Waooo! 'Instruction' imeshatoka na bilioni 10 imeshatua TBA. What a life style!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,873
Naomba nikupongeze sana ewe mkuu sana na kiongozi wetu rais John Pombe Magufuli. Naona sasa tender zote za ujenzi ni TBA. Ushauri na uchoraji ni BICO. Umeme na ufundi ni TEMESA! Hivyo vikampuni vingine vya ukandarasi na ushauri elekezi tupa kule kwanza vinatozatoza tu wakati hela yako haiendi bure bure!!

Naona tayari kule Ukonga mambo bwerere na fedha zote zipo TBA tayari kwa kujenga maflat ya askari kama ulivyosema utatoa "instruction" kwa chief secretary! Hakuna cha bajeti, kutangaza tenda wala nini!

Hapa kazi tu!

=======

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kukagua eneo la ujenzi wa makazi ya askari wa Magereza unaotarajiwa kuanza baada ya wiki tatu zijazo

Akizungumza na askari wa magereza kabla ya kufanya ukaguzi huo leo (Jumamosi, Desemba 24, 2016) Waziri Mkuu amesema ziara aliyoifanya leo, ni ufuatiliaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipoenda kukagua gereza hilo.

Novemba 29, mwaka huu, Rais Magufuli alifanya ziara kwenye gereza hilo na kupokea taarifa ya uhaba wa nyumba za kuishi askari wa jeshi hilo zipatazo 9,500 na akaagiza zitafutwe sh. bilioni 10 haraka ili kupunguza tatizo hilo.

Akizungumzia kuhusu ujenzi huo, Waziri Mkuu amesema amefarijika kukuta Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wako eneo la kazi na wameanza kusafisha eneo hilo.

“Nimefarijika kukuta TBA wako kazini na nimeelezwa hatua inayofuata ni upimaji wa sampuli za udongo kabla hawajaanza kujenga msingi. Nawapongeza TBA kwa kazi nzuri wanazofanya za ujenzi wa nyumba zenye viwango na kwa haraka kama tulivyoona kule Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nyumba za Magomeni Kota,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mchango uliofanywa na Serikali ya awamu ya nne katika suala la makazi ya askari kama vile wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Polisi. “Nia ya Serikali ni kuhakikisha makamanda wote wanapata nyumba nzuri ili waendelee kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa wakiwa na uhakika familia zao zimetulia kwenye makazi bora”.

Amesema katika ziara alizozifanya kwenye mikoa mbalimbali, alitembelea magereza ya Isanga, Msalato (Dodoma), Lindi, Singida na Keko (Dar es Salaam) alikuta nyumba za askari hazina viwango na kama zipo zimechakaa sana.

Mapema, akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa nyumba hizo, Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa alisema wanamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa makazi ya askari na kwamba jeshi hilo litafanya kazi zote zisizo za kitaalamu ili kuokoa fedha za Serikali na badala ya kulipwa watu binafsi, fedha hizo zitatumika kuongeza nyumba zaidi.

“Tumekubaliana na TBA kazi zote zisizohitaji utalaamu kama kufyatua matofali, kubeba mizigo au kufyeka zitafanywa na askari wetu pamoja na wafungwa ili tuokoe gharama zote hizo na badala ya kulipa watu binafsi, fedha hizo zitumike kujenga nyumba nyingine 80,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema wamejipanga kufanya kazi hizo kwa saa 24 kila siku ili kuokoa muda ambao TBA walikuwa wameuweka wa kukamilisha ujenzi ndani ya miezi minane.

Alisema wako tayari kuanzisha kambi za ujenzi kwa kutumia wafungwa na askari ili wafanye kazi zisizohitaji utaalamu na fedha zitakazopatikana, badala ya kuwalipa watu binafsi zitumike kujenga nyumba zaidi za askari.

Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBA, Bw. Baltazar Kimangano alisema wanataraji kuanza ujenzi ndani ya wiki tatu baada ya kupokea matokeo ya uchunguzi wa sampuli za udongo kutoka taasisi ya BICO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alisema wanataraji kujenga majengo (block) manne ya ghorofa sita kila moja ambayo kwa ujumla yatakuwa na nyumba 240 zenye ukubwa wa vyumba viwili vya kulala. Pia watajenga majengo (block) mengine mawili ya ghorofa sita kila moja ambayo yatakuwa na nyumba 80 zenye ukubwa wa vyumba vitatu vya kulala.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

2 MTAA WA MAGOGONI,

L. P. 3021,
11410 – DAR ES SALAAM

JUMAMOSI, DESEMBA 24, 2016
 
Naomba nikupongeze sana ewe mkuu sana na kiongozi wetu rais John Pombe Magufuli. Naona sasa tender zote za ujenzi ni TBA. Ushauri na uchoraji ni BICO. Umeme na ufundi ni TEMESA! Hivyo vikampuni vingine vya ukandarasi na ushauri elekezi tupa kule kwanza vinatozatoza tu wakati hela yako haiendi bure bure!!

Naona tayari kule Ukonga mambo bwerere na fedha zote zipo TBA tayari kwa kujenga maflat ya askari kama ulivyosema utatoa "instruction" kwa chief secretary! Hakuna cha bajeti, kutangaza tenda wala nini!

Hapa kazi tu!
umechukia?
 
PPRA na visheria vyao vya manunuzi tupa kule mara oooh tenda itangazwe miezi mitatu...mara mikataba ipitiwe na mwanasheria wa silikareee.....mara sjui vikao vipitie hakuna....nasema hakuna hapa mi ndio nampendea mzee wa kazi tu....
 
Naomba nikupongeze sana ewe mkuu sana na kiongozi wetu rais John Pombe Magufuli. Naona sasa tender zote za ujenzi ni TBA. Ushauri na uchoraji ni BICO. Umeme na ufundi ni TEMESA! Hivyo vikampuni vingine vya ukandarasi na ushauri elekezi tupa kule kwanza vinatozatoza tu wakati hela yako haiendi bure bure!!

Naona tayari kule Ukonga mambo bwerere na fedha zote zipo TBA tayari kwa kujenga maflat ya askari kama ulivyosema utatoa "instruction" kwa chief secretary! Hakuna cha bajeti, kutangaza tenda wala nini!

Hapa kazi tu!
Wewe huna ndugu anaye fanya kazi kwenye Private sector?. Ukoo wenu wote ni watumishi wa umma?
 
Naomba nikupongeze sana ewe mkuu sana na kiongozi wetu rais John Pombe Magufuli. Naona sasa tender zote za ujenzi ni TBA. Ushauri na uchoraji ni BICO. Umeme na ufundi ni TEMESA! Hivyo vikampuni vingine vya ukandarasi na ushauri elekezi tupa kule kwanza vinatozatoza tu wakati hela yako haiendi bure bure!!

Naona tayari kule Ukonga mambo bwerere na fedha zote zipo TBA tayari kwa kujenga maflat ya askari kama ulivyosema utatoa "instruction" kwa chief secretary! Hakuna cha bajeti, kutangaza tenda wala nini!

Hapa kazi tu!
Hujaenda tenda ya uwanja wa ndege? Ungependa makampuni ya serikali yasipate kazi? Kumbuka toka enzi za nyerere makampuni ya serikali yalipewa kandarasi kubwa kubwa kwa mfano mecco imejenga barabara nyingi nchini imejenga ghorofa la kitega uchumi dar imejenga soko la kariakoo nk kumbuka kwamba sio rahisi kampuni ya serikali kupata tender ya kujenga mradi wa mtu binafsi lkn ni rais kampuni bunafsi kupata tender serikalini na sekta binafsi hivyo aliyekuwa anachezewa rafu kwa muda mrefu ni makampuni ya ujenzi ya serikali kwa sasa anayayewezesha lkn na watu binafsi nao wana nafasi yao kwa sab serikali haina makampuni ya kutosha na kila eneo la uhandisi lazima sekta binafsi itahusishwa tu.
 
We akili zako hazina akili,tambua hizo kampuni za ujenzi zinalipa kodi na nilazima zipate Nazi ili ziweze kujiendesha na kutoa ajira kwa vilaza wanaomaliza chuo,fikiri mara mbili kabla huja post utumbo wako.
 
Hujaenda tenda ya uwanja wa ndege? Ungependa makampuni ya serikali yasipate kazi? Kumbuka toka enzi za nyerere makampuni ya serikali yalipewa kandarasi kubwa kubwa kwa mfano mecco imejenga barabara nyingi nchini imejenga ghorofa la kitega uchumi dar imejenga soko la kariakoo nk kumbuka kwamba sio rahisi kampuni ya serikali kupata tender ya kujenga mradi wa mtu binafsi lkn ni rais kampuni bunafsi kupata tender serikalini na sekta binafsi hivyo aliyekuwa anachezewa rafu kwa muda mrefu ni makampuni ya ujenzi ya serikali kwa sasa anayayewezesha lkn na watu binafsi nao wana nafasi yao kwa sab serikali haina makampuni ya kutosha na kila eneo la uhandisi lazima sekta binafsi itahusishwa tu.
"Nikapiga simu TBA nikawauliza, kwani nyie mtatoza shiringi ngapi? Wakajibu birioni 13 nikawaambia washushe mpaka birioni 10 wakakubari nikawapa mradi wa mafrat ya UDSM"
 
Kampuni nyingi zitakufa kifo cha mende na serikali itakosa mapato wakati huo huo mzunguko wa fedha utakuwa kidogo.

Umuhimu wa serikali ya majimbo ndo huu.
Zitakufaje kwani zilianzishwa kwa ajili ya kujenga majengo ya serikali tu? Na wakati zinaanzishwa makampuni ya serikali hayakuwepo? Ile interchange ya mbagala inajengwa na serikali? Uwanja wa ndege wa chato unajengwa na serikali?
 
Kwani hayo makampuni ya serikali si yameajiri watanzania pia, kama ni dereva au engineer wote ni watz kama bei ni ndogo na ubora ni sawa acha wapewe tu. Tenda nyingi za serikali bei ilikuwa inflated sana kwa sababu ya 10% za watu.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom