Wapangaji waijulishe TRA kuwa nyumba si zao ili TRA isifanye kosa kuwatoza kodi ya jengo

Yani kuhangaika kote Huku ni kwasababu ya 1000 tu kwa mwezi?
Tunalalamika mno vitu vya kipuuzi ndio maana tukiwa na malalamiko ya msingi serikali haiyatilii maanani maana imetuzoea ni wapayukaji hovyo.
Huyo mpangaji atakayegombana na mwenye nyumba kwasababu ya 1000 atakuwa juha
Umesema kweli tupu.
 
Wewe ni tajiri na haujui kuna watu mchana huu hawatakua na sh. 1,000/= ya kununua unga wa dona wale na watoto wao. Kumbuka unapotoa sh.1,000/= kununua umeme utakatwa hivyo utapata uniti pungufu zaidi na kusababisha mzunguko wa kununua umeme uwe karibu karibu. Ni vizuri kama wewe ni tajiri pita pembeni waachie masikini walilie ugali bila mboga.
Ukiwa washindwa na elfu moja ya unga wa dona,utaweza kupangisha nyumba yenye umeme,ambayo nina hakika nyumba nzima,kama Dar kwa mwezi ni laki sita.Huyo wa kukosa elfu ya unga wa dona ni wakuishi nyumba ya chumba elfu tano na bila ya umeme na ni nje ya mji.
 
Tumia kichwa kufikiri, kwanini nilipie sh.1,000/= wakati nyumba si ya kwangu? Wewe unaona hiyo hela ni ndogo wakati wenzako hawana sh 400/= ya kupandia daladala hivyo wanatembea kwa mguu toka Ubungo (kama unaifahamu) mpaka Magogoni (kama unakufahamu) Dar. Ukiona watu wamejipanga kwenye misikiti ya wahindi siku za Ijumaa usiwacheke, ni umasikini walioupata ndani ya Uhuru.
Huyo anayeshindwa kulipa umeme wa elfu,sio mpamgaji wa nyumba nzima,labda ni mpangaji wa chumba cha elfu tano,na itakuwa nyumba ina vyumba kumi,wakichangishana kulipia umeme,itakuwa kila mwenye chumba katoa shilingi mia kwa mwezi,sasa hapo ikiwa ameshindwa kulipa mia ya kila mwezi,atafute nyumba isikokuwa na umeme,apangishe.
 
Ukiwa washindwa na elfu moja ya unga wa dona,utaweza kupangisha nyumba yenye umeme,ambayo nina hakika nyumba nzima,kama Dar kwa mwezi ni laki sita.Huyo wa kukosa elfu ya unga wa dona ni wakuishi nyumba ya chumba elfu tano na bila ya umeme na ni nje ya mji.
Nyie matajiri wa Sinza hamjui kuna watu wanishi nyumba zenye umeme lakini wao hawautumii.
 
Tanesco haihusiki na kodi hii, Tanesco ni kama wakala tu wa kukusanya, mhusika ni TRA.
Tanesco wala sio wakala yeye kazi yake kupokea malipo ya bill tu asijipe kazi ya ziada bill huko ndani kuna nini si yake. Bill yasomeka jina la mwenye nyumba yatosha
 
Kwanza tu ni kuweke sawa ni kuwa wewe ni mnafiki wa wazi kabisa.

Katika swala dogo kama hili umeshindwa kujua nan adui na nani mwenzako usimame nae katika kupambania haki ambayo wewe inakuhusu.

Nadhani unakumbuka ile hadithi ya mtego wa panya ulioua kuku, mbuzi, kondoo na ng'ombe na panya ambaye ndie muhusika wa mtego akapona. Lakini panya huyo huyo aliwaonya na kuwashirikisha hawa wanyama wakubwa wamsaidie na walikataa wakiamini huo mtego wa panya hauwahusu.

Anyways kama hauifahamu hiyo story hebu nenda kaitafute uisome uielewe. Utapata ujumbe.

Wewe raia wenzako wanalalamika kunyanyaswa wewe unatetea bila hata chembe ya huruma. Mbona hauna upendo na watanzania wenzako?!

Unakuwa kama Job ndugai akikaa kwenye kiti kile cha uspika anajibu majibu utadhani yeye anamiliki hii Dunia. Acha dharau.

Kama 1000 kwako ni ndogo kuna wenzako wanaitafuta kwa shida sana na hawapo tayari kunyang'anywa hiyo 1000 kiuonevu kwa kisingizio cha sijui kuchangia kodi ya nini sijui. Ni upumbavu.

Hebu jaribu kuwa muungwana wewe.
Haifiki elfu moja kwa wanaopangisha chumba chumba,katika nyumba za kupanga,nyingi zina vyumba zsidi ya kumi,kila mpangaji akichangia umeme kila mwezi,atakuwa amelipa haiziidi shilingi mia.
 
Ili kuondoa mgogoro kati ya mwenye nyumba na mpangaji TRA iwatake wapangaji wapeleke namba zao za mita na kuiwezesha TRA iwaondoe kwenye kulipishwa kimakosa. Hata hivyo tatizo litabaki pale mwenye nyumba na mapangaji wanatumia mita moja ambapo mwenye nyumba atalazimisha wapangaji walipe kodi ya jengo.
Sijui kwanini tunakimbiliaga mambo haya bila kujipanga kisawasawa..
 
Wew unaoongea tu.. kuna mtu ana anamiliki nyumba nyumba kila chumba kina mita yake.. kwa mfano kuna vyumba kumi.. huoni kama kuna 10000/= apo lazima TRA wapite nayo.. mfumo wao na wa hovyo tu kuna miingiliano mingi sana kwenye hili
Hakuna nyumba kila chumba kina mita yake,labda frem za biashara,na hakuna mfanyabiashara anayeshindwa kulipa elfu kwa mwezi.
 
Hii na me niliwaza.. katika kodi ikatwe hiyo 12000/= ambayo ni ya miez 12. Ishu iko kwenye hizi nyumba zenye mita zaidi ya moja.. kuna nyumba inamiliki mita hata 5. Hili inabidi mwenye nyumba kwa hali ya haraka aliport mahala husika isajiliwe nyumba 1 zilizobaki zitolewe katika mfumo haina kutia uvivu maana itakula kwake pale wapangaji watapompa kodi wakiwa wamekata na kodi ya jengo.. let say una mita 5 ×12000=60000 matokeo yako wazi kabisa
Mwenye nyumba anawahi kulipa kawaida kila mwanzo wa mwaka,hawezwi kukatwa hizo pesa.Wapo waliokwishalipa kwa njia za kawaida sio za luku,hawakatwi kwenye luku.
 
Yani kuhangaika kote Huku ni kwasababu ya 1000 tu kwa mwezi?
Tunalalamika mno vitu vya kipuuzi ndio maana tukiwa na malalamiko ya msingi serikali haiyatilii maanani maana imetuzoea ni wapayukaji hovyo.
Huyo mpangaji atakayegombana na mwenye nyumba kwasababu ya 1000 atakuwa juha
We jamaa sio wote mnashea nyumba za kupanga kuna watu wamepanga migorofa harifu
 
Ili kuondoa mgogoro kati ya mwenye nyumba na mpangaji TRA iwatake wapangaji wapeleke namba zao za mita na kuiwezesha TRA iwaondoe kwenye kulipishwa kimakosa. Hata hivyo tatizo litabaki pale mwenye nyumba na mapangaji wanatumia mita moja ambapo mwenye nyumba atalazimisha wapangaji walipe kodi ya jengo.
Serkali iagize kwamba!;
KODI YA JENGO NI KWA MWENYE JENGO TU!
MPANGAJI HAHUSIKI!
Hivo mpangaji na mwenye jengo wakubaliane jinsi ya kurudishiana makato aliyo katwa mpangaji kwa ajili ya kulipia jengo!
 
Tumia kichwa kufikiri, kwanini nilipie sh.1,000/= wakati nyumba si ya kwangu? Wewe unaona hiyo hela ni ndogo wakati wenzako hawana sh 400/= ya kupandia daladala hivyo wanatembea kwa mguu toka Ubungo (kama unaifahamu) mpaka Magogoni (kama unakufahamu) Dar. Ukiona watu wamejipanga kwenye misikiti ya wahindi siku za Ijumaa usiwacheke, ni umasikini walioupata ndani ya Uhuru.

Sidhani umeelewa point ya jamaa. Na mifano yako ni irrelavant ukiilinganisha na anachosema. Anakwambia, mtu anakipa kodi ya lakini 4 kwa mwezi na anatumia umeme wa laki 2 kwa mwezi - huyo ndio agombane na mwenye nyumba kuhusu 1,000 katika mwezi huo mmoja?? Sasa wewe unazungumzia anayekosa 400 ya nauli. Mbona husemi mtu huyo amepanga nyumba bei gani na anatumia umeme kiasi gani kwa mwezi??? Hapo ndio kungekuwa na ulinganifu.

Huwezi kukinganisha chungwa na embe ukasema chungwa tamu! Unalinganisha chungwa la Tanga na la Ukerewe!!
 
Back
Top Bottom