Wanyakyusa na ujuzi wa Kuchunguza na kupasua maiti

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
WANYAKYUSA NA UPASUAJI WA MAITI

Afrika haikuwahi kuwa na wajinga kiasi hicho ndio maana watu walifuatwa kufanywa watumwa na kwenda kujenga Ulaya, ila ni lazima kuwalisha waafrika matango pori kwa sababu ya shida zao ili waamini kweli walikuwa wajinga.

Hebu leo tutazame kabila la Wanyakyusa na namna walivyokuwa wakifanya uchunguzi wa maiti.

Katika utamaduni wa wanyakyusa enzi hizo za zamani, baada ya marehemu wao kufariki, muda mfupi baada ya kifo chake watu hawakutakiwa kulia kwa sauti na sababu kubwa waliamini kuwa marehemu alitakiwa kupoa kwa utulivu, yaani hawakutaka kumsumbua marehemu wao, dah.

Baada ya marehemu kukata roho na kupoa, taratibu nyingine za kifo na maandalizi ya mazishi hufanya, lakini kwa upande mwingine kuna watu wanakuwa wakiendelea kutoa huduma kwa maiti kama vile kumkanda kanda na kumnyoosha viongo vyake ili marehemu asikakamae na wengine walikuwa wakipasha mikono yao moto na kumshikashika marehemu kichwani kwa ajili ya kupunguza baridi.

Baada ya taratibu zote kukamilika na siku ya kumzika marehemu kufika, marehemu huviringishwa Katika mkeka na kufungwa kwa kamba ambayo inakuwa haijakazwa sana ili kufanya urahisi wakati wa kumfungua makaburini.

Maiti baada ya kufikishwa makaburi, mtu Maalumu kwa ajili ya upasuaji alikuwa anawasili na kufanya kazi yake,

Zoezi la kumpasua maiti ili kujua chanzo cha kifo chake hufanyika makaburini tofauti na sayansi ya sasa ambayo zoezi hilo huifanyika Katika chumba Maalumu Katika hospitali.

Maiti kwa mujibu kwa taratibu za Kinyakyusa alikuwa akipasuliwa kwa kutimia mti mkali wa muwanzi ulokuwa na uwezo wa kumchana maiti upande wa tumbo ili kugundua kitu gani kiliweza kumuua marehemu lakini kabla ya kumpasua maiti, mpasuaji alitumia udongo aloupata hapo makaburini sehemu maiti alipolazwa na udongo huo ulitumika kumchora marehemu sehemu ambayo mpasuaji alikusudia kupitisha muanzi kwa ajili ya upasuaji huo, aise hawa jamaa walikuwa na teknolojia, ila wazungu waliwaovateki paaap !

Baada ya maiti kuwa amepasuliwa vitu kadhaa viliweza kutoa ishara ya nini kilikuwa chanzo cha kifo cha marehemu, kwa mfano kama katika maiti, nyongo yake ilionekana kuwa na mafuta mafuta, basi waliamini kuwa marehemu huyo alikufa kwa kulogwa au kufanyiwa uchawi, au kama maiti matumbo ya marehemu yangeonekana kuwa yamesukwa sukwa basi hiyo ilikuwa ni dalili ya ugonjwa wa matoki.

Mambo mengine yalikuwa yakionekana kwa marehemu yaliweza kutolewa tafsiri yake na mpasuaji kama vile ifanyikavyo sasa.

Ila swali la kujiuliza, ilikuwaje utaalamu huo wazee hawakuufundisha au kuirithisha kwa vijana wao, kama utaalamu huo ungerithiswha leo sayansi ingefeli kweli kugundua kifo halisi na kifo cha kutengeneza ?

Hongereni sana Wanyakyusa almaarufu kama Wakonde.

Idd Ninga
Arusha.
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160
 
Uongo mkubwa hakuna kitu kama hicho unyakyusani.

Ninachojua ni kwamba walikuwa wananchunguza Mnyama kama ngombe endapo kafa kwa ushirikina. Walikuwa wanaichunguza nyongo yake lakn sio ulichoandika hapo
 
Kule ni uchawi tu na mtu akifa ni mkeka anazikwa shughuli imeisha.

Kufukua maiti hayo maneno tu ila yote mengine wanafanya kwa upendo tu.

Hao wanalia mwezi mzima mtu akifariki huku wanatembea kwa magoti,alafu useme hawalii mpaka badae
 
Back
Top Bottom