waomba mikopo heslb 2013/2014 wote watapata kwa asilimia mia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

waomba mikopo heslb 2013/2014 wote watapata kwa asilimia mia.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by British economist, Aug 17, 2013.

 1. B

  British economist Senior Member

  #1
  Aug 17, 2013
  Joined: Jul 14, 2013
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [h=2][​IMG] Waomba mikopo heslb 2013/14 wote watapata mikopo kwa 100%[/h]
  Leo HESLB wametoa taarifa kwa Umma juu ya idadi ya waombaji wa mikopo kama ilivyoandikwa hapa chini:

  UTANGULIZI:
  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kwamba mchakato wa maombi mikopo kwa mwaka wa masomo 2013/2014 ulizinduliwa rasmi tarehe 1 Mei, 2013. Mchakato huo unaendelea vizuri na kwamba wanafunzi wengi wameweza kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS).

  WAOMBAJI WA MIKOPO WA MARA YA KWANZA:
  Utaratibu wa kujaza fomu za maombi kwa waombaji wa mara ya kwanza, unawaelekeza waombaji hao kutoa taarifa zao za kihistoria kama vile shule za sekondari walizosoma (Kidato cha IV na Kidato cha VI), hali ya mwombaji au wazazi wake kiafya na pia taarifa za mdhamini wa mwombaji mkopo. Taarifa hizo zinaiwezesha Bodi kuchambua na kujua iwapo mwombaji husika ana sifa ya kukopesheka au la. Ikumbukwe kwamba lengo la utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za elimu ya juu kusaidiwa kufikia malengo yao. Kwa njia ya uchambuzi huo Bodi inaweza kubaini kiasi cha mkopo unaohitajika au kiasi ambacho mwanafunzi anapaswa kuchangia katika gharama zake za elimu ya juu.Kwa vile taarifa za ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita hazihitajiki katika hatua hii ya Mwanzo, mwombaji wa mkopo haulizwi mahali popote katika fomu yake ya maombi kuhusu kiwango cha ufaulu. Hapo baadaye Bodi itakapohitaji kuthibitisha kiwango cha ufaulu wa mwombaji itapata taarifa hizo za ufaulu moja kwa moja kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Kutokana na utaratibu huu, mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita mwaka 2013 anaweza kuomba mkopo hata kabla ya matokeo ya Kidato cha Sita kitaifa kutolewa. Hii ni muhimu ili kuipa Bodi muda wa kutosha kupokea maombi ya mikopo, kuchambua na kisha kupanga mikopo kwa wanafunzi stahiki watakaokuwa wamedahiliwa kwa mwaka mpya wa masomo 2013/2014

  WANAFUNZI WALIOKWISHA OMBA MIKOPO:
  Hadi kufikia tarehe 30 Mei, 2013, waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha maombi yao ni 424, Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji ni 5,320 na wanafunzi wanaoedelea na masomo waliokwishathibitisha kuendelea kupatiwa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo ni 60,367, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.

  HITIMISHO:
  Bodi inatoa msisitizo kwa waombaji wa mikopo kama ifuatavyo:(i) Kuzingatia taratibu zote muhimu zilizowekwa kwa ajili ya maombi ya mikopo.(ii) Kutumia huduma ya msaada kwa wateja (Help Desk) kikamilifu kila wanapopata tatizo lolote katika mchakato wa ujazaji wa fomu za maombi. Huduma hiyo inapatika kwa kupiga namba 022 550 7910; kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku siku za jumatatu hadi ijumaa na kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 alasiri siku ya jumamosi.(iii) Kuzingatia muda uliopangwa wa maombi ya mikopo ambapo siku ya mwisho ni tarehe 30 Juni, 2013.
  IMETOLEWA NA:

  BODI YA WAKURUGENZI

  BODI YA MIKOPO YA ANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

  NB:
  Budget ya Wizara ya Elimu kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ni kutoa mikopo kwa jumla ya waombaji 98,025; yaani waombaji wapya watakao pata mikopo ni watu 35,649 na waombaji wanaoendelea na masomo ni 62,376.


   
 2. Mbrazili

  Mbrazili JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2013
  Joined: May 7, 2013
  Messages: 652
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Na iwe kweli basi
   
 3. s

  spleen JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2013
  Joined: Apr 24, 2013
  Messages: 1,178
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Positive changes are never happen in Tanzania
   
 4. Pompoo

  Pompoo JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2013
  Joined: Jul 19, 2013
  Messages: 362
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  outdated
   
 5. Landcruiser

  Landcruiser JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2013
  Joined: May 27, 2013
  Messages: 1,746
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Fake news
   
 6. s

  sir imma Member

  #6
  Aug 18, 2013
  Joined: Aug 17, 2013
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Loading....
   
 7. hekimatele

  hekimatele JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2013
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 9,500
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Ahsante kwa taarifa mkuu

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 8. K

  Khatwab mohamed New Member

  #8
  Aug 18, 2013
  Joined: Aug 17, 2013
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lkn inaweza kuwa kwel coz aijawah kutokea watu kulekebishwa kuomba mkopo
   
 9. xir jyerphy

  xir jyerphy JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2013
  Joined: Jul 12, 2013
  Messages: 996
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwani ni wapi watu walirekebishwa kuomba mkopo
   
 10. CYBERTEQ

  CYBERTEQ JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 7,466
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 0
  una uhakika na unachokisema?:disapointed:
   
 11. m

  moes JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2013
  Joined: Oct 30, 2012
  Messages: 1,859
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  nazani mleta mada hana hakika na anachokisema,

  pia inabidi afanye edit kwenye heading yake,maana ya kupata mkopo asilimia mia,kwamba kila mwombaji atakopeshwa fedha yote atakayoomba,kitu ambacho hakiwezekani.
  bora ungesema waombaji wa mkopo wote watakopeshwa kwa viwango tofauti(asilimia tofauti tofauti eg 100%,80%,60% etc.
   
 12. M

  Molembe JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2013
  Joined: Dec 25, 2012
  Messages: 7,581
  Likes Received: 3,833
  Trophy Points: 280
  Mpaka sasa waombaji wapya wapo 54000 wakati bodi wametenga bajeti ya kulipia watu 35000 tu sasa mleta mada anaposema watalipiwa wote simuelewi kabisa.
   
 13. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2013
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,784
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Heading na content vinatukanana!
   
 14. m

  mpuaj New Member

  #14
  Aug 18, 2013
  Joined: Aug 14, 2013
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cc tunachosubiria ni mkopo tu,,,,,haijalishi ni asilimia ngap watatupa.....
   
 15. HAMIS MOHAMED

  HAMIS MOHAMED JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2013
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  calling......
   
 16. C

  Cizokalugwagu Member

  #16
  Aug 18, 2013
  Joined: Jul 25, 2013
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heading na content ziko tofauti!
   
 17. Idd Omary

  Idd Omary JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2013
  Joined: Aug 11, 2013
  Messages: 242
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kaka umeckia kwenye redio ya mabox au? Coz baraza lishasema wanafunzi 1771 na zaidi wanaoendelea na masomo hawatapa mkopo mwaka 2013/2014 coz haeajakizi vigez pa1 na late submission!!!!!! Take easy!!!!
   
 18. M

  Malengo Jr JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2013
  Joined: Aug 19, 2013
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Kikubwa boom yaani 7,500/- kwa siku hayo mambo mengne ya ada cjui tuition fee ni minor issues.
   
 19. b

  besi boy Member

  #19
  Aug 23, 2013
  Joined: Aug 22, 2013
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha utani kaka haya mambo utatufanya tuchanganyikiwe
   
 20. b

  besi boy Member

  #20
  Aug 23, 2013
  Joined: Aug 22, 2013
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakubwa 2juzane kuhusu kupanda kwa boom kutoka 7500 mpaka 10,000 je,issue hii ni ya kweli?
   
Loading...