Wanyonge ni watu ambao hawana nguvu ya kuwasaidia kutatua kero na matatizo yao katika nchi

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,318
8,229
Wanyonge ni watu ambao hawana nguvu ya kuwasaidia kutatua kero na matatizo yao katika nchi.

Zamani sana tulishindwa kutambua maana ya Wanyonge.. Ila leo hii mimi nimeelewa kiurahisi sana nini maana ya wanyonge.

Wanyonge ni watu ambao hawana nguvu ya kuwasaidia kutatua kero na matatizo yao katika nchi.

Wanyonge hawana nguvu kuwaambia viongozi watatue matatizo yao, wanyonge hawana sauti katika jamii.

Kiongozi anaposema mimi ni kiongozi wawanyonge maana yake ni kwamba yeye ameamua kuwa upande wa watu wenye shida, kero na matatizo mbalimbali. Na yupo tayari kuyatatua muda wowote.

Katika hili mbunge hawezi kuwa mnyonge, waziri hawezi kuwa mnyonge na kiongozi mwingine ambaye amejiweka katika muhimili wenye nguvu hawezi kuwa mnyonge.
 
Back
Top Bottom