Wanzanzibar wanaotaka kuvunja Muungano wajifunze Comoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanzanzibar wanaotaka kuvunja Muungano wajifunze Comoro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Jun 3, 2012.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kumekuwa na hisia kwamba Zanzibar kwa kuungana na tanganyika aka Tanzania bara, kuna wanyima fursa za kufanya nchi yao kuwa na maendeleo, kama kuifanya Zanzibar iwe Duty Free Port kama ilivyo Dubai , au nafasi ya kujiongoza wao wenyewe vizuri zaidi bila ya kubanwa na Tanganyika(Tanzania Bara), lakini wakati huo huo wanatakiwa waangalie mazuri au mabaya ya kuwa nje ya muungano, kwa kuiangalia Comoro ambayo ina hali kama yao au twawenza kusema ni binamu zao.

  Je, kwanini Comoro wameshindwa kufanya visiwa vyao kuwa ni duty free port kama ilivyo dubai?

  Sana sana utawaona wa comoro hao hao wakienda dubai kununua mahitaji yao ya biashara au kuja tanzania bara, pili demokrasia yao pia imekuwa ya mashaka mashaka kutokana na kila kisiwa kuona kingine kina ibana, kiasi cha kusababisha umoja wa afrika kwenda kumuondoa kiongozi moja aliye taka kungangania madaraka bila kujali katiba na haki za visiwa vingine.

  Sasa Zanzibar hiyo inayo taka kujitenga inaweza vipi kulinda maslahi ya Pemba au Unguja, maana dalili hizo tuliziona wakati wa komandoo alivyo taka kuendelea kuwa madarakani hata pale muda wake ulivyoisha na katiba kuto mruhusu kugombea tena.

  Na kuhusu mafuta wataalamu wana sema yapo kati ya Tanga na pemba sasa Unguja watafaidika vipi ikiwa nao Wapemba watasema sisi ni weupe saana kuliko Waunguja hivyo tunataka kujitenga?

  Ndipo hapa tunapo ikumbuka kauli ya Mwl Nyerere kwamba nje ya muungano , kuna sisi wanzanibari na wao ni wanzanzibara na akitoka hapo sisi wapemba wao wa unguja,
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tuanajaribu kuongeza mijadala kila siku, lakini ukweli utabaki pale pale kwamba Wazanzibar wana haki ya kujiamulia mambo yao wenyewe na aina ya maisha wanayotaka kuishi bila kuingiliwa na mtu yeyote. Kwa hivyo kama wanataka kuwa nje ya muungano, sioni sababu ya kuwalazimisha kuwatawala bila ridhaa yao.
   
 3. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mhe. August,

  Niliposoma kichwa cha thread yako nilidhani unapendekeza Zanzibar ijiunge na visiwa vya Comoros. Wangekuwa "The Federation of West Indian Ocean Islands" with Anjuan as their capital. Wana lugha zinazoshabihiana.
   
 4. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unajadili assumption! hii ndo ubaya wa michogo! tujadili reality sivyo mnavyofikiri na michogo yetu! itatokea, ikitokea huo ni uzoba wa michogo!!!
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Reality tunajua na inaeleweka komanda alitaka kuendelea kuwa madarakani, pili inajulikana wazi kwamba wa unguja ndio wametoa maraisi zanzibar mara 4, huku wapemba wakilalama hali hiyo, inajulikana wazi kutokana na hali hiyo , baada ya kuf(cuf) kushinda viti vya ubunge vyote huko pemba walitaka wajitenge ili waachane na kubanwa na unguja.

  Sasa baada ya mimi kukupa facts, wewe mwenye kichwa mviringo kama manga koko nipe facts zako ambazo zinaonyesha mkisha jitenga Zanzibar itakuwa Dubai, na kwamba hamtakuwa na mitafaruku ya upemba na Uunguja.au Unzanzibari na Uzanzibara.
   
 6. Z

  ZIGZAG Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wabara nyinyi sio kazi yenu kuijadili zanzibar itakuaje baada ya kuvunja muungano, hata wakiuwana itakua ndio walivyotaka nyinyi mtaendelea na kuchimba dhahabu, tanzanite, mtajenga barabara za juu ni sawa tu.kinachotakiwa ni kuwapa zanzibar yao tu.
   
 7. Z

  ZIGZAG Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wabara nyinyi sio kazi yenu kuijadili zanzibar itakuaje baada ya kuvunja muungano, hata wakiuwana itakua ndio walivyotaka nyinyi mtaendelea na kuchimba dhahabu, tanzanite, mtajenga barabara za juu ni sawa tu.kinachotakiwa ni kuwapa zanzibar yao tu. kuna vichogo humu wanaijadili zanzibar kiutamadun wala hawajawahi kufika.
   
Loading...