Elections 2010 Wapambanaji Halafu Waoga

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Kuna wabunge/madiwani wapo CCM hawapendi kabisa mtindo wa chama chao wa "Penye uzia pitisha rupia". Lakini ni waoga wasio kifani. Na tuseme si wabunifu. Wanadhani wamezaliwa kuwa wabunge/madiwani kupitia CCM, na kama wakiukosa ubunge/udiwani, basi ndiyo utakuwa mwisho wao kisiasa na kimaisha.

Ushauri wa bure.
Kama unapendwa unapendwa tu. Mafisadi hawana ubavu wa kushawishi Watanzania wachukie kile wanachokipenda.

Jaribuni kuthubutu.
John Shibuda amethubutu na mumeona leo ni Mbunge wa Maswa aliyechaguliwa kwa kura nyingi.

Ezekiel Wenje naye vilevile. Alipikiwa zengwe kumpisha 'mteule wa Rais' bwana Masha. Umma ukataka kuaminishwa kwamba Wananyamagana hawahitaji mtu mwingine....wanamtaka Masha tu. Wapi?

Na hiyo ni mifano michache tu. Tunajua Fredy Mpendazoe amedhulmiwa tu. Ni Mbunge wetu halali wa Segerea.

Kwa hiyo basi, kama kuna mbunge/diwani yuko CCM na hakubaliani na mambo fulani-fulani ya CCM, ninamshauri auvae ujasiri. Ahame.

Ole Sendeka, Lukas Selelii, Mwakyembe. Acheni uoga.

Wanaume gani munakuwa waoga??
 
Tutalisambaratisha kama ilivyokuwa USSR na Ugoslavia ya Zamani.

Stop anything. Chakachua kura. Tukana Chadema.

But You CAN'T stop time.

Muda unakuja ambapo CCM kitakufa.

Sasa kwanini unaomba msaada tuka CCM? ni dalili za chadema kushindwa?
 
Hajaomba msaada kasema wale walioko huko na roho zao haziko huko ccm jiungeni na timu ya ushindi. mabadiliko yaja na hamtaweza kuyazuia thru chakachuesheni!!! yatawasomba tu.
 
Sasa kwanini unaomba msaada tuka CCM? ni dalili za chadema kushindwa?
Nisikilizapo bongofleva saa zingine huwa nafikiria walichoimba sicho kile walichomaanisha; hapo ndipo huwa nafananisha ule wimbo wa Joti.... "...kelele ni nyingi pasina matendo... unaomuenesha mwenyewe kwamba wewe ndiye mwenyewe lakini mwishowe huomba msaada kwa mwenyewe...." hiyo ni tafsiri yangu fupi katika wimbo ule:smile-big:
 
Back
Top Bottom