Wanyonge ni kina nani?

j kisumu

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
289
236
Nimekuwa nikisikia mtu anasema fulani ni kiongozi wa wanyonge. Hivi kweli kwa miaka 55 ya Uhuru mtu unaweza kujivunia uwepo wa wanyonge ndani ya nchi yako?

Wanyonge ni kina nani? Kwanini wawepo ndani ya nchi miaka yote hiyo? Je wale watu wenye ulemavu waliokuwa wanakula kichapo Jana kutoka kwa mapolisi ni kundi gani?

Naombeni majibu ya maswali haya yanayonitatiza
 
Wakiacha. Kupanua mavitambi hutawah kuskia
Nchi kubwa kama hiii
Ikiwa na,wanyonge
 
Wanyonge ni wale wanaonyanyasika na kupewa vipigo, nenda kamnyanyase Chenge uone moto wake
 
Hatariii...wanyonge ni masikini, watu wa hali ya chini, walalahoi, hohehahe, watu wasiopatiwa haki zao za msingi, wanaonyanyaswa ( kwa tafsiri isio rasmi)
 
Wanyoge Ni Wale Walionyongwa Na Serikali Ya Mnyonge Akiiba Kuku Wanamuua Ila Ngeleja Akiiba Mabillion Nani Wa Kumgusa
 
Back
Top Bottom