Wanyonge wenzangu, bei ya Saruji huko kwenu ipo vipi?

MAMDALI

Member
Aug 13, 2015
86
123
Wanyonge wenzangu huko mkoa uliopo bei ya cement ikoje? Mimi huku nilipo Cement ya dangote 23000/mfuko na twiga ni 25000/mfuko. Bei ya Dangote kutoka 18500 mkapa 23000. Mnyonge mnyongeni lakini mnyonge kabisa.

Soma: Serikali iruhusu kuingiza saruji kutoka nje

====

Bei saruji haishikiki
09 NOV 2020

Katika baadhi ya maeneo kumekuwa na ongezeko la Sh. 3,000 hadi 8,000, mfuko mmoja wa kilo 50 ukiuzwa kwa Sh. 35,000.

Katika baadhi ya viwanda kumeshuhudiwa msururu wa magari yakisubiri bidhaa hiyo, mengi yakitoka nchi za Burundi na Rwanda na kusota kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Wafanyabiashara wa ndani wanaonunua kwa jumla bidhaa hiyo wamejikuta wakisota kwa zaidi ya miezi mitatu bila kupata kiasi walicholipia kiwandani.

Kwa mikoa iliyopakana na Kenya wananchi wananunua saruji ya nje ambayo bei yake ni kati ya Sh. 16,500 hadi 17,000 huku ya nchini ikiuzwa kwa Sh. 24,000.

Tanzania kuna viwanda vya saruji ambavyo uhudumia mikoa na kanda mbalimbali ambavyo ni Twiga Cement, Simba Cement, Nyati Cement, Tanga Cement, Mtwara Cement, Dangote, Mbeya Cement huku Kanda ya Ziwa ikiwa haina kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Viwanda vinavyotarajiwa vinavyojengwa maeneo ya Shinyanga na Bunda.

DAR ES SALAAM

Maeneo ya Tandika, Temeke, Kibamba, Ukonga na Gongo la Mboto, kwa sasa mfuko mmoja wa saruji unauzwa kati ya Sh. 15,000 hadi 16,000 kutoka Sh. 14,000 hadi 14,500.

Muuzaji wa duka la vifaa vya ujenzi lililopo Mombasa, Ukonga, Jinnihi James, alisema saruji inapokuwa dukani kwake ya Twiga, huuzwa kati ya Sh. 15,000 hadi 16,000 ingawa kwa hivi sasa hana bidhaa hiyo.

“Kwa takribani mwezi mmoja sina saruji, nikiuliza wanaotusambazia mara kwa mara mfano saruji ya Twiga, wanasema uzalishaji umeshuka na mahitaji yapo zaidi,” alisema James.

ARUSHA

Katika Jiji la Arusha bidhaa hiyo imepanda kutoka Sh. 14,500 hadi 19,000 kwa baadhi ya maduka ya ujenzi kwa kipindi cha miezi mitatu tangu Julai, mwaka huu.

Mfanyabiashara na mmiliki wa duka la ujenzi la Tulivu Hardware, alisema mfuko mmoja wa saruji ya Simba uko juu, tofauti na ya Twiga, Kilimanjaro na Moshi Cement.

NGORONGORO

Mfuko mmoja wa saruji ya kampuni ya Simba unauzwa Sh. 25,000 hadi 35,000. Akizungumza na gazeti hili, Lotha Saigurani, mkazi wa Loliondo, alisema awali walinunua kwa Sh. 10,000 na sasa imepanda zaidi.

Katika Mji Mdogo wa Namanga uliopo mpakani mwa Tanzania na Kenya, saruji inauzwa Sh. 18,000 bei ambayo wameizoea tangu awali.

TANGA

Mkoani Tanga ambako kuna kiwanda cha Tanga Cement, bei imepanda kutoka Sh. 12,000 hadi Sh.14,000.

"Ukweli ni kwamba kuna maeneo inauzwa 13,000 na maeneo mengine mpaka 15,000 kwa saruji ya kampuni ya Simba, lakini upo uhaba wa saruji hapa Tanga," alisema Denis Komba, mkazi wa jijini hapa.

KILIMANJARO

Mfuko mmoja wa kilo 50 umepanda kutoka Sh. 14,500 hadi Sh. 21,000, huku baadhi ya wafanyabiashara wa jumla wakilalamikia kutopatikana kwa saruji kutoka viwanda vya kutengeneza bidhaa hiyo nchini.

Mmoja wa maofisa masoko wa kiwanda cha saruji cha Moshi (hakutaka kutajwa jina lake) alisema bidhaa hiyo imepanda kutokana na uhitaji kuwa mkubwa sokoni, lakini bado wanawauzia mawakala wao mfuko mmoja kwa Sh. 12,500 na kuwaelekeza wasiuze zaidi ya Sh. 14,000.

MANYARA

Mji wa Babati bidhaa hiyo haikamatiki licha ya kuwa adimu, imepanda kutoka 15,000 hadi 20,000.

Mfanyabiashara wa saruji na mkazi wa Babati, Nelson Mosha, alisema hadi sasa hawajui kinachosababisha bidhaa hiyo kupanda bei na kushuka na kuiomba serikali kuingilia kati.

Msimamizi wa Timber & Yard, Emmanuel AsanteRabi, wauzaji wa saruji, alisema hali hiyo ya bei imekuwa ikibadilika kutoka Sh. 18,000 kwa jumla hadi 19,000 kwa mfuko mmoja wa kilo 50, saruji ya Simba.

MOROGORO

Wakala wa mauzo ya saruji kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro duka la rejareja, Zuberi Ngonyani, alisema bei ya saruji imepanda kutoka Sh. 13,500 hadi Sh. 17,000, bei ambazo wanauza kwa wateja wao kutokana na kupanda kwa gharama za ununuzi.

Naye Mariamu Abasi alisema kwa sasa anashindwa kuendelea na ujenzi kutokana na bidhaa hiyo kupanda na kuiomba serikali kuingilia kati.

Muuzaji wa jumla ya saruji, Riziki Hardware, alisema ununuzi wa saruji umepanda viwandani kwa sasa wanalazimika kuuza Sh. 13,000 hadi 16,000.

SONGEA

Mkoani Ruvuma mfuko mmoja uliokuwa unauzwa Sh. 14,500 sasa ni Sh. 22,000 na kulazimu wengi kusimamisha ujenzi.

Stanlei Mgaya, maarufu kwa jina la Mwanzo Mgumu ambaye ni mfanyabiashara kwenye eneo la soko kuu la Songea mjini na Somoni Mkoma, mkazi wa Lizaboni waliiomba serikali kuingilia kati.

Songea na Ruvuma wanategemea saruji kutoka katika kiwanda cha Dangote Mtwara, lakini kwa hivi sasa waliyo nayo ni ya kiwanda cha Twiga.

DODOMA

Mfuko mmoja umepanda kutoka Sh. 15,000 hadi Sh.18,500 kwenye maduka ya jumla huku wauzaji wa rejareja wakiuza kwa Sh. 19,500 hadi Sh. 20,500.

Akizungumza na Nipashe jana, Hamidu Msemo, ambaye ni muuzaji wa rejareja, alisema wanashindwa kumudu gharama hizo na kuhofia kupata hasara kutokana na bei kubadilika mara kwa mara.

“Mimi nina mwezi mzima sijanunua saruji kuweka dukani kwangu, na hii inatokana na kuhofia kupata hasara kwa sababu ya kushuka na kupanda kwa bei mara kwa mara,” alisema Msemo.

IRINGA

Bidhaa hiyo imepanda kutoka Sh. 13,500 hadi 22,000 tangu mwezi Septemba.

SHINYANGA

Sasa mfuko mmoja umepanda kutoka Sh. 17,000 hadi Sh. 23,000, huku ikiwa adimu kwenye maeneo mengi na watu wengi kusitisha shughuli za ujenzi.

Mmoja wa wafanyabiashara Shinyanga mjini Emmanuel Mboya, akizungumza na Nipashe jana, alisema bidhaa hiyo imepanda bei kutokana na kuadimika na kwamba matofali ya saruji yamepanda kutoka Sh. 1,100 hadi 1,400.

MWANZA

Bei imepanda kutoka Sh. 18,000 hadi 23,000. Amosi Kazungu mkazi wa Nyamagana na Rediance Rayson mkazi wa Magu, walisema bei hiyo imewakwamisha kuendelea na ujenzi.

TARIME WANUNUA YA KENYA

Maeneo ya Tarime wananchi wanatumia saruji kutoka Kenya ambayo inauzwa Sh. 16,500 hadi 17,000 huku ya Tanzania ikiuzwa Sh. 24,000.

LINDI NA MTWARA

Inauzwa kati ya Sh. 16,000 hadi 17,000 ikiwa ni ongezeko la Sh. 3,000 hadi 4,000. Sababu kubwa inayoelezwa ni kupungua kwa uzalishaji katika viwanda vya Dangote na Mtwara Cement.

PWANI

Imepanda kutoka Sh. 14,500 hadi 17,000.

KATAVI

Ilikuwa Sh. 20,000 sasa ni Sh. 24,000, walikuwa wakitegemea kiwanda cha Dangote, lakini imeadimika.

MAGARI YA NJE YASOTA

Nipashe ilishuhudia zaidi ya malori 100 yakiwa yameegeshwa kiwanda cha Wazo Hill (Twiga), Tegeta jijini Dar es Salaam, yakisubiri bidhaa hiyo.

Wakizungumza na Nipashe jana baadhi ya madereva ambao wameweka kambi kusubiri kupakia saruji hiyo kutoka Tanzania, Rwanda na Burundi, walisema kwa sasa wanalazimika kukaa hapo hata zaidi ya wiki moja.

Abdulkarim Rashid, dereva kutoka nchini Rwanda aliiambia Nipashe kuwa tangu afike nchini ana siku ya tano na hakuna dalili ya kupakia mzigo.

“Nina siku ya tano nimekuja hapa na hakuna dalili ya kupakia, kama unavyoona hata sehemu ya parking kumejaa, wote hawa wanasubiri foleni yao ifike na hatujui ni lini,” alisema Rashid.

“Kipindi cha nyuma tulizoea tukifika leo, tunapakia kesho yake na kurudi nyumbani, lakini sasa imekuwa tofauti.

Hii inatusababishia hasara kubwa sana kwa sababu inabidi tuingie gharama zaidi kwa hizi siku zinazoongezeka tukiwa hapa.”

Mohammed Ally, alisema anatoka Kahama mkoani Shinganya na ana siku ya nane hajapata saruji.

“Hatujui kwa nini kwa sasa tunachelewa sana kupakia, ila tunaona siku hizi gari zinaingia kwa wingi kutoka nchi za jirani tofauti na kipindi cha nyuma labda huenda ndiyo sababu foleni imekuwa kubwa.”

KAULI YA SERIKALI

Mwezi uliopita, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Riziki Shemdoe, alikwenda mkoani Tanga kuzungumza na wenye viwanda vya saruji na kuwasihi kiwango cha uzalishaji.

Alisema uzalishaji huo utasaidia kukabiliana mahitaji makubwa ya miradi kimkakati inayotekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, serikali ipo katika mkakati wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo kimsingi hutegemea zaidi matumizi ya saruji.

“Tusingependa kusikia visingizio vyovyote katika hilo, tunahitaji muongeze uzalishaji wa bidhaa hii, ieleweke kwamba taifa lina uhitaji mkubwa wa saruji na hatuna mpango wa kuchukua kutoka nje, tutanunua kutoka kwenye viwanda vyetu vya ndani.”

SIMBA CEMENT

Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Simba Cement, Benny Lema, alisema kukosekana kwa umeme wa uhakika, kumepunguza kasi ya uzalishaji wa bidhaa hiyo na kusababisha kupungua kwa saruji kwenye soko la ndani.

Aliiomba serikali kuangalia upya namna ya kuviunganisha viwanda hivyo na bomba la gesi ili kuvipa uhakika wa umeme katika shughuli za uzalishaji.

MBEYA CEMENT

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya saruji ya Mbeya, Khaled Ghareib, alisema kupanda kwa saruji kunatokana na hali ya usambazaji na uhitaji kuwa mkubwa na kushindwa kutosheleza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Neelkanth Ltd, Amboni jijini Tanga, Rashid Lihemba, alisema awali walikuwa wakisafirisha saruji kwenda nje tani 20,000 kwa mwezi, lakini kwa sasa wanasafirisha 10,000.

“Tumesikia agizo la serikali na tulikuwa na mpango wa kuongeza uzalishaji huko siku za usoni kutoka asilimia 75 za sasa, hadi kufikia asilimia 90 ambayo ni sawa na tani 3,600 kwa siku," alisema Meneja Msaidizi wa Maweni Lime Simon Kikota.

*Imeandikwa na Richard Makore (Mwanza), Godfrey Mushi, Allan lsack, (Arusha), Christina Mwakangale na Beatrice Shayo (DAR), Woinde Shizza (Ngorongoro), Lulu George (Tanga), Mary Mosha (Moshi), Jaliwason Jasson na Daniel Sabuni (Manyara), Christina Haule, Morogoro, Gideon Mwakanosya (Songea), Said Hamdani (Lindi), Neema Hussein (Katavi), Renatha Msungu na Ibrahim Joseph, (Dodoma), Francis Godwin (Iringa), Marco Maduhu (Shinyanga) na Julieth Mkireri (Kibaha).
 
Wanyonge wenzangu huko mkoa uliopo bei ya cement ikoje? Mimi huku nilipo Cement ya dangote 23000/mfuko na twiga ni 25000/mfuko. Bei ya Dangote kutoka 18500 mkapa 23000. Mnyonge mnyongeni lakini mnyonge kabisa.
Upo mkoa gani mkuu
 
Wanyonge wenzangu huko mkoa uliopo bei ya cement ikoje? Mimi huku nilipo Cement ya dangote 23000/mfuko na twiga ni 25000/mfuko. Bei ya Dangote kutoka 18500 mkapa 23000. Mnyonge mnyongeni lakini mnyonge kabisa.
Wewe uko mkoa gani?
 
Huko ulipo ni wapi?.
Kwa kuwa uchaguzi umeisha cement itarudi kwenye Hali ya KAWAIDA.
Wazalishaji wanaogopa kuzalisha bidhaa nyingi kwa hofu ya kutokea matukio mabaya nchini kipindi hichi Cha uchafuzi .
Alafu mzigo ukabaki stop ikawa ni hasara kwao.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Huko ulipo ni wapi?.
Kwa kuwa uchaguzi umeisha cement itarudi kwenye Hali ya KAWAIDA.
Wazalishaji wanaogopa kuzalisha bidhaa nyingi kwa hofu ya kutokea matukio mabaya nchini kipindi hichi Cha uchafuzi .
Alafu mzigo ukabaki stop ikawa ni hasara kwao.

Wewe unaongea nini ndugu, Cement ipo madukani tatizo ni bei na sio uhaba wa cement.
 
Katavi imefika 23,000 ila huku ikishuka sana huwa ni 20,000 mwaka jana ilifika 17,000 nilishangaa sana nahisi haijawahi na haitotokea tena.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom