Wapangaji wa nyumba dar kama wana wa israel nyikani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapangaji wa nyumba dar kama wana wa israel nyikani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ninja, Mar 30, 2010.

 1. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  Wapangaji nyumba Dar kwa kuhama hama.

  Wakuu heshima kwa wingi kwenu. Jamani naomba mtazame mfano wa jamaa huyu kwa jina la mpangaji nyumba Dar es Salaam ambaye anawakilisha wengi wa wapangaji nyumba walioko jijini, hasa wafanyakazi. Mpangaji huyu ana familia yenye mwenzi na watoto.

  2000 tandale chumba kimoja, 2001 temeke chumba na sebule choo cha kushea, 2002 sinza chumba na sebule self contained miezi sita, halafu miezi sita mingine Mwananyamala upande, 2003 mabibo upande miezi sita halafu miezi sita mingine changanyikeni chumba na sebule, 2004 tabata vyumba viwili na sebule, 2005 magomeni nyumba nzima, 2006 mbagala kizuiani amehamia kwake lakini hajapaua, 2007 mbagala kumemshinda kapangisha na yeye kaenda kupanga kimara upande, 2008 mbezi beach nyumba nzima anapangiwa na shirika mambo mazuri, 2009 kahamia kwake boko, 2010 Boko kumemshinda kapangisha nyumba yake na yeye karudi sinza na familia yake kupanga kwenye vyumba viwili na sebule self. Loh.

  Hivi huu mzunguko ni vipi na mwisho wake ni nini.
   
 2. G

  Generator New Member

  #2
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hayo ni maisha tu kaka, live where u feel confortable, majirani wakikuboa.. afadhali uanze.
   
 3. N

  Nanu JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mwisho wake nyumba yake ya milele!!!
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha Ninja umenichekesha huoni kutoka 2000 mpaka 2002 aliweza kuhama na kuingia self container badala ya room moja
   
 5. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #5
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii sredi nilifikiri Ingeongelea jinsi mpangaji anavyotoa hela yake kumlipa mwenye nyumba halafu inabidi awe anamnyenyekea mwenye nyumba. Yaani mwenye nyumba anamuona mmpngaji kana kwamba isingekua yeye huyu mpangaji asingekua na maisha!!! too sad kwa sisi wapangaji. Ndo maana kuna watu wameamua kuishi kwao Kiluvya lakini ofisi ziko posta.
  Asubuhi kila siku wanakutana na kibao karibu Dar Es salaam Jioni Kibao kwaheri Dar Es salaam. jamani msicheki. wenye nyumaba nomaaaa!!
   
 6. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Baada ya mizunguko yoooote hii mwishowe AKISHA KUSITAAFU tu atarudi kweye moja ya nyumba yake ya MBAGALA KIZUIANI AU BOKO kusubiri kupata nyumba yake ya milele kwa maana uwezo wa kulipia hata hicho chumba kimoja utakwisha au kupungua akisha kustaafu kazi
   
 7. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Full kimasai,yaani Normadic life kwa kwenda mbele!!
   
 8. l

  lagusya Member

  #8
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 26, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kweli huyo keshazoea kuhama hama,kwangu mimi kazi ya kuhama naona ni ngumu sana,nikifikiria kupaki vitu na kuvipanga tena
   
 9. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145

  kiluvya ni dar es saalam mkuu mail moja mpakani ndo kunakibao darajani pale kwako ni kwako tu nyumba za kupanga kero asa ukute ya choo cha kushea da yani usiombe yakukute yalonikutaga umebanwa na haja kubwa na mtu yuko ****** unabana kila stail unaomba kila maombi jamaa atoki na akuna mbadala mpaka unawekeana bifu na jamaa du
   
 10. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ila hii imekaa mvurugiko sana maana kawaida mtu anaanza room 1 kisha chumba na sebeule halafu huyoo anahamia kwake au wengine wanapanga nyumba nzima lkn huyu eeh shughuli!
   
 11. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,464
  Likes Received: 1,410
  Trophy Points: 280
  mkuu hiyo red si mchezo
   
 12. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  Huyo pengine ana afadhali, nina mdingi wangu mmoja yeye hajawahi kupanga tangu enzi za ujana wake wote, alijaliwa kuwa na mijumba tele. Baadaye alikuja kupata kimwana akamwendesha, akauza nyumba zote. Hakupanga ujanani amekuja kupanga uzeeni.

  Huyu naye mwisho wake ni vipi?
   
 13. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  Drphone hii ni kali, hivi kama ndio umekutana na dodo la buguruni halafu linakata tumboni sasa inakuaje. Maana ukipumua tu mafuriko. Yaani sijui utabana pumzi!
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Mar 31, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Sio wote wanaoweza kufuata trend hiyo hapo, wengi wetu tupo kama huyo jamaa hapo juu!
   
 15. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  Duh hii kali.
   
 16. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33

  Huyo tunafanana fanana.......mie sehemu nyingine nimekaa wiki moja tu nikahama. 2009 Mwenge Dar, 2009 Buguruni Dar, 2009 Jangwani Dar, 2009 Kibera Slums Nairobi, 2009 Muthaiga Nairobi, 2009 Kinyerezi Dar,2010 January Ukonga madafu Dar, 2010 February mwenge Singida, 2010 March Kasozi Kampala....KOOTE HUKO CHUMBA KIMOJA CHOO CHA KUSHEA FAMILIA KAMA KUMI HIVI PAMOJA NA ZAMU ZA KUFAGIA NA KUDEKI, NA CHABO KIBAO TU. Ndiyo maana location yangu imebidi iwe hivyo unavyoiona.

  Baada ya pasaka narudi Dar, kuhakikisha safari hii wananchi ndiyo tunaweka serikali madarakani na siyo mafisadi. 'you will see'. Naomba unitafutie chumba kimoja na choo cha kushea Manzese sisi kwa sisi, mi sina hela ya kupanga nyumba kubwa, nina hela ya uchaguzi tu. Mtanzania halisi, pesa ya uchaguzi ipo, ya afya hakuna.

  Unaona sasa kwa nini tunalazimika kuhama mara kwa mara!
   
 17. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  akashube chumba umepata, lakini siyo manzese sisi kwa sisi, huko kumejaa, tutakupatia chumba kimoja cha kushea watu wawili manzese darajani, bei laki mbili unusu kwa mwezi (250,000/=). Sawa tu na mshahara wa kima cha kati, ingawa nasikia unalipwa 180,000/= kwa mwezi. Usijali chukua mkopo kazini au benki au saccos.
   
 18. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kaka mimi nalipwa 85,000/= kwa mwezi, ukitoa NSSF 8,500/= nabaki na76,500/=. kampuni yetu ni ya wachina wana tenda afrika mashariki kote. Tunajitegemea kila kitu kasoro usafiri wa kikazi na hatupewi mikopo. Sasa 76,500/= inayobaki, na hivi fanilia nimeiacha nyumbani kijijini, na mimi natafuta maisha, inabidi niwe nawatumia pesa mara kwa mara, nitaishi wapi jiji la Dar.

  Ikiwa tu chumba cha kushea ni shs 250,000/= kwa mwezi. Itabidi nirudi kulala kwenye maboksi kariakoo. Hivi mnafikiri wabeba maboksi ni mbele tu peke yake, si lazima USA, siku hizi Dar maboksi kama kawa.
   
 19. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  Loh hapa akashube umenionyesha kitu kipya, wabeba maboksi ndani ya Dar?
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ninja Umenikumbusha mbali.
  Kuna mwenye nyumba wangu alikuwa ananiwekea mazingira ili niwe na mahusiano ya kimapenzi na binti yake.
  nilipokuwa sionyeshi dalili za kuwa na mpango naye akaanza kuniwekea vikwazo.
  Kama kawaida miezi sita ilipoisha nikahamia kwenye chumba kingine.
   
Loading...