Waomba Kikwete ampe Kimaro ubunge;Hatumaanishi kuwa mbunge wetu Mrema hataweza kutuletea maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waomba Kikwete ampe Kimaro ubunge;Hatumaanishi kuwa mbunge wetu Mrema hataweza kutuletea maendeleo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Apr 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na Grace Michael

  BAADHI ya wananchi wa Jimbo la Vunjo, wamemwomba Rais Jakaya Kikweye kuangalia uwezekano wa kumteua aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Bw. Aloyce
  Kimaro kuwa mbunge.

  Rai hiyo ilitolewa juzi na wananchi hao ambao waliongozwa na Bw. Sadik Mneney kuwa pamoja na kuwa na imani kubwa na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Bw. Augustino Mrema, lakini bado wanaomba Bw. Kimaro ateuliwe ili kuongeza nguvu na kukamilisha kazi aliyoianzisha.

  "Tuna imani kubwa na mbunge wetu kuwa atatekeleza kwa vitendo ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni kwa ajili ya kutuletea maendeleo ya kiuchumi hasa katika kufufua zao la Kahawa ambalo ndio zao kuu la uchumi wetu, lakini hata Bw. Kimaro bado tunamhitaji na ndio maana tumeamua kumwomba rais kwa kutumia mamlaka aliyonayo kumteua," alisema Bw. Mneney.

  Alisema kuwa katika kipindi chake cha miaka mitano (2005-2010), Bw. Kimaro alijitahidi kubuni, kutafuta fedha na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Vunjo na miradi hiyo ni pamoja na na uanzishwaji wa Benki Vijijini (VICOBA), miradi ya maji, elimu, ujenzi wa Hospitali yenye hadhi ya wilaya na ujenzi wa barabara.

  "Sisi Wananchi wa Jimbo hili tunaona kuwa miradi hii ambayo ni ya manufaa makubwa kwa Wananchi wa Jimbo hili itasimamiwa vizuri kama aliyeibuni atapata nafasi ya kuipigania katika vyombo vya maamuzi likiwamo bunge letu," alisema na kuongeza kuwa.

  "Hatumaanishi kuwa mbunge wetu Mrema hataweza kutuletea maendeleo, la hasha! Bali uzoefu unaonesha kuwa pale ambapo mwanzilishi wa jambo fulani anakuwa ameondoka hasa viongozi wa kisiasa, uendelezaji wa mawazo yake na fikra zake utategemea zaidi utashi wa kisiasa wa mrithi wake," alisema.

  Alisema kuwa nia ya wananchi hao ya kutaka kurejeshwa kwa Bw. Kimaro ndani ya bunge ni kutaka kusaidiana na Mrema katika kupigania maendeleo ya wananchi wa Jimbo la Vunjo.

  Taarifa hiyo ilitolewa kwa ushirikiano wa Mchungaji Joram Monyo, Bw. Sadik Mneney, Bw. Shaban Ombasele, Bi. Prisca Tarimo, Bi.Monica Temba na Bw. Jullius Mkojera.
   
 2. n

  nndondo JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  wanawazimu hawa kama Kimaro alikua anawafaa wangempa kura arudi bungeni wasitupangie cha kufanya. Kama kweli huyo mrema wao anafaa basi na amalizie miradi aliyoanzisha kimaro, wamembwaga mbunge mwenye hela zake wamempa omba omba halafu wanataka eti kimaro arudi aje amalizie swala la kuanzisha benk imekula kwao, kimaroa baba yangu kazana na mambo yako achana na hayo mabwege watanzania ndivyo walivyo huku wataka na huku wataka, kura wampe mrema kula wale kwa kimaro
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hao ndio wapiga kura wa tanzania wasiojua waamue nini kwa ajili ya hatma yao ya baadaye!
   
Loading...