Wao wanamtukana Lissu kila wakiwa na mkutano ila Lissu hawatukani

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
457
1,973
Wakuu, huyu Polepole anamtukana lisu kisa yuko juu ya katiba; asubirie siku ifike aone ataeleza nani alikuwa anamtuma.

Katika ufuatiliaji Wangu Siku zote sijawahi kumsikia Lissu akimtukana mtu, Lissu mikutano yote aliyohutubia amekuwa akieleza mabaya yaliyofanywa na Magufuli, akieleza madhara waliyopata Watanzania na yeye atakayoyafanya kwa Watanzania.

Sasa hawa waliozoea kusifiwa, wakitesa wanasifiwa, wakinyanyasa wanasifiwa, wakitukana wanawake wanasifiwa, wakibagua wanasifiwa, akisema kamweleze mume wako anapigiwa makofi, akisema Mimi ni jiwe kweli kweli anapigiwa makofi, akisema kuwa nyie ni Malaya ndio maanaa huo mto uliitwa mto nini sijui (nimemsahau wakuu), anapigiwa makofi; akisema siwez Leta Maendeleo kwa kuwa mmechagua upinzani anapigiwa makofi, sikuleta tetemeko makofi kila alichokuwa akikifanya alikuwa akipigiwa makofi kiwe kibaya, makofi ndio maana wanashangaaa kuona mtu amejitokeza gafla anakosoa wanahangaika na kufokafoka na kutokwa na mapovu.

Hivi niwaulize swali: Hivi nyie hamjui maana ya siasa? Hivi nyie hamjui maana Ya kutaka madaraka? Yani Kwa akiri yako Pole Pole ulitegemea lisu asimame jukwaaani aseme anayoyasema lipumba, asimame jukwaani ayaseme anaeyasema mrema, asimame jukwaani ayaseme maneno anayoyasema mbatia? Yani lisu asimame jukwani amsifie magufuli?

Hivi Kwa akili ya kawaida lisu aliepigwa risasi 32 na 16 zikampata mwilini mwake kwa maagizo ya wakubwa wenye mamlaka na akapona Kwa miujiza, asimame jukwaani asiseme ukweli wa mateso wanayoyapata wananchi amsifie magufuli kiunafiki?

Ulisikia wapi? Hata ungekuwa ni wewe umepigwa marisasi Yote hayo umeamua kujitoa muhanga kutetea watu waliofungwa minyororo huwezi kuogopa maanaa Yule alishakufa akafufuka, ndio jukwaa pekee la kusemea tu, hawa wengne hawajakufa yule keisha kufa kafufuka ndio wa kuwaokoa hawa Watanzania usitegemee kusikia akimsifia Magufuli.

Halafu mnaposema kuwa mlitegemea aongee tu atakayoyafanya hiyo sio siasa, Polepole hakuna siasa kama hiyo duniania kote, haipo siasa hiyo.

Yani hata wewe ukiandika andiko kupeleka kwa mabeberu wenu hao wa bank ya duniani lazima uanze kueleza tatizo lililopo limeletwa na nini ndipo useme utaenda kulitatua Kwa njia zipi, usitegemee kuwa lisu atasema tu atakachoenda kufanya, lazima aanze na shida iliyopo ililetwa na nani ndio siasa. Sema Magufuli hakujua hiyo siasa maanaa miaka yake Yote hata ubunge alikuwa anapita bila kupingwa hajawahi kuombea na mtu na miaka hiii mitano hajawahi kukosolewa ndio anashangaaa sasa.
 
Mtu aliepigwa risasi 32 Hakufa unataka kujidanganya Kuwautamshinda kwenye Uchaguzi? Unapaswa kujiuliza Mara mbili mbili Uchaguzi ni tarehe 28 mwezi wa kumi ndio Kwanzaa baaado unahangaika kumtukana lisu kwenye mkutano wako, hivi hadi 28 October si utakiwa umejinyea?
 
Mtu aliepigwa risasi 32 Hakufa unataka kujidanganya Kuwautamshinda kwenye Uchaguzi? Unapaswa kujiuliza Mara mbili mbili Uchaguzi ni tarehe 28 mwezi wa kumi ndio Kwanzaa baaado unahangaika kumtukana lisu kwenye mkutano wako, hivi hadi 28 October si utakiwa umejinyea?
Comrade ndio siasa ilivyo usitokwe sana na mapovu.
 
Siasa ni mapambano yenye kutafuta njia ya kumvutia mpiga kura.

Timu ya Kampeni ya CCM toka chaguzi 1995, 2000, 2005 ,2010, 2015 zile timu zilikuwa makini na zenye mpangilio ulioshiba kisiasa chini ya manguli wakiongozwa na kampeni manager Kinana.

Hawa nakumbuka ilikuwa na kazi ya kumuandaa vyema mgombea wa CCM akiwa na jukumu moja tu , kuelezea Ilani ya chama cha Mapinduzi.

Tuhuma zote toka Kona yoyote ile zilikuwa zinajibiwa kwa weledi na timu ya kampeni na si mgombea.

Hii ilisaidia sana kumfanya mgombea kurelux muda wote wa kampeni. Lkn timu hii ya sasa ya CCM kwangu mm naiona imepwaya kiasi imemuachia mgombea mwenyewe na timu ya Wasanii kuipigania CCM.

Mgombea wa CCM, katika utendaji wake hana shaka hata kidogo.

Mwisho mishahara kwa watumishi majibu yake ni yale ya kuweka sementi kwa kuwa alishaahidi ataongeza wavute subira hivyo mameneja wangeweka neno watumishi watashangaa nyongeza yao.
 
Mkuu umeandika kwa uchungu....

By the way ngoja oct 29 Lisu akiapishwa mumpeleke bwna slow slow Ze HEGI
 
Back
Top Bottom