Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja

Wanabodi,

Tangu baada ya Uingereza kupiga kura kujitoa kwenye EU, wanabodi wetu humu ambao ni Wanzanzibari, wanashadadia sana uamuzi huo, na kushinikiza wananchi wa Zanzibar nao, wapewe fursa ya kupiga kura ya maoni kwa kuulizwa kama bado wanataka kuendelea kusalia kuwa ndani ya muungano wetu, au wanataka kujitoa!. Wanaotaka kujitoa wakishinda, utaratibu wa jinsi ya kuuvunja muungano huu adhimu ziandaliwe, tuuvunje rasmi huu muungano wetu, na tuachane kwa amani, kuliko kuendelea huku baadhi ya wenzetu ni kila siku malalamiko, manung'uniko, na ghubu lisiloisha la kutwa kucha!.

Swali kwa wenzetu wa Zanzibari, sheria ya kura ya maoni si mnayo?!, sasa nini kinachowazuia kuitumia sheria hiyo kupiga hiyo kura ya maoni kuhusu muungano?!.

Kwa msio jua kuwa wenzetu Zanzibar, waliishaipitisha sheria hiyo ya kura ya maoni toka mwaka 2010, na ndio iliyotumika kuunda SUK!.

Kura ya Maoni Zanzibar ni Sheria Nambari 6 ya 2010 kuhusu uendeshaji wa kura ya maoni ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi mnamo mwezi wa Machi 2010 na kutiwa saini na Mheshimiwa Rais Karume mnamo mwezi wa Aprili 2010.

Tayari sheria hiyo iliishatumiwa na wananchi wa Zanzibar walipopiga kura ya maoni siku ya
Jumamosi tarehe 31 Julai 2010. Kura hiyo ilikuwa na lengo la kutafuta ridhaa ya wananchi wa visiwa hivyo vya Unguja na Pemba, kuamua iwapo wanalikubali wazo la kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2010.

Auamuzi wa kupigwa kwa kura hiyo ya maoni ulianzia katika kikao cha BLW ambacho kilipitisha Azimio la Baraza kufanywa kura ya maoni (referendum) iliyowashirikisha wananchi wa Zanzibar moja kwa moja katika kupata ridhaa ya wananchi kuanzisha mfumo na muundo wa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Kura hiyo iliendeshwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na kwa mujibu wa Kifungu cha 11(1) cha
Sheria ya Kura ya Maoni Nambari 6 ya 2010, ushindi wa Kura ya Maoni utaamuliwa kwa
wingi wa kura. Hivyo, kwa mujibu wa matokeo hayo, Wazanzibari waliopiga kura
ya NDIO kuunga mkono kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na SUK ikaendwa!.

Hayo yote yalifanyika Zanzibar bila kuishirikisha JMT, hadi ninavyozungumza hapa, japo SUK inatambuliwa rasmi na serikali ya JMT, lakini hadi leo, Katiba ya JMT ya 1977, bado haitambui SUK, hakuna kipengele chochote kinachoitambua SUK, wala katiba yetu haiwatambui wale makamo wawili wa rais wa Zanzibar, bali bado inamtambua Waziri Kiongozi ambaye doesn't exist anymore!.

Mabadiliko hayo ya Katiba ya Zanzibar ya 2010, yalikiuka katiba ya JMT na kuuvunja rasmi muungano kikatiba kwa katiba hiyo kuitangaza Zanzibar kuwa ni nchi, wakati katiba ya JMT inatamka nchi ni moja tuu JMT, na kuitambua Zanzibar kama sehemu ya JMT!.

Katiba hiyo ya Zanzibar ilivunja mamlaka yote ya Bunge la JMT, na mamlaka yote ya rais wa JMT, kwa kumtangaza rais wa Zanzibar ndio mkuu wa nchi ya Zanzibar na Amiri Jeshi Mkuu wa Vokosi vya SMZ!, na kuamua sheria yoyote itakayotungwa na Bunge la JMT, haitatumika Zanzibar mpaka BLW liridhie!, hii ni dharau kiasi gani kwa rais wa JMT na Bunge la JMT?!.

Kama yote haya yaliweza kufanyika bila kuishirikisha JMT, sasa ni nini kinachowashinda Wazanzibari kujiitishia kura yake ya maoni, kuamua kama isalie katika muungano au ijitoe?!.

Sasa tumechoshwa na hizi kelele, hivyo natoa wito kwa wenzetu Wazanzibari, waamue moja, ama waache kelele watulie, ama wafikie maamuzi waamue!.

Nawatakia Jumapili Njema.

Pasco
NB. Pasco wa JF ni muumini wa falsafa ya Nyerere kuhusu muungano, Nchi Moja, Serikali Moja chini ya Rais Mmoja wa JMT!, ila pia ni mtu mwenye maslahi fulani binafsi na Zanzibar!.

Rejea.
Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, Then "Twende kwenye Serikali Moja!.

Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?
Swali: Hivi Muungano Tanzania Upo Kweli?! au ni Dhana Tuu?! .
Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano?
Je, wajua kuwa kuna uwezekano Tanzania sio nchi halali Kisheria ...
Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto ...
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima .
Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena
Muundo wa Serikali Tatu ni Illegal, Unjustifiable, na Ni Kuvunja ...
Kumbe Sultan Jamshid Alifurahia Kuuawa kwa Karume!. Alitaraji ..
Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein ...
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua ...
Balozi Karume: 'CCM pekee iwe inasimamisha mgombea urais Zanzibar
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? |
Mbowe Alipua Bomu la Siri ya Ushindi Wa CCM Zanzibar
Imethibitishwa pasi na shaka kuwa CUF Ilishinda, Zanzibar ...
Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano ...
Inawezekana Vipi Zanzibar Hakuna Div I, Div II, wala Div III , Wao ..
Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na .
Hahahhahaha inaonyehs una uelewa mdogo sana wa Katina ya JMT ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.kazisome upya hizo katiba na utaona jinsi gani ulivyovurunda na kuizikanganya katiba kwa lengo la kupotosha watu.
Hivi Nauliza kwani wa ZNZ pekee yao ndiyo wasiopenda Muungano?
 
Pasco bana,yaani huyuhuyu aliyesimamia uchaguzi na kuamua alivyotaka ndo asimamie hiyo kura?hata wakikataa atasema wamekubali.
 
Tunaongea sana ila katika duania hakuna taifa linalojitambua linaruhusu kataifa kadogo kujiuendesha karibu na mipaka yake. Ndo yaliyopo Macao, Taiwan, Hong Kong, Gilblatar, hata visiwa vingi vidogo vinavyo zunguka Marekani, UK, Uholanzi, Ufaransa, Uturuki, Urusi, n.k.

Kwa maana moja hata nyingine, huwa watawala hawako radhi kuachia maeneo kama haya. Sisi tunalalamika ila itabaki hivyo.

MkuuMkuu Nguruvi heshima kwako.
Kwa wa Zanzibar na hii set up ya mfumo wa utawala itakuwa ni vigumu sana kuitisha kura ya maoni kuhusu kujitoa katika muungano huu, sababu kuu wanufaika wakubwa wa huu muungano ni CCM Zanzibar ambao kwa mfumo huu unawapa nafasi ya kuendelea kubakia madarakani wakitumia JMT.

Huu muungano unalindwa na kudumishwa Dodoma, nina imani kama si nguvu za dola zilizokuwa nyuma ya Jecha visiwa hivi vingekuwa chini ya Maalim Seif ambaye CCM hawaamini hatma yao chini yake. Rejea kauli ya Mkapa kuwa muungano utalindwa kwa gharama yeyote na akaonyesha kwa vitendo kwa kumwaga damu mwaka 2001, hata uchaguzi uliopita ilikuwa hivyo.

Tatizo kubwa ni unafiki mkubwa waliokuwa nao wa Zanzibari, ndani ya wabunge na wawakilishi wa CCM wanalalama na kulaumu, lakini deep within wanajua kuwa bila uwepo wao CCM wao hawatasalia madarakani kwa hiyo hata ile dhamira ya wazanzibari walio wengi ya kutaka kuwa huru nje ya muungano kwa kiu ya madaraka hawatokubaliana nayo.

Na wakiitisha kura ya maoni fairly muungano unaodumishwa na kufanywa imara kwa vifaru vya kivita hautodumu, sababu hakuna uchaguzi wowote ambao CCM hata ASP waliowahi kushinda kihalali. BWZ liko chini ya CCM, bunge licha ya kuwa na wabunge wengi wa CCM bado kwa maelekezo ya ofisi kubwa wabunge wote wa upinzani outspoken wanabanwa na kuwekewa mizengwe wasisikike.

Unadhani kwa kaliba ya wabunge kama Lusinde na bosi wao Tulia au kwenye BLW kuna anayeweza kuanzisha na kuruhusu motion ya kura ya maoni ya Zanzibar kujitoa kwenye muungano? Kwa maamiri jeshi tulio nao(Magufuli na Dk Shein) Sioni wapi itakapochipulia
 
Kwanza hiyo sheria ya kura ya maoni ilikuwa mahususi kuhusu kuunda SUK na wala si jambo lingine lolote,pili hata kama ingekuwa inahusu kuhoji muungano lakini kuna wenye mamlaka ya kuitisha hiyo kura si jambo la mtu yeyote tu anaweza kuamua,sasa inashangaza mtu mwenye akili timamu kuja na mawazo ya kipuuzi kiasi hiki ilihali anajua kabisa wengi wa hao wanaolalamikia muungano hawana mamlaka yoyote lakini pia muanzisha uzi anashangaza sana kuwashambulia Wazanzibar utadhani ni wao tu wanaolalamikia huu muungano wakati anajua kabisa hata upande wa Tanganyika wapo wasioutaka,Naamini ni chuki tu hasa za udini ndio zimemsukuma kuanzisha mada hii si kingine.
Acha kumshambulia bwana Pasco.ameeleza ukweli tukitaka kuliamua hili suala iitishwe kura ya maoni mbona ni simple tu.tena kura yenyewe ipigwe nchi nzima si Zanzibar pekeyake.
 
Inachekesha sana, nimemsikia kwa masikio yangu mawili jinsi ya Dr.Kikwete alivyojinasibu vipi ameweza kusimamia mpaka maridhiano ya kisiasa Zanzibar kupatikana; halafu leo eti unasema JMT haikushirikwishwa. Lipi CCM Zanzibakuwaondoa ye bila ya ridhaa ya Dodoma? hawawezi hata kuweka mgombea wa Urais wamtakae. Acha kusinzia, Zinduka.
Mkuu Baraghash naomba kukuunga mkono, wakati wote mimi huamini kuwa adui wa wazanzibari ni CCM tu. Mambo yote na maamuzi yote ya kisiasa ndani ya Zanzibar hufanyika Dodoma, kwa hiyo hakuna haja ya wazanzibari kuwachukia wala kuwakasirikia wamrima. Adui yenu CCM, siku mkiweza kuwaondoa na maninja wao basi mtakuwa mmeshinda.
 
Acha kumshambulia bwana Pasco.ameeleza ukweli tukitaka kuliamua hili suala iitishwe kura ya maoni mbona ni simple tu.tena kura yenyewe ipigwe nchi nzima si Zanzibar pekeyake.
Usiwafanye wenzenu wajinga, Kura tupige sote mkoloni na mkoloniwa, umeoana wapi? Mbona mulipopiga kura ya kujitawala Tanganyika mlipiga peke yenu na mkoloni akawa msimamiaji tu
 
Tunaongea sana ila katika duania hakuna taifa linalojitambua linaruhusu kataifa madogo kujiuendesha karibu na mipaka yake. Ndo yaliyopo Macao, Taiwan, Hong Kong, Gilblatar, hata visiwa vingi vidogo vinavyo zunguka Marekani, UK, Uholanzi, Ufaransa, Uturuki, Urusi, n.k.

Kwa maana moja hata nyingine, huwa watawala hawako radhi kuachia maeneo kama haya. Sisi tunalalamika ila itabaki hivyo.
Hivyo visiwa kwa ridhaa yao vingi vinajitawala, na vingine kwa mapenzi yake vimeamua kuwa chini ya tawala hizo, siyo kwa hila, vitisho, mauaji na ukandamizaji kama huu wa akina Jecha na CCM yenu
 
Hiyo Zanzibar unayoongelea ni Muunganiko wa Pemba na Unguja, nao wanahitaji kura ya maoni kubaki kuwa Zanzibar au kila kisiwa kijiamulie mambo yake
Zanzibar tafsiri yake ni Unguja, Pemba,Mombasa, Mafia na kisiwa cha Latham.
Mombasa tumeiuza kwa Kenya. Mafia na Latham vimeporwa kwa mabavu na bara. Ikiwa jina la Zanzibar linakutia kichechefu, basi kura ya maoni hiyo iishie Mafia,sio unguja na Pemba tu
 
Tunaongea sana ila katika duania hakuna taifa linalojitambua linaruhusu kataifa kadogo kujiuendesha karibu na mipaka yake. Ndo yaliyopo Macao, Taiwan, Hong Kong, Gilblatar, hata visiwa vingi vidogo vinavyo zunguka Marekani, UK, Uholanzi, Ufaransa, Uturuki, Urusi, n.k.

Kwa maana moja hata nyingine, huwa watawala hawako radhi kuachia maeneo kama haya. Sisi tunalalamika ila itabaki hivyo.
Unalijua Taifa linalojitambua au kutambulika Hivi wewe umo?Zanzibar ilianza kujitambua na kutambulika duniani kabla ya Tanganyika. Nchi ya kwanza kuwa na uhusiano wa kibalozi na USA barani Afrika ni Zanzibar.Tanganyika wakati huo inaitwa MRIMA
 
Mkuu Pasco hilo ni wazo zuri tu na lenye manufaa zaidi kwa upande wa Zanzibar.

Hapa kuna mambo mawili ya msingi, kwanza Uingereza kama tunavyofahamu ni muungano wa England, Wales, Northern Ireland na Scotland.

Pili, alie na mamlaka ya kuamua iwepo kura ya maoni ni waziri mkuu wa Uingereza ambae ni David Cameron.

Aliekuwa waziri wa nchi wa Scotland (first minister) katika serikali ya UK na anaeiwakilisha Scotland kwenye bunge la UK (house of Commons bwana Alex Salmond ndie alieitisha kura ya maoni ya Scotland kujitenga kutoka UK mwaka 2014, na hiyo ni baada ya kuomba ruhusa kutoka kwa David Cameron ambae ni waziri mkuu wa UK.

Alex Salmond akiwa kiongozi wa chana cha SNP alikuwa na "ambition" ya kuona Scotland inakuwa nchi huru bila kufuata nyuma na kuitikia kila kitu kutoka serikali ya UK.

Hali kadhalika David Cameron nae akiwa waziri mkuu wa Uingereza akatoa ahadi iliyokuwepo kwenye manifesto ya kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2015 kwamba angeitisha kura ya maoni mwaka 2016.

Lakini kiufundi ni kwamba ni David Cameron ambae amefanikisha kura za maoni ile ya Scotland na hii ya UK kujitoa kwenye umoja wa Ulaya EU ndie mwenye mamlaka ya kuitisha au kuidhinisha hizi kura za maoni akiwa waziri mkuu wa UK.

Na hata sasa waziri wa nchi wa Scotland mama Nicola Sturgeon anaandaa utaratibu wa kuomba ruhusa kutoka kwa David Cameron ili awezeshe Sctoland kupiga kura ingine ya maoni ya kutaka kujitoa kutoka Uk maana wa-scotish wanaamini kwamba wameamuliwa maamuzi ya kutoka kwenye EU bila ya wao kupenda na wangependa kuendelea kuwa wanachama wa EU wakiwa nchi huru.

Hivyo basi tukiangalia hali hiyo ya wazungu hawa na utaratibu wao waliojipangia, mimi naona itakuwa ni vigumu sana kwa Zanzibar kupiga kura ya maoni ya kutaka kujitoa kwenye Muungano na Tanzania Bara.

Hiyo ni kwasababu kuu mbili.

Kwanza, ni lazima uamuzi huo ufanywe kwa makubaliano ya raisi wa Zanzibar na raisi wa JMT na baada ya hapo suala hilo lijadiliwe na Bunge la JMT kukubalina na wazo hilo.

Hii ni tofauti na kura za maoni kama ile ya ZUK ambayo ilihusu masuala mengine kabisa.

Pili, bado katiba ya sasa haijaweka mazingira mazuri kwa Zanzibar kuweza kujiamulia kufanya kura ya maoni.

Na hata kama katiba itabadilishwa, bado haitaboresha hicho kipengele cha kuipa nafasi Zanzibar kujiamulia mambo yake yenyewe.

Hitimisho langu ni kwamba suala la Zanzibar ni gumu sana na kama hakuna tume huru ya uchaguzi kama wenzetu wa Uingereza ambao wana uhakika wa matokeo tusitegemee jipya.

Tume za uchaguzi za kiafrika zinaendeshwa kwa mtindo wa kiafrika na demokrasia ya kiafrika.
 
Back
Top Bottom