Wanyalukolo wazuia ndugu yao kuzikwa bila kulipwa mahali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanyalukolo wazuia ndugu yao kuzikwa bila kulipwa mahali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Che-lee, Jun 14, 2011.

 1. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dunia haiishi vituko! Umetokea mtafaruko huko songea baada ya wazazi wa marehemu Esta kihwele wa tosamaganga iringa kuzuia kuzikwa kwa binti yao kisa mkwe wao hakumaliza kulipa mahali ya 900000, alilipa 400000 tu! Hivyo baada ya binti yao kufariki na watu wakiwa tayari wameshaliandaa kaburi, baba wa binti huyo Mzee Kihwele aliamuru mwili usafirishwe kwenda iringa tosamaganga! Chanzo tbc ccm.
   
 2. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado akili yangu haikai sawa juu ya hili!! Vava mwagito de!!
   
 3. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  no comment! wapo correct kabisaa kuzuia, tena bint? mila bana very interesting.
  mie bibi yangu pia alizuiwa kuzikwa kisa babu hakumalizia sh 30, hivo watoto wake
  ndo wakamalizia hiyo sh 30/= then tukaruhusiwa kumzika
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Kwa watani wangu wa huko Tarime hili ni jambo la kawaida. Jidanganye ukae na mtoto wa Kikurya hujatoa mahari kisha afariki nawe ujipendekeze kumzika bila ya kutoa mahari; ukisamehewa sana haki yako itakuwa mapanga ya shingo tu!!!
   
 5. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  nadhani ni "mahari" na siyo mahali mkuu
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Wanyalu wenzangu hii nimeipenda sana! Nikumbuka nyumbani kweli,
   
 7. A

  Aine JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa najiuliza hilo kaburi lililochimbwa Songea inakuwaje? mila zingine bwana hazina maana yoyote, kusumbua maiti tu, kwani akizika halafu mkamuambia taratibu inakuwaje na itapunguza nini? Out of date kabisa, mimi sijaipenda kabisa na sioni logic hata kidogo
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli mahri ni deni ambalo ni lazima lilipwe kama deni lingine miongoni mwa MALI au WARITHI wa marhum.
   
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sasa imeishaje?
   
 10. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Du hiyo kali....umenifurahisha,eti chanzo ni tbc ccm
   
 11. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Bwana harusi (mfiwa) katendewa sawasawa kabisa na alistahili hivyo!

  Hapa msiba hauwezi kutumiwa kama "defensive" ya yeye kuruhusiwa kuzika kwani hio lilikuwa ni deni, mahari huwa haikopwi.
   
 12. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Dawa ya deni kulipa,si walipe tu wakamzike marehemu.
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ndimgaya sida beeh
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hiyo 900,000 si ndio gharama yenyewe ya usafiri? Huyo mzee hakumpenda mkwewe
   
 15. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2011
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  ha ha mkuu duh ngoja nikalipe mahari yote, manake nataka kuoa mkulya.
   
 16. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo dada yetu wa bba inabidi amweleze erenest mapemaaaaaaaaaa!
   
 17. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  samahani sijaelewa vizuri, mahari ilikuwa milioni moja na laki tatu au ulikusudia laki moja na elfu thelathini? maana kama hiyo mahari ni milioni moja na laki tatu basi wazazi nao wana makosa kwa kumkandamiza mkwe wao, pia muowaji ana makosa mpaka anakubaliana na kiwango hicho manake ana uwezo mzuri, sasa mbona hakumaliza? Jamani mahali ni mali ya binti anayeolewa na soyo ya wazazi, kwahiyo ilitakiwa binti ndiye amtajie mchumba wake, naamini kama huyo marehem ndiye angemtajia huyo kaka mahari asingetaja kiasi hichi chote.
   
 18. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwani wewe ukienda kanisani au msikitini na kuomba usiku kucha au hadi unagaagaa chini na kulia Mungu akusaidie huwa una logic gani? Una ushahidi gani kama huyo unayemuomba yupo? Similarly, mila na zenyewe zina utaratibu wake. Na kwa koo zinazofuata sana mila, msipotekeleza hayo unaweza kukutana na magumu yasiyotarajiwa. Au watoto wake wakapata shida sana katika maisha. Ni suala la imani na taratibu. Kwa hiyo sioni kosa la hawa kusimamia mila na taratibu walizojiwekea
   
 19. N

  NCHABIRONDA JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haaaaaa!! Huo mkasa nikama vile umenifumbua macho! Ebu ngoja nikamalizie deni la wa2 yasije yakanikuta kama ya huyo ndugu ye2. na nyie WAZAZI wenye mabinti nyie ndo chanzo cha haya yote, mahari kubwaaaaaa!! Mpaka inamulazimu kijana anaamua kutoa advance kwanza ndo anachukua binti.
   
 20. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa nikuwa mkwe aliliandaa kaburi la sakafu likiwa na mfuniko na alitumia gharama ya 600,000/ kuliandaa na vyakula vingi sana!! Hivyo awambia waombolezaji wale tu chakula kwakuwa msiba ushaenda unyaluni!! Mwekiti wa s/mtaa alisema suala hilo ni la kindugu zaidi!!
   
Loading...