wazee wakaketi chini na kubadilisha jina la Ukoo ili kuondokana na laana za washana.
Inawezekana swali nililimuuliza @Hardwood jibu lake likawa hili ulilozungumza hapa
 
Kwanza Washana sio kabila bali ni ukoo ndani ya kabila la Wapare. And for your information, Washana ndio ukoo tajiri kuliko koo zote za kabila la Wapare. Source ya utajiri wao ni biashara ya chuma waliokuwa wakifanya kabla ya kuja kwa Wakoloni. Kwa mfumo wa 'Barter Trade' waliwauzia Wachagga, Wamasai, Wasambaa, Wakamba na Wataita zana za chuma kama Mikuki, mishale, visu, mapanga na kadhalika. In return, walipata ngo'mbe, mbuzi, kondoo, vyakula(hasa wakati wa njaa) na kadhalika. Hali hii imewafanya Washana kuongoza katika kabila la Wapare kwa mifugo mingi na uwezo mkubwa wa kibiashara hadi hivi leo.

Kihistoria, koo zingine za kipare zilishindwa kuoa mabinti wa Kishana kwa sababu tayari mabinti hao walishazoea maisha fulani ya class ya juu tokea wakiwa kwao na wazazi wao hali iliyosababisha vijana wa koo zingine za Kipare kushindwa kuhimili mahitaji ya mabinti wa Kishana hasa ikizingatiwa kwamba koo hizi za kipare hazikuwa na uwezo mkubwa wa mali kama wa koo ya Washana. Hali hii ilisababisha vijana wa koo zingine za Kipare waliooa mabinti wa Kishana kushindwa kukuza uwezo wao wa kumiliki mali kwa sababu ya kutumia akiba kubwa ya mali yao kuwalea wake zao wa kishana.

Kwasababu hiyo, simulizi zimeendelea hadi leo hii kuwa Wanawake wa Kishana ni Mlango wa nane! Ikumbukwe kuwa, kasumba hii ni ya kawaida kwa binadamu....mwanaume yeyote yule asingependa kuoa mwanamke mwenye matumizi makubwa kuliko uwezo wa mwanaume kumlisha. Nijuavyo mimi hili ni jambo la zamani ila kwa maisha ya zama hizi hali-apply tena. Kwahiyo, washana wanaolewa tu kama kawaida siku hizi na waliowaoa wana maisha mazuri tu.

Kwa upande wa Tanga, Wabondei ndio wanaojulikana kama mlango wa nane. Kasumba hii ya kuwaita Wabondei mlango wa nane ilienezwa na Wasambaa kwasababu wanawake wa Kibondei ni Wavivu na wanajua sana kutumia kuliko kutafuta hali inayosababisha mwanaume kutumia nguvu nyingi kumlea. Hadi hivi leo Wasambaa hawaruhusiwi kuoa wanawake wa kibondei na wanaowaoa hufanya hivyo ki-ubishi tu. Imani hii dhidi ya Wabondei ilienea hadi kwa Wapare, Wachagga, Wazigua na Wadigo tokea long time. Likewise, hizi ni simulizi za kale, and by now hazina nafasi kabisa, wanawake wa Kibondei wanaolewa tu kama kawaida siku hizi na walio waoa wana maisha mazuri tu.
Mkuu nimekukubali,content yako imejaa logics na facts na umeipeleka kwa mtiririko unaoeleweka.Nami pia nilikuwa nikiambiwa tahadhari hii na nilipata kumuuliza mzee mmoja wa siku nyingi na muelewa kule ugweno akanipa vipande kama vilivyomo hapo kwako.Embu fanya ututafutie kuhusu wamachame na wakibosho nao mpaka recently walikuwa hawaoleani issue ni nini?
 
Kwanza Washana sio kabila bali ni ukoo ndani ya kabila la Wapare. And for your information, Washana ndio ukoo tajiri kuliko koo zote za kabila la Wapare. Source ya utajiri wao ni biashara ya chuma waliokuwa wakifanya kabla ya kuja kwa Wakoloni. Kwa mfumo wa 'Barter Trade' waliwauzia Wachagga, Wamasai, Wasambaa, Wakamba na Wataita zana za chuma kama Mikuki, mishale, visu, mapanga na kadhalika. In return, walipata ngo'mbe, mbuzi, kondoo, vyakula(hasa wakati wa njaa) na kadhalika. Hali hii imewafanya Washana kuongoza katika kabila la Wapare kwa mifugo mingi na uwezo mkubwa wa kibiashara hadi hivi leo.

Kihistoria, koo zingine za kipare zilishindwa kuoa mabinti wa Kishana kwa sababu tayari mabinti hao walishazoea maisha fulani ya class ya juu tokea wakiwa kwao na wazazi wao hali iliyosababisha vijana wa koo zingine za Kipare kushindwa kuhimili mahitaji ya mabinti wa Kishana hasa ikizingatiwa kwamba koo hizi za kipare hazikuwa na uwezo mkubwa wa mali kama wa koo ya Washana. Hali hii ilisababisha vijana wa koo zingine za Kipare waliooa mabinti wa Kishana kushindwa kukuza uwezo wao wa kumiliki mali kwa sababu ya kutumia akiba kubwa ya mali yao kuwalea wake zao wa kishana.

Kwasababu hiyo, simulizi zimeendelea hadi leo hii kuwa Wanawake wa Kishana ni Mlango wa nane! Ikumbukwe kuwa, kasumba hii ni ya kawaida kwa binadamu....mwanaume yeyote yule asingependa kuoa mwanamke mwenye matumizi makubwa kuliko uwezo wa mwanaume kumlisha. Nijuavyo mimi hili ni jambo la zamani ila kwa maisha ya zama hizi hali-apply tena. Kwahiyo, washana wanaolewa tu kama kawaida siku hizi na waliowaoa wana maisha mazuri tu.

Kwa upande wa Tanga, Wabondei ndio wanaojulikana kama mlango wa nane. Kasumba hii ya kuwaita Wabondei mlango wa nane ilienezwa na Wasambaa kwasababu wanawake wa Kibondei ni Wavivu na wanajua sana kutumia kuliko kutafuta hali inayosababisha mwanaume kutumia nguvu nyingi kumlea. Hadi hivi leo Wasambaa hawaruhusiwi kuoa wanawake wa kibondei na wanaowaoa hufanya hivyo ki-ubishi tu. Imani hii dhidi ya Wabondei ilienea hadi kwa Wapare, Wachagga, Wazigua na Wadigo tokea long time. Likewise, hizi ni simulizi za kale, and by now hazina nafasi kabisa, wanawake wa Kibondei wanaolewa tu kama kawaida siku hizi na walio waoa wana maisha mazuri tu.
Umeelezea vizuri sana mkuu...nikamkumbuka Prof Mshana wa Chuo Kikuu DSM
 
Sorry mkuu can u tell me somthing about Wagweno?
 
Wagweno ni Wapare wenye asili ya Kichagga. Wagweno ni Bilingual (i.e., wanaongea lugha mbili yaani Kigweno ambacho kinafanana sana na Kichagga cha Marangu-Mwika na vilevile wanongea Kipare). Kabla ya zama za ukoloni, eneo la Uchaggani lilikuwa lilikuwa ndio eneo lenye vita vingi kuliko maeneo yote ya Kaskazini. Hii ilisababisha baadhi ya wachagga kulikimbia eneo hilo na kuhamia maeneo ya Jirani.

Notable wars ambazo zilizalisha zilikuwa tatu:

1. Upareni na Taita/Taveta ambako wakimbizi wa Kichagga walikimbilia kutokana na vita vya Wamarangu na Warombo na vilevile vita vya Wa-oldmoshi/Wauru na Wakibosho vilizalisha wakimbizi wa Kichagga waliokimbilia katika maeneo haya.

2. Meru ambako wakimbizi wa Kichagga walikimbilia kutokana na vita vya Wakibosho na Wamachame/Wasanyajuu/Wasiha. Kitamaduni na kilugha Wameru wanashahibiana sana na Wasiha na Wasanyajuu na Wamachame. Mpaka leo hii Wameru (Jina lao halisi ni Wa-roh) na Wachagga wa sehemu hizi wanasikiliza vizuri sana hata kama kila mtu atazungumza lugha yake.

Ikumbukwe kuwa Wakibosho ndio walikuwa wababe wa vita hii na mkoloni wa Kijerumani alivyokuja alikuta mtiti huu wa Wakibosho vs Wamachame na Wakibosho vs Wa-oldmoshi/Wauru bado unaendelea. Mjerumani akafanya collaboration na Mangi Meli wa Oldmoshi ili kum-defeat Mangi Sina wa Kibosho.

Jamii zote hizi za Kichagga ziliuziwa silaha za chuma na Wapare wa Kaskazini(notably Usangi). Wapare wa ukoo wa Washana ndio walikuwa Wahunzi wakuu katika kabila la Wapare. Neno Mshana maana yake ni Mhunzi yaani kwa kimombo blacksmith/ironsmith.

3. Vita nyingine ambayo ilizalisha wakimbizi wa Kichagga ni vita kati ya Wachagga kama unified tribe dhidi ya Wamasai. Hiyo vita ilikuwa ni ya muda mrefu kwani Wamasai wakipigwa wanarudi nyuma kufanya re-grouping na wanarudi upya kulianzisha.

Ilibidi Wachagga wachimbe mahandaki kwenye miteremko ya mlima Kilimanjaro na kuficha mali zao, wanawake na watoto, ikiwemo mifugo, ili kupunguza hasara za vita. Mahandaki haya bado yapo mpaka leo katika maeneo ya Uru, Kibosho na Oldmoshi.

Mpaka leo hii makabila yote ya kaskazini wanaikumbuka hii 'RESILIENCE' ya Wamasai kwasababu hawakuwa watu waliokubali kushindwa kirahisi.

Wamasai walikuwa wanataka maeneo ya milima yenye hali ya ubaridi kwasababu maeneo mengi ya tambarare yalikuwa na magonjwa mengi ikiwemo ndigana ambaao yalikuwa yanaua sana mifugo na binadamu. Sehemu za baridi zilikuwa hazina magonjwa haya.
 
Wagweno ni Wapare wenye asili ya Kichagga. Wagweno ni Bilingual (i.e., wanaongea lugha mbili yaani Kigweno ambacho kinafanana sana na Kichagga cha Marangu-Mwika na vilevile wanongea Kipare). Kabla ya zama za ukoloni, eneo la Uchaggani lilikuwa lilikuwa ndio eneo lenye vita vingi kuliko maeneo yote ya Kaskazini. Hii ilisababisha baadhi ya wachagga kulikimbia eneo hilo na kuhamia maeneo ya Jirani. Notable wars ambazo zilizalisha zilikuwa tatu:
1. Upareni na Taita/Taveta ambako wakimbizi wa Kichagga walikimbilia kutokana na vita vya Wamarangu na Warombo na vilevile vita vya Wa-oldmoshi/Wauru na Wakibosho vilizalisha wakimbizi wa Kichagga waliokimbilia katika maeneo haya.
2.Meru ambako wakimbizi wa Kichagga walikimbilia kutokana na vita vya Wakibosho na Wamachame/Wasanyajuu/Wasiha. Kitamaduni na kilugha Wameru wanashahibiana sana na Wasiha na Wasanyajuu na Wamachame. Mpaka leo hii Wameru(Jina lao halisi ni Wa-roh) na Wachagga wa sehemu hizi wanasikiliza vizuri sana hata kama kila mtu atazungumza lugha yake. Ikumbukwe kuwa Wakibosho ndio walikuwa wababe wa vita hii na mkoloni wa Kijerumani alivyokuja alikuta mtiti huu wa Wakibosho vs Wamachame na Wakibosho vs Wa-oldmoshi/Wauru bado unaendelea. Mjerumani akafanya collaboration na Mangi Meli wa Oldmoshi ili kum-defeat Mangi Sina wa Kibosho.

Jamii zote hizi za Kichagga ziliuziwa silaha za chuma na Wapare wa Kaskazini(notably Usangi). Wapare wa ukoo wa Washana ndio walikuwa Wahunzi wakuu katika kabila la Wapare. Neno Mshana maana yake ni Mhunzi yaani kwa kimombo blacksmith/ironsmith.

3.Vita nyingine ambayo ilizalisha wakimbizi wa Kichagga ni vita kati ya Wachagga kama unified tribe dhidi ya Wamasai. Hiyo vita ilikuwa ni ya muda mrefu kwani Wamasai wakipigwa wanarudi nyuma kufanya re-grouping na wanarudi upya kulianzisha. Ilibidi Wachagga wachimbe mahandaki kwenye miteremko ya mlima Kilimanjaro na kuficha mali zao, wanawake na watoto, ikiwemo mifugo, ili kupunguza hasara za vita. Mahandaki haya bado yapo mpaka leo katika maeneo ya Uru, Kibosho na Oldmoshi. Mpaka leo hii makabila yote ya kaskazini wanaikumbuka hii 'RESILIENCE' ya Wamasai kwasababu hawakuwa watu waliokubali kushindwa kirahisi. Wamasai walikuwa wanataka maeneo ya milima yenye hali ya ubaridi kwasababu maeneo mengi ya tambarare yalikuwa na magonjwa mengi ikiwemo ndigana ambayao yalikuwa yanaua sana mifugo na binadamu. Sehemu za baridi zilikuwa hazina magonjwa haya.
MKUU UKO VIZURI, UCHAMBUZi WAKO NIMEUPENDA! NAOMBA HISTORIA KUHUSU WAMARANGU NA WAROMBO ,
 
Kwanza naomba kudeclare kuwa mm ni Mpare tena Mshana . Mtoa mada amepotosha sana na nadhan anatakiwa ku edit alichoandika ili kilete maana na nashukuru mkuu @hardwood ameeleza vizuri sana.

Kwa kifupi Washana ni wafua vyuma hivyo tangu enz walikuwa matajir sana maana walikuwa wanauza chuma kwa makibila yote ya nyanda za juu kaskazini.

Ila washana wana makundi mawili;

1. Washana wenye asili ya Ugweno ambao ni wengi sana. Hawa ndio wafua vyuma japo baadae walisambaa maeneo ya Kilomeni na Usangi hasa baada ya kushindwa vita na Wachaga. Hawa ndio matajiri sana hata leo japo wachache sana ni wasomi. Wengi hupenda biashara na ufundi. Wengi sana kwa sasa wanaishi Arusha na kule wana vyama imara sana.

2. Hawa ni washana wachache sana ambao hawakujihusisha na kufua vyuma na ni maskini na washirikina sana kule upareni wanaitwa washana wawaka moto (Vashana veaka moto). Hawa ndio washana ambao koo nyingine haziruhusiwi kuoa kwao au kushirikiana kwa lolote.

Pamoja na kwamba mimi ni Mshana, lakini kwetu ni laana kushirikiana na kundi hili la washana. Kwa kule kijijini huruhusiwi hata kukaa nao ukapata kinywaji(dengelua) ni laana.
Wanawaita pia washana mlango wa nane (vashana mlango wa mnane).

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Kwanza naomba kudeclare kuwa mm ni Mpare tena Mshana . Mtoa mada amepotosha sana na nadhan anatakiwa ku edit alichoandika ili kilete maana na nashukuru mkuu @hardwood ameeleza vizuri sana. Kwa kifupi Washana ni wafua vyuma hivyo tangu enz walikuwa matajir sana maana walikuwa wanauza chuma kwa makibila yote ya nyanda za juu kaskazini. Ila washana wanamakundi mawili1 Washana wenye asili ya ugweno ambao ni wengi sana hawa ndio wafua vyuma japo baadae walisambaa maeneo ya Kilomeni na usangi hasa baada ya kushindwa vita na Wachaga. Hawa ndio matajir sana hata leo japo wachache sana ni wasomi. Wengi hupenda biashara na ufundi. Wengi sana kwa sasa wanaishi Arusha na kule wana vyama imara sana. 2 Hawa ni washana wachache sana ambao hawakujihusisha na kufua vyuma na ni maskini na washirikina sana kule upareni wanaitwa washana wawaka moto. ( Vashana veaka moto) hawa ndio washana ambao koo nuingine haziruhusiwi kuoa kwao au kushirikiana kwa lolote. Pamoja na kwamba mm ni mshana lakin kwetu ni laana kushirikiana na kundi hili la washana kwa kule kijijin huruhusiwi hata kukaa nao ukapata kinywaji(dengelua) ni laana. Wanawaita pia washana mlango wa nane( vashana mlango wa mnane).

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Nimekaa sana kule ila sijawahi ona hawa Washana wakitengwa hivi japo story hizi nilizisikia
 
Back
Top Bottom