Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
Kuna wabunge/madiwani wapo CCM hawapendi kabisa mtindo wa chama chao wa "Penye uzia pitisha rupia". Lakini ni waoga wasio kifani. Na tuseme si wabunifu. Wanadhani wamezaliwa kuwa wabunge/madiwani kupitia CCM, na kama wakiukosa ubunge/udiwani, basi ndiyo utakuwa mwisho wao kisiasa na kimaisha.
Ushauri wa bure.
Kama unapendwa unapendwa tu. Mafisadi hawana ubavu wa kushawishi Watanzania wachukie kile wanachokipenda.
Jaribuni kuthubutu.
John Shibuda amethubutu na mumeona leo ni Mbunge wa Maswa aliyechaguliwa kwa kura nyingi.
Ezekiel Wenje naye vilevile. Alipikiwa zengwe kumpisha 'mteule wa Rais' bwana Masha. Umma ukataka kuaminishwa kwamba Wananyamagana hawahitaji mtu mwingine....wanamtaka Masha tu. Wapi?
Na hiyo ni mifano michache tu. Tunajua Fredy Mpendazoe amedhulmiwa tu. Ni Mbunge wetu halali wa Segerea.
Kwa hiyo basi, kama kuna mbunge/diwani yuko CCM na hakubaliani na mambo fulani-fulani ya CCM, ninamshauri auvae ujasiri. Ahame.
Ole Sendeka, Lukas Selelii, Mwakyembe. Acheni uoga.
Wanaume gani munakuwa waoga??