Wanufaika bodi ya mikopo tupaze sauti bila kuchoka haki itendeke huo ni wizi mkubwa

Mm kwa kweli hii dhambi inanitafuna lakn siwezi kulipa,labda wanikamate wenyewe..kwenye taasisi nnayoifanyia kazi tuliandika majina wote tuliosomeshwa na Loan board..majina yakaenda..wenzangu wote kuanzia mwaka juzi wanakatwa..mm peke yangu ndo sikatwi

Sasa maumivu na usumbufu wanaokutana nao ni shida..Mara deni lizidi,mara akatwe deni lipungue kdg,yani shida tupu
Umemaliz chuo 2014?
 
Mimi inaonyesha wamenikata 141k katika mshahara huu wa june lkn ukiangalia tofauti ya Deni kwa mwezi June na Mei ni 31k sasa sijawaelewa kabisa huh sio utapeli ni ujambazi kabisa na wanatakiwa kuwa mahakamani na watanieleza kwa kweli...
 
Kama retention fee imefutwa na bado wamekata basi hatua stahiki zichukuliwe!

Mkuu utamchukulia hatua nani? Taasisi zote za serikali zina kinga ya kutoshtakiwa isiyo rasmi. Hao jamaa wa loan board huwa wanabiashara zao hasa za miamala ya simu, hivyo hizo hela huwa wanazizungusha kisha wanazofundisha muda watakao.
 
Back
Top Bottom