Waongoza ndege Ujerumani kugoma kesho!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Wasafiri wa ndege nchini Ujerumani huenda kesho wakakumbwa na ucheleweshaji na kufutwa kwa safari kutokana na mgomo* wa waongoza uliyopangwa kufanyika kesho.

Kiasi ya safari 2,500 huenda zikaathirika kutokana na mgomo huo ambapo chama cha waongoza ndege kinadai nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi hao.

Chama hicho kinadai nyongeza ya asilimia sita na nusu.Wiki iliyopita mgomo uliyopangwa kufanyika ulifutwa dakika za mwisho baada ya mahakama ya Frankfurt kusitisha zoezi hilo.

Uamuzi ulikuwa ukitarajia leo hii jioni iwapo mgomo huo wa kesho uendelee au la.Mgomo huo unatarajiwa kuanza saa 12 asubuhi hadi mchana kwa saa za Ulaya ya Kati.

*
 
Back
Top Bottom