Wanywaji mnywe kistaarabu, mwenzenu huku kateketeza zaidi ya laki sita na bado anadeki bar

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,700
9,778
Majira ya usiku siku ya jana niliona ni vyema kama ningepata sehemu yenye mkusanyiko wa watu ili kidogo nirefresh mind kutokana na mawazo niliyonayo! Hivyo niliamua kuingia bar yenye hadhi kidogo! Nilisogea hadi mwisho wa bar ile kwenye kona nikaagiza chupa yangu ya fanta orange ili kuzimua!

Dakika chache, alifika mwanababa mmoja pale bar, akatazama meza iliyokuwa na mrembo akajisogeza pale na kuketi kisha taratibu akaanza mazungumzo na yule mwanadada huku wakishushia vinywaji!

istockphoto-469188298-1024x1024.jpg


Ilipofika mida ya saa tano, pombe zilikuwa tayari zimekwisha mkolea, alikuwa akimuita mhudumu na kumpatia pesa alete vinywaji hata hivyo vinywaji vyenyewe havikuwa vikiletwa, hivyo aliita wahudumu na wahudumu! Alikuwa akifuja pesa mpaka mtu najiuliza Hivi huyu ana habari ya mafuta kupanda bei kweli? Zilipomkolea zaidi, alimuita dj na kumpatia kitita ili amuweke wimbo aupendao! Dakika chache kilisikika kicheko kutoka kwenye spika kikifuatiwa na neno Jeeshii! Wimbo ule wa Altitude ulimfanya akose uvumilivu akajikuta akisimama katikati ya bar na kuanza kulisakata lumba bila aibu, jinsi watu walivyomsifia zaidi ndivyo jinsi alivyozidi kujibetua akili!

images%20(1).jpg


Kichwa kilivyomjaa, alisikika akisema "Wasambazie bia watu wooote waliomo humu ndani" kisha akatoa kitita cha pesa na kumpatia mhudumu na kumwambia,"kama pesa itapungua, wape tu, kisha niandikie bili nitalipa" Kiukweli aliokoa jahazi nami nikasogezewa bia mbili mezani

Baada ya wimbo kuisha akatamka tena kwa sauti kuu kuwa wimbo urudiwe! Kuna meza moja walikaa wakina dada tupu waliokuwa wakimtazama kimahaba! "Wapatie bia wanazozitaka za gharama yoyote ile ntalipa", alisikika mlevi mmoja huku akiyumba yumba Kisha kutoa kadi yake ya benki na kusogelea karibu na mlango wa kutokea ili kuvuta mpunga na kumpatia waiter!

Baada ya pale alisikika akisema, "Mabinti kunyweni, pesa zipo, bado kuna laki sita!" bila hiyana waliendelea kuagiza! katika cheza cheza zake akapanda juu ya meza moja iliyokuwa jilani na meza ya mabinti na kucheza juu yake, hatimaye meza ilivunjika! Aliskika akisema "Ntalipaaaaaaaa"!

Baada ya muda kidogo, alimwagiza yule mwanamke aliyekuwa naye kwenda kumnyofolea pesa! alimtajia namba ya siri kiasi kwamba watu wote tuliiskia

Alikaa akisubiri labda binti angerudi, lakini wapi! Binti alitokomea mazima!! Hapo ndipo pombe zilimtoka kichwani, akataka kuchoropoka ndani kumtazama kwa upande wa nje lakini walinzi walimzuia mpaka pale atakapolipa pesa kwanza! Aliishia kuuliza "Yule binti aliyekuwa kavaa kigauni kifupi cha blue mmemuona" pasi na msaada wowote!

photo-1579168765467-3b235f938439.jpg


Ilifikia muda nikawa nimeondoka kurejea nyumbani! Leo asubuhi wakati naelekea kwenye kutafuta nimepita njia ya karibu na pale baa, nimekuta anafanya usafi (mopping) huku mlinzi akimwambia kuwa amsubiri boss waone wanafanyeje

low-angle-view-of-a-young-man-mopping-a-bar-floor-2EFA91A.jpg


Dah! Hii dunia ni ndogo sana!

N.B: Picha hizo hazihusiani na mhusika wa tukio hilo!
 
Ila wanawake wanaokunywa pombe wengi wao wanachakaa sana, kiufupi wanazeeka.
Hao hawana pesa, wanakunywa kwa ofa.
Pombe haizeeshi ila kama huli vizuri, unakunywa pombe kali bila mpangilio si mwanaume wala mwanamke utazeeka kabla ya wakati.
 
Back
Top Bottom