Wapagani nasi sasa tukumbukwe Jumatatu iwe siku ya mapumziko kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapagani nasi sasa tukumbukwe Jumatatu iwe siku ya mapumziko kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 27, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wandugu,
  Kumekuwa na vuguvugu la chinichini linalofanywa na waumini wa dini ya kiislam kutaka Ijumaa nayo iwe ni siku ya mapumziko kitaifa. Kwa muda mrefu sisi wapagani tumesahaulika sana kiasi cha kuonekana kama hatupo. Jumatatu iliyopita tulifanya kikao mkoani Shinyanga ambako ndiko waliko viongozi wetu wakuu wa kitaifa. Pamoja na kujadili masuala mbalimbali kuhusu imani yetu, tulijadili kwa kina suala la kupata siku ya kupumzika ili kupata muda mzuri wa kuabudu miungu yetu. Tulikubaliana kuwa nasi tuwasilishe ombi letu serikalini la kutaka JUMATATU iwe ni siku ya mapumziko. Kwa kawaida misa zetu zinazoambatana na matambiko huwa tunazifanya siku ya Jumatatu.

  Angalizo: hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana jumuiya yetu ya wapagani ilikuwa na waumini 11,678,982. Katika kipindi cha miaka 5 iliyopita kumekuwa na ongezeko la waumini kwa wastani wa asilimia 2.7 kwa mwaka.
   
Loading...