Waombolezaji 380 wanusurika kufa baada ya kunywa maji ya kisima yenye sumu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,008
9,873
Waombolezaji waliokuwa kwenye msiba wanaokadiriwa kufikia 380 wamenusurika kifo baada ya kugundua kutumia maji ya kisima yenye sumu kwa kupikia na kunywa mara baada ya mifugo wakiwemo ng'ombe 16 kufa papo hapo baada ya kunywa maji hayo.

Mifugo mingine iliyokufa baada ya kunywa maji hayo ni punda, bata na paka. Tukio hilo limeripotiwa kutokea juzi katika kijiji cha Mkusa kilichopo katika Kata ya Kilangawana katika Bonde la Ziwa Rukwa katika wilaya ya Sumbawanga na kusababisha taharuki na huzuni kwa waombolezaji waliokusanyika katika nyumba ya mfugaji Elias Juma

Taarifa kutoka eneo hilo la tukio zinaeleza kuwa katika nyumba ya Juma iliyokuwa na msiba kuna kisima cha maji ambacho alikichimba kwa matumizi ya nyumbani kwa kupikia, kunywa na kunywesha mifugo yake

Taarifa zilisema kuwa kabla ya waombolezaji hao hawajaanza kuyatumia maji hayo kwa kunywa na kupikia, wanyama hao walichotewa na walipoyanywa walikufa papo hapo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo amethibitisha kuwa tukio hilo lilitokea juzi wakati wakazi wa Kijiji cha Mkusi walipokusanyika msibani kwa mfugaji Juma.

Alisema kuwa watu wawili wamekamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kumwaga sumu katika kisima kilicho jirani na nyumba ya Juma.

Aliongeza kusema kuwa wawili hao ni majirani wa Juma ambapo walishashtakiana mahakamani katika shauri la mgogoro wa ardhi.

"Maofisa Polisi na mtaalamu wa afya walifika kijijini hapo na kufanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kuwa mifugo hiyo ilikunywa maji yenye sumu ambayo haikuweza kufahamika mara moja,"alieleza. Alithibitisha kuwa hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kupoteza maisha kutokana na tukio hilo.

Akielezea tukio hilo, Juma alisema mifugo yake hiyo wakiwemo ng'ombe wa kisasa 16, punda, bata na paka walikufa papo hapo baada kuyanywa maji hayo.

"Nimepata hasara kubwa kwani ng'ombe wangu 16 wamekufa baada ya kunywa maji hayo, kati yao ni madume matatu ya kisasa aina ya Boran ambao kwa pamoja wana thamani ya Sh 24,900,000 kwani kila mmoja wao ana thamani ya Sh 8,300,000.

Chanzo: HabariLeo
 
Mifugo mingine iliyokufa baada ya kunywa maji hayo ni punda, bata na paka. Tukio hilo limeripotiwa kutokea juzi katika kijiji cha Mkusa kilichopo katika Kata ya Kilangawana katika Bonde la Ziwa Rukwa katika wilaya ya Sumbawanga na kusababisha taharuki na huzuni kwa waombolezaji waliokusanyika katika nyumba ya mfugaji Elias Juma.

Taarifa kutoka eneo hilo la tukio zinaeleza kuwa katika nyumba ya Juma iliyokuwa na msiba kuna kisima cha maji ambacho alikichimba kwa matumizi ya nyumbani kwa kupikia, kunywa na kunywesha mifugo yake.

Taarifa zilisema kuwa kabla ya waombolezaji hao hawajaanza kuyatumia maji hayo kwa kunywa na kupikia, wanyama hao walichotewa na walipoyanywa walikufa papo hapo

Kuna maswali ya kujiuliza
  1. Aliyewachotea maji mifugo aliwaza nini kabla ya kuyapeleka maji hayo kwa matumizi ya ndani
  2. Je kwanini maji hayo hayakusababisha vifo kabla ya siku hiyo kama mwenye kisima alikuwa anayatumia tangu alipokichimba?
 
Swali la kwanza tunajibu, God works in mysterious ways
Swali la pili ni kuwa hiyo simu inaweza kuwa iliwekwa usiku wa tukio mradi awaue wote watakaokuwa msibani haswa ndugu wa mgomvi wake ambaye ni lazima wangekuwepo kwa wingi siku ya msiba
 
Kuna maswali ya kujiuliza
  1. Aliyewachotea maji mifugo aliwaza nini kabla ya kuyapeleka maji hayo kwa matumizi ya ndani
  2. Je kwanini maji hayo hayakusababisha vifo kabla ya siku hiyo kama mwenye kisima alikuwa anayatumia tangu alipokichimba?
1. Kazi ya kusafisha mabanda na kuwawekea mifugo maji hufanyika mapema subuhi. 2. Ni vigumu mtu kuweka sumu mchana sababu anaweza kuonekana. Bila shaka sumu iliwekwa usiku wa kuamkia siku ya tukio. Ndio maana hakukuwa na madhara siku moja kabla ya siku ya tukio.
 
Mkuu liulize hilo jamaa una swali jingine?
 
Mwenyezi Mungu siku zote akiamua jambo lisitokee haliwezi tokea kamwe hata liwe limebakiza sekunde 1 kuleta madhara lazima liumbuke au mpango uvurugike tu! Ndio tunabaki kushangaa kwamba kama ingetokea ingekuaje!

Hapo tungesikia watu sio chini ya 100+ wamepoteza maisha sabu misiba ya vijijini huwa na watu wengi sana wa kila aina na kutoka kila kijiji au mtaa wa jirani na wengi hulala msibani au kuwahi asubuhi na mapema kwa ajili ya kusaidia wafiwa hasa kina mama na hawa ndio tungelisikia wamepoteza maisha sana...
 
Waombolezaji waliokuwa kwenye msiba wanaokadiriwa kufikia 380 wamenusurika kifo baada ya kugundua kutumia maji ya kisima yenye sumu kwa kupikia na kunywa mara baada ya mifugo wakiwemo ng'ombe 16 kufa papo hapo baada ya kunywa maji hayo.

Mifugo mingine iliyokufa baada ya kunywa maji hayo ni punda, bata na paka. Tukio hilo limeripotiwa kutokea juzi katika kijiji cha Mkusa kilichopo katika Kata ya Kilangawana katika Bonde la Ziwa Rukwa katika wilaya ya Sumbawanga na kusababisha taharuki na huzuni kwa waombolezaji waliokusanyika katika nyumba ya mfugaji Elias Juma

Taarifa kutoka eneo hilo la tukio zinaeleza kuwa katika nyumba ya Juma iliyokuwa na msiba kuna kisima cha maji ambacho alikichimba kwa matumizi ya nyumbani kwa kupikia, kunywa na kunywesha mifugo yake

Taarifa zilisema kuwa kabla ya waombolezaji hao hawajaanza kuyatumia maji hayo kwa kunywa na kupikia, wanyama hao walichotewa na walipoyanywa walikufa papo hapo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo amethibitisha kuwa tukio hilo lilitokea juzi wakati wakazi wa Kijiji cha Mkusi walipokusanyika msibani kwa mfugaji Juma.

Alisema kuwa watu wawili wamekamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kumwaga sumu katika kisima kilicho jirani na nyumba ya Juma.

Aliongeza kusema kuwa wawili hao ni majirani wa Juma ambapo walishashtakiana mahakamani katika shauri la mgogoro wa ardhi.

"Maofisa Polisi na mtaalamu wa afya walifika kijijini hapo na kufanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kuwa mifugo hiyo ilikunywa maji yenye sumu ambayo haikuweza kufahamika mara moja,"alieleza. Alithibitisha kuwa hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kupoteza maisha kutokana na tukio hilo.

Akielezea tukio hilo, Juma alisema mifugo yake hiyo wakiwemo ng'ombe wa kisasa 16, punda, bata na paka walikufa papo hapo baada kuyanywa maji hayo.

"Nimepata hasara kubwa kwani ng'ombe wangu 16 wamekufa baada ya kunywa maji hayo, kati yao ni madume matatu ya kisasa aina ya Boran ambao kwa pamoja wana thamani ya Sh 24,900,000 kwani kila mmoja wao ana thamani ya Sh 8,300,000.

Chanzo: HabariLeo
Kwenye watu 10 binadamu mmoja ,Dunia ya sasa imani imekwisha!!
 
Back
Top Bottom