Waomba siku nzima, kufufua maiti

Ab-Titchaz

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
14,631
4,225
Rare prayers to bring back dead pastors

PIX.jpg

Pastors and faithful of Kingdom Seekers Fellowship International pray for the resurrection of pastors Patrick Wanjohi and Francis Ndetei, who died in a road accident last week

By SIMON SIELE
Posted Monday, February 22 2010 at 20:00​

They came from the four corners of the country and even neighbouring Uganda with one mission - to pray for a miracle.

Two pastors in the Kingdom Seekers Fellowship International church were killed in a road accident on Monday last week and the faithful believed that God would resurrect them if they prayed hard enough.

Their death in a car that rolled on the Nairobi-Nakuru highway, the faithful believed, was the work of the devil and the miracle was to shame the evil one.

"Our pastors have been perishing in road accidents and it is time for us to shame the devil, who is behind the tragedies," Pastor John Kamau William, the church's general overseer, announced to the congregation outside their church in Nakuru.

There was a large congregation of faithful and curious onlookers who were eager to witness the resurrection.

Word had gone round the town that a miracle was to happen during the requiem mass for pastors Patrick Wanjohi Wanja and Francis Kamau Ndetei.

So, when the caskets carrying the remains of the two were taken to the church, crowds of people milled around to see what would happen.

The neutral people in the crowd were amazed by the aggressive and drawn out prayers that the believers engaged in.

Even a heavy downpour that pounded Nakuru as the prayers went on did not dampen their spirits. In fact, the sudden rains were seen as a sign that the miracle was about to happen. The prayers continued with even more vigour.

Scores of pastors surrounded the caskets and cried out to God for more than an hour.

At one point, Pastor Ndetei's widow, went to the tent where the coffin was placed and shook it as she hysterically pleaded with God to raise her husband.

Another worshipper pushed the coffins in an attempt to stir the dead pastors to wake up from their "deep sleep." Nothing happened.

By this time, one could sense doubts creeping into the minds of some of the faithful. To banish any such thoughts, Apostle Steven Bulungi from Uganda chased away the doubting Thomases.

He kept on telling the congregation that they were not being "fanatical or emotional" enough. '‘You are practising the word of God," he exhorted them.

Nevertheless, the worshippers eventually lost hope. One of the pastors announced: "Some miracles do not happen instantly, as was the case when Jesus cursed the fig tree."

http://www.nation.co.ke/News/-/1056/866782/-/vqm23b/-/index.html
 
Ukitzama video n'do basi tena, maana ni vituko mtindo mmoja...:D

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=LfD41MTuqw0&feature=player_embedded[/ame]​
 
Speaking as a christian, what they are doing is absurd. Of-course in Jesus name dead can be raised, but with a purpose and a special reasons, and all miraclea are meant to show people who dont believe!

I dont see any spiritual katika hili, ilikuwa ni uchungu na mshtuko walioupata

Poleni kanisa, kila kitu kina sababu
 
Rare prayers to bring back dead pastors

PIX.jpg

Pastors and faithful of Kingdom Seekers Fellowship International pray for the resurrection of pastors Patrick Wanjohi and Francis Ndetei, who died in a road accident last week

By SIMON SIELE
Posted Monday, February 22 2010 at 20:00​

They came from the four corners of the country and even neighbouring Uganda with one mission — to pray for a miracle.

Two pastors in the Kingdom Seekers Fellowship International church were killed in a road accident on Monday last week and the faithful believed that God would resurrect them if they prayed hard enough.

Their death in a car that rolled on the Nairobi-Nakuru highway, the faithful believed, was the work of the devil and the miracle was to shame the evil one.

“Our pastors have been perishing in road accidents and it is time for us to shame the devil, who is behind the tragedies,” Pastor John Kamau William, the church’s general overseer, announced to the congregation outside their church in Nakuru.

There was a large congregation of faithful and curious onlookers who were eager to witness the resurrection.

Word had gone round the town that a miracle was to happen during the requiem mass for pastors Patrick Wanjohi Wanja and Francis Kamau Ndetei.

So, when the caskets carrying the remains of the two were taken to the church, crowds of people milled around to see what would happen.

The neutral people in the crowd were amazed by the aggressive and drawn out prayers that the believers engaged in.

Even a heavy downpour that pounded Nakuru as the prayers went on did not dampen their spirits. In fact, the sudden rains were seen as a sign that the miracle was about to happen. The prayers continued with even more vigour.

Scores of pastors surrounded the caskets and cried out to God for more than an hour.

At one point, Pastor Ndetei’s widow, went to the tent where the coffin was placed and shook it as she hysterically pleaded with God to raise her husband.

Another worshipper pushed the coffins in an attempt to stir the dead pastors to wake up from their “deep sleep.” Nothing happened.

By this time, one could sense doubts creeping into the minds of some of the faithful. To banish any such thoughts, Apostle Steven Bulungi from Uganda chased away the doubting Thomases.

He kept on telling the congregation that they were not being “fanatical or emotional” enough. ‘‘You are practising the word of God,” he exhorted them.

Nevertheless, the worshippers eventually lost hope. One of the pastors announced: “Some miracles do not happen instantly, as was the case when Jesus cursed the fig tree.”

http://www.nation.co.ke/News/-/1056/866782/-/vqm23b/-/index.html

hii Sasa Sio ibada bali Kukufuru Mungu . Kwani Mwenyeezi mungu kuwauwa hao imekuwa vibaya? si kila mtu anakwenda kwa wakati wake? Ehhh Ndugu zetu Walokole kazi ipo kwenu mnataka kugeuka Bwana Yesu Aliowafufuwa Wafu Kazi kweli dunia ndio inakwenda ukingoni jamani tuache imani Potofu jamani
 
The irrational nature of faith is funny. No one comes back from death... No one. Especially a fatal trauma case like this, these people are just so caught up in myths that they fail to see reality. How can someone come back from a fatal car accident.lol
 
SALA KUU INATUAMBIA TUSALI HIVI:-
Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe makosa yetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.] Amin.

SASA NAONA HAO JAMAA HAWATAKI MAPENZI YA MUNGU YATIMIZWE.SASA SIJUI WANAMUABUDU NANI?
 
Imani zingine hizi zina utata mwingi!
Wafufuke kwaajili ya mission gani kubwa sana waliyokuwa wanaifanya? Mbona tumewasikia hiyohiyo jana wakati habari hizi zikitoka!..kwanini pia waliita watu wa Press ili wawe wanashoot ile maneno, kama si kujishaua?
Walitakiwa wajifungie mahala pa utulivu, at least ingesaund!
 
.......Hapo wataomba, watalia na kunena juu ili wafu wafufuke, imani hizi jamani acheni tu.
 
Duh jana niliokuwa natazama TBC1 taarifa ya habari sikuamini nilichokuwa nakitazama kuna baadhi ya wahubiri wanawapotosha waumini wao kiasi kwamba wanakuwa wanawaabudu wao badala ya mwenyezi mungu.

Watumishi wa mungu kama Askofu Kakobe wanaingia moja kwa moja katika hili kundi la kuabudiwa wao badala ya Mungu.Fikiria waumini wanashinda siku nzima kanisa kulinda TANESCO wasipitishe waya kwenye kanisa lao,sijui wanatafuta riziki zao saa ngapi ?.Twende mbali kidogo hivi Askofu Kakobe akitangulia mbele ya haki waumini wake wataacha kufanya vituko kama hao jamaa wa huko Kenya ?.Niliwahi kusema haya makanisa ya aina Mzee wa upako,Askofu Kakobe,Mtume na Nabii Jodev na nk yafaa yatazamwe kwa makini sana kwasababu mara nyingi badala ya kumhubiri Kristo mfufuka yamejikita zaidi kuwatukuza viongozi wao.
 
Naye (YESU KRISTO) akamjibu shetani ...USIMJARIBU BWANA MUNGU WAKO.
Hawa ndicho wanachokifanya. Ni sawa na wale waliopo morogoro road....
 
Ndio hali ya siku hizi katika makanisa ya kajanja. Unakuta Kanisa linaitwa kwa mfano Chalinze Miracle Centre, lingine miracle this and that. Kama mtu mmoja alivyosema hapa JF makanisa haya yote yana majina ya Kiingereza! This is region taken too far and bordering on nuisance. Kibwetere kule Uganda aliwadanganya waumini wake kwamba mwisho wa dunia unakaribia. Ilivyoshindikana akawachoma na mafuta! Na kule Guyana miaka ya 1970 waumini walinyeshwa sumu wakapoteza maisha! Na hapa DAR wapo. Mwenye macho hambiwi tazama.
 
Hawa watu wamezidi.... na wanaendelea kupata nguvu maana kuna wakristo wanawasikiliza na kuwaamini.
 
Hata hivyo wanakubali kuwa huo muuijiza unaweza usitokee na hivyo by Thursday kama hawatafufuka watawazika. Pengine wataanza kuwaombea wafufuke toka makaburini. Imani ni hakika ya mambo utarajiayo na bayana ya yale yasiyoonekana. Kazi kubwa. Inabidi waliotoa wazo hili wajipange ili wasipoteze waumini pale muujiza utakapogoma.
 
Imani nyingine zinaweza kuathiri maana halisi ya dini. Nina hakika kinachosubiriwa na hao waumini ni miujiza ya Bwana ambayo kwa asilimia kubwa haitatokea. Sasa je jamii itawachukuliaje hao mapastor baada ya kushindwa kutimiziwa lengo lao. TUWE NA KIASI KATIKA IMANI. Nyanda
 
Kufufuka inawezekana kabisa. Yesu ndiye ufufuo na uzima.

Wakati anajiandaa kumfufua Lazaro, Mariam na Martha walifikiri anazungumzia ufufuo siku ya kiama.

Kilichoshindikana kwa hawa jamaa ni mambo yafuatayo:

1. Yesu hakumuweka Lazaro kwenye jeneza, wala si yeye aliyemzika, sasa hawa jamaa miili wameiweka wenyewe kwenye jeneza tayari kuzikwa halafu wanaomba ufufuo, hapo hakuna Imani.

2. Yesu alikuwa anakesha milimani akiomba, mpaka kesho yake anapoingia hekaluni uweza wa Mungu unakuwepo kuponya, leo hii wachungaji wanakesha wakisengenyana, wamegeuza makanisa miradi, hapo hakuna uweza wa Mungu bali uweza wa mwekundu wa msimbazi ambao hauwezi kufufua.

3. Yesu alifufua kwa utukufu wa Mungu, hao jamaa wanataka mtu afufuke kwa uchungu binafsi walio nao, na wengine ili wajaze makanisa mapato yaongezeke, hapo Mungu hashawishiki kufufua.

4. Makanisa ya sasa yamemfukuza Roho mtakatifu na kumkaribisha roho ya fedha itawale, sasa bila Roho mtakatifu ufufuo utatokea wapi? Leo hii ukiingia makanisa yao unaendesha Hummer unapewa uzee wa Kanisa siku hiyo hiyo. Kuna ufufuo hapo?

5. Wakristo wa leo wanaogopa uchawi, shetani na kifo kuliko Mungu. Mungu anasema akiogopacho muovu ndicho kimpatacho. Leo hii ukitaka watu waache kusikiliza neno la Mungu na wakusikilize wewe masaa yote wewe danganya kuwa ulikuwa mchawi na sasa umeokoka. Wataacha mambo yote ya maana kanisani ili wasikilize ulivyokuwa mchawi mahiri Afrika nzima ukichezea mapadre, wachungaji na mashehe.

Naomba niishie hapo. Ufufuo unawezekana kabisa isipokuwa mwana wa adamu atakaporudi JE ATAIKUTA IMANI DUNIANI?
 
Hapa ndo kweli sisi tunaonekana ni wanadamu, kimsingi Mungu hana ubaya na mwanadamu kwasababau yoyote na Mungu hakumkatilia Mwanadamu kufanya/ kuaamini chochote ispokuwa dhambi. Kwa Mambo ya imani Mungu amempa mwanadamu Heshima ya juu kabisa ya kuamini lolote na na kutenda kwa imani kubwa na litatendeka bila kujali Mungu alisha amua nini juu ya jambo hilo.
Kwa mfano Ezekieli aliambiwa na MUNGU utakufa lakini yeye akaamini kuishi na akamuomba MUNGU kuishi na akaishi, Mama mjane alifiwa na mtoto wake mbele ya mtumishi wa MUNGU Elisha au Elia(Sina kumbukumbu vizuli kati ya hao wawili) Naye akaomba na akaishi.

Swala ndugu zangu hapa sio kwamba mtu akifa kwa kifo chochote hawezi kurudi, swala ni kumshawishi MUNGU aruidi aje kufanya nini? Kinacho mtachi MUNGU ni sababu yakumrudisha mtu huyo lakini kurudi sio isue.

Nanapenda kusisitiza hapa na sijui kwanini tunalogwa eneo hili. Ili imani ionekane kuwa ni imani thabiti lazima ifanye kazi ambayo wengine watashangaa, na kama imani zetu zitabakia kufukuza mapepo tu; nafikiri tunahitaji kutafakari makuuzi ya imani zetu, tunazo ahadi za kufanya kazi zaidi ya alizo fanya bwana YESU je ni kazi ipi ambayo sisi wanadamu tumefanya hadi YESU ashangae?

Hapa ni upungufu tunahitaji kutafakari zaidi.
 
Imani nyingine zinaweza kuathiri maana halisi ya dini. Nina hakika kinachosubiriwa na hao waumini ni miujiza ya Bwana ambayo kwa asilimia kubwa haitatokea. Sasa je jamii itawachukuliaje hao mapastor baada ya kushindwa kutimiziwa lengo lao. TUWE NA KIASI KATIKA IMANI. Nyanda

Sasa wakifufuka kweli hiyo Alhamis mtawaamin au mtazidi kuwakataa
 
Mungu anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Sote pamoja na hao wafiwa na hao mapastor tunataka kwenda mbinguni. Mbinguni huendi bila ya kufa iwe kwa ajali, maradhi, kuzama baharini, umri na kadhalika. Kifo siyo laana wala balaa. Unapokufa roho yako inakuwa imelivua joho au koti ambalo ni mwili wako. Ndipo waenda mbinguni. Sasa hao waliokuwa wanafanya maombi hayo walikuwa hawako kirohoni hata kidogo bali walitegemea akili zao ambayo ni mwilini. Nina hakika hao marehemu walikuwa wanachukizwa na matendo yao. Wenzao wako kwenye raha ya pepo wao wanahangaika wanataka warudi hapo duniani ambako Yesu alituambia kuwa kumejaa dhiki. Ama kweli njia iendayo mbinguni ni nyembamba mno na ile iendayo jehanamu ni pana na wengi wataenda huko.
 
Back
Top Bottom