Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
KIGONGO CHA BABA ASKOFU DR BAGONZA KUELEKEA KWA SPIKA WA BUNGE
Kweli common sense is not common. Ebu tufikiri pamoja:
-Wakristo tukihubiri na kuamini ufufuko, tunamaanisha haijalishi mtu alikufaje, lakini siku hiyo atafufuka.
Aliyeliwa na simba, aliyekufa na kuzikwa, aliyepotea asijulikane kazikwa wapi, na hata aliyeyeyuka na ndege iliyopotelea baharini; wote watafufuliwa.
-Mtu angedhani pamoja na kuwa hospitali zote zina taratibu za kupokea wagonjwa, lakini kuna wagonjwa wa dharula wasiopita njia ya kawaida ili wahudumiwe kuokoa maisha yao.
Hivi mbunge akiugulia safarini Dubai, analazimika kurudi DsM kupata vibali vyote aweze kutibiwa?
Bwana Yesu aliichangamotisha sheria ya torati pale alipotibu siku ya sabato na kusema sabato ni kwa ajili ya watu, si watu kwa ajili ya sabato. Hatuwezi kumwacha ng'ombe kisimani kwa sababu ya sabato.
Ugonjwa na ajali havibagui. Kaburi halibagui. Tusibaguane kwa ajili ya majanga yasiyobagua.