Wapangaji waijulishe TRA kuwa nyumba si zao ili TRA isifanye kosa kuwatoza kodi ya jengo

Yani kuhangaika kote Huku ni kwasababu ya 1000 tu kwa mwezi?
Tunalalamika mno vitu vya kipuuzi ndio maana tukiwa na malalamiko ya msingi serikali haiyatilii maanani maana imetuzoea ni wapayukaji hovyo.
Huyo mpangaji atakayegombana na mwenye nyumba kwasababu ya 1000 atakuwa juha

Hiyo 1,000 moja, vat kwenye umeme, ewura. Kuna ya tozo za miamala, kuna parking, kuna mafuta ya gari, kuna maongezeko lukuki na yatokanayo na maongezeko ya mafuta, kuna mafuta ya kupikia, sukari, ada, into Shirikishi, kuna Corona biashara hamna, ukiugua utalipa, paye, nk.

Ni uzwazwa uliopitiliza kudhani hii ni 1,000 tu kwa mwezi.

Kwani wanaopeana takrima za majumba na magari walipoaminishwa siyo sisi?

Vipi mapato yao wanalipa kodi?
 
Ili kuondoa mgogoro kati ya mwenye nyumba na mpangaji TRA iwatake wapangaji wapeleke namba zao za mita na kuiwezesha TRA iwaondoe kwenye kulipishwa kimakosa. Hata hivyo tatizo litabaki pale mwenye nyumba na mapangaji wanatumia mita moja ambapo mwenye nyumba atalazimisha wapangaji walipe kodi ya jengo.
Kwanini wasioanishe jana la mwenye nyumba na jana la mwenye luku badala ya kutengeneza misongamano tra na hii mikorona
 
Mimi nadhani muhimu watueleze hao waliolipishwa kimakosa watarudishiwa pesa yao au nayo Mwigulu ataitangaza kwenye mafanikio ya makusanyo!
 
Ili kuondoa mgogoro kati ya mwenye nyumba na mpangaji TRA iwatake wapangaji wapeleke namba zao za mita na kuiwezesha TRA iwaondoe kwenye kulipishwa kimakosa. Hata hivyo tatizo litabaki pale mwenye nyumba na mapangaji wanatumia mita moja ambapo mwenye nyumba atalazimisha wapangaji walipe kodi ya jengo.
Kuna kodi ya rent hapo inakuja
 
Mfano kuna nyumba huku Kisasa -Dodoma ilikuwa guest house inavyumba 15na ina mita moja na wapangaji tuu!Kodi hii lazima wanaibeba wapangaji!
 
TRA wamefafanua vizuri,kuwa kodi ya majengo ni jukumu la mwenye nyumba kulipa,mwenye nyumba na mpangaji (anayelipa kodi kupitia kwenye luku),waingie makubaliano ya kukatana kiasi kilicholipwa kupitia umeme wa luku,kwenye kodi ya nyumba.TRA wamefafanua vizuri kuwa ,kwa nyumba yenye frame au apartment nyingi,mwenye nyumba aende TRA na orodha ya mita za kwenye nyumba hiyo na kuchagua mita moja itakayotumika kulipia kodi ya majengo.Leo nimesikia kwa watu wa vijijini au nyumba za nyasi hawalipi kodi ya majengo kwa hivi sasa na wazee wenye umri wa miaka 60 (na kuendelea ) waende TRA kuomba msamaha wa kodi ya majengo kwa nyumba moja wanayoishi wao wenyewe.Ninadhani kwa wapangaji wa naoishi nyumba moja na baba/mama mwenye nyumba(Kama atakuwa bado kufika 60 walifuzu kusemehewa)basi busara itumike,wapangaji wachangie gharama za umeme tu(baada ya kuondoa kodi ya jengo) ambayo atalipa mwenye nyumba mwenyewe.Watu wanaopanga nyumba mzima kwa fedha kubwa,sidhani Kama ndiyo hawa wanaolalamika ongezeko la shs12,000 kwa mwaka.Lakini yote kwa yote TRA wameshatolea ufafanuzi suala lao.
 
Serikali haiendeshi mambo yake kwa kutolea ufafanuzi, serikali huendesha mamno yake kwa sheria na kanuni tu. Aliyetunga sheria ni serikali TRA na Tanesco ni wakusanyaji tu hivyo ufafanuzi wao si sheria, serikali ndiyo inayotakiwa kuweka mwongozo wa kisheria wa nani anatakiwa alipe na si kuwaambia wenye nyumba na wapangaji watumie busara ya nani alipe! Nyumba yako lipa mwenyewe kodi ya jengo. Kuna kila dalili kuwa serikali haikutarajia kukutana na hiki kinachoendelea, wao walijua watanzania wanyonge watalipa tu bila kuhoji, hawajui kuwa kuna watu hununua umeme wa sh. Elfu moja 1,000/= hivyo kwa hali hii hawawezi kuupata.
 
Yani kuhangaika kote Huku ni kwasababu ya 1000 tu kwa mwezi?
Tunalalamika mno vitu vya kipuuzi ndio maana tukiwa na malalamiko ya msingi serikali haiyatilii maanani maana imetuzoea ni wapayukaji hovyo.
Huyo mpangaji atakayegombana na mwenye nyumba kwasababu ya 1000 atakuwa juha
Acha bana, buku kwa mtanzania wa huku vijjini ni hela.
 
Tukiambiwa tunaishi in a shit hole country tunaona kama tunaonewa,TRA kujihusisha na kukusanya mapato ya kodi hii ambayo ni wajibu wa serikali za mitaa
Haya mapato yamekua yakikusanywa na TRA kama hujui unakaa kimya
 
TRA ina mambo ya ajabu ajabu, TRA imekuwa ikiwalipisha wapangaji Withholding Tax, kodi hii ni ya jengo ambayo inatakiwa ilipwe na mwenyenyumba lakini pamoja na kumjua mwenye nyumba TRA inasema ni rahisi kwao kuikusanya toka kwa mpangaji kisha mpangaji amdai mwenyenyumba! Hii ni Tanzania. Mwezi uliopita serikali ilijisifu kukusanya mapato ya mabavu ambayo sasa yamepunguzwa japo waliolalamika na kulipishwa hawatarudishiwa kiasi kilichozidi kwenye malipo ya lazima.
TRA inawajua wenyenyumba iwatake wao wawasilishe TRA namba za mita zao badala ya kuwatska wapangaji.
 
Haya mapato yamekua yakikusanywa na TRA kama hujui unakaa kimya
Wewe ni middle class mpumbavu,next time soma kwanza ili uelewe then jibia kama unataka kujibia,ukinisoma vizuri hapo juu sikua na maana ya kusema hizi kodi TRA ilikua haikusanyi NIA yangu ni kutaka kutambulisha vikodi hivi vikusanywe kama sehemu ya mapato kwa local governments,TRA wajihusishe na kodi kubwa
 
Tumia kichwa kufikiri, kwanini nilipie sh.1,000/= wakati nyumba si ya kwangu? Wewe unaona hiyo hela ni ndogo wakati wenzako hawana sh 400/= ya kupandia daladala hivyo wanatembea kwa mguu toka Ubungo (kama unaifahamu) mpaka Magogoni (kama unakufahamu) Dar. Ukiona watu wamejipanga kwenye misikiti ya wahindi siku za Ijumaa usiwacheke, ni umasikini walioupata ndani ya Uhuru.
Elfi moja ina kuuma!
Uharibifu mnaotufanyia kwenye nyumba huuoni
 
Back
Top Bottom