Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,901
- 1,338
MHE. WANU HAFIDH AMEIR AJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA WA SERIKALI ZA MITAA
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Wanu Hafidh Ameir amejiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa linaloendelea nchi nzima tangu 11 - 20 Oktoba, 2024.
Mhe. Wanu Hafidh Ameir ametoa wito kwa wananchi ambao bado hawajajiandikisha Wajiandikishe katika Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa ili wapate haki yao ya Msingi ya Kupiga Kura kuchagua viongozi ifikapo tarehe 27 Novemba, 2024.
Aidha, Wanu Hafidh Ameir amefurahishwa na muda mchache sana (Dakika Moja) unaotumika kuwaandikisha wananchi, hivyo wananchi watahudumiwa kwa muda mchache kisha kuendelea na majukumu yao.