Wanyonge wameungana na mabeberu wamewasikiliza

Najiuliza tu! Hivi kweli kuna mwanasiasa anaeweza kusimama jukwaani akailaumu serikali kuwafukuza shule wanaopata mimba wakiwa shuleni na wananchi wakamwelewa kabisa kama anahoja?

Au kuna mzazi mama yeyote anaejua uchungu wa mwana ambae anaweza kwenda kumuandikisha mwanae shule waliyojazana wazazi?
 
Binafsi nmefurahi kinyama,wanyimwe tuuu hakuna namna kama wana akili hii alarm si nzur kwao ila sabab wajinga wajinga hawataelewa na wanaomzunguka watampa ngojera nzuriiiii tofauti na uhalisia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mara ya kwanza nimeanza kuona Watanzania wamechoka na matamko yenye kuwaminya. Watanzania wamechoka kutumiwa kwa kudanganyiwa unyonge.

Unaweza kukubali ama kukataa, lakini nimeona na nimesikia, idadi kubwa ya Watanzania wanyonge wamefurahi nchi yao, kunyimwa mkopo na Bank ya Dunia.

Watanzania hawa hoja yao kubwa ni kubaguliwa kwa mtoto wa kike kupata elimu, huku mkopo ukilenga kuboresha elimu. Wengi wamehoji elimu ipi inayoboreshwa ikiwa mtoto anaepata mimba na kuzaa, anaishia kubaki mbumbumbu yeye na kizazi chake.

Wengine wametolea mfano wa mabinti waliobakwa ambao kupata mimba si kupenda kwao, wengine wanasema mtoto kupata mimba na kuendelea na masomo, kulipunguza vifo vya watoto wanaojaribu kutoa mimba, kwa nia ya kuendelea kusoma na kutokuonekana malaya, kama ilivyokuwa ikitafsiriwa.

Wapo pia waliosema wanadanganywa ili waendelee kuwa wajinga, ikiwa watoto wa vigogo wanasoma private school, baada ya kujifungua.

Kwa mitazamo hiyo michache, inaonesha sasa watanzania si wajinga tena. Wanajua jema na baya, wanajua wanahujumiwa na wimbo mzuri 'UNYONGE'.

Kuna mtu kaita jopo la watu anaowaamini ili kujadili hili jambo. Lakini binafsi nataka kumwambia hilo jopo halitamshauri, wala halitampa ukweli wa kwa nini mkopo umezuiliwa.

Lakini ukweli ni kwamba; mdomo wake unamponza na unawaponza wanyonge wake wote. Miaka yote tangu tuwe huru, hakuna serikali iliyosema inarudisha wanafunzi wajawazito shuleni bali, walikaa kimya na walioachiwa kuwafukuza ni walimu wa wanafunzi hao, pia mwanafunzi mwenyewe alijifukuza baada ya kupata mimba, kwa sababu alijua hawezi kusoma tena.

Kauli yake ya wazi imeleta yote haya, imewafunua wanyonge akili zao, nao wamejua Elimu ni haki ya kila mtu na, kibaya zaidi, wamejua mkopo wanalipa wao.

Hii si ishara nzuri kwa mtawala yeyote mwenye nia yake kwa wanyonge. Mmoja wa watawala ni Sabaya, nimeona wananchi wamemkataa palepale mkutanoni baada ya kuongea utumbo wake kwa kuwahusisha waganga wa kienyeji na mimba za utotoni.

Sinema ukiichoka huwa haiwezi kukuvutia, hata kama ikitangazwa kutazamwa bure.

Asilimia tisini wamefurahi kunyimwa mkopo. Asilimia tano ni MATAGA ambao wameishia kulaani vibaraka wa mabeberu kuwashawishi mabeberu kuwanyima mkopo.

Hawa wao wanakauli ya hatusomeshi wazazi. Wengine wanasema tumesalitiwa..

Kifupi hawajui wasimamie lipi kwenye hili kwa sababu, wanajua mkopo haungepelekwa mashuleni, bali kuwanufaisha wao.

Asilimia tano nyingine, hawa ni wale ambao wapo wapo, wao wanaamini kauli ya mtu mkubwa ni kauli ya mwisho na haipingwi, japo hata wao wanapenda watoto wao wasome. Wapo kishabiki tu na pengine hawajui kama mkopo ulikuwa ni kwa ajili ya elimu.

Nawakumbusha tu; Mabeberu hawaji kuwapanda mabinti zetu ili kuwapa mimba, tunawapa wenyewe kisha tunavimba kuwafukuza mashuleni.
tuna jiwe la ajabu halijawahi kutokea tanzania hilo jiwe huwa linajikwamisha lenyewe kwa kauli zake halafu baadaye linaanza kutafuta mchawi nani? Mfano wa kauli zake zitakazo mkosti ni 1.mpaka 2020 litakuwa limeua upinzani,2. Sisi ni dona cantri tuna pesa za kutosha ni matajiri,3. Katika awamu yake anataka matajiri waishi kama mashetani, 4. Kuna mahali aliwaambia wapiga kura wake kwamba yeye hakuwapelekea tetemeko. 5. Tena akasema Kama kuna watu wamekula hela flani kupitia midomo yao basi zitawatokea sehemu yeyote yenye tundu .6. Hasomeshi wazazi.7.tena akatangaza kwamba wale ambao ndugu zao wanapotea wanatekwa wanauawa wakae kimya na wa wasilie wala kusema chochote hasa kuwatuhumu wale wenye jukumu la ulinzi ukinyanyua domo utakiona cha mtema kuni n.k sasa hapa kwa kauli hizi kweli bado mtu atafutamchawi ni nani? Kiufupi huyo jiwe atavuna alichokipanda ktk tanzania na dunia hii
 
Najiuliza tu! Hivi kweli kuna mwanasiasa anaeweza kusimama jukwaani akailaumu serikali kuwafukuza shule wanaopata mimba wakiwa shuleni na wananchi wakamwelewa kabisa kama anahoja?

Au kuna mzazi mama yeyote anaejua uchungu wa mwana ambae anaweza kwenda kumuandikisha mwanae shule waliyojazana wazazi?
Wewe una mtoto wa kike? Unataka ndoto ya mtoto wako ifutwe kisa mimba, kama yeye hana future unategemea mtoto wake naye atakuwa na future yoyote? Kila mtu anahitaji second chance.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najiuliza tu! Hivi kweli kuna mwanasiasa anaeweza kusimama jukwaani akailaumu serikali kuwafukuza shule wanaopata mimba wakiwa shuleni na wananchi wakamwelewa kabisa kama anahoja?

Au kuna mzazi mama yeyote anaejua uchungu wa mwana ambae anaweza kwenda kumuandikisha mwanae shule waliyojazana wazazi?
Nyumbani kwako ujauzito wa mkeo na mtoto wako mchanga, kumeathiri vipi familia yako, hasa watoto wako ambao wanaenda shule wanarudi nyumbani kuna mzazi/mjamzito?
 
Back
Top Bottom