Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,204
- 128,012
Kati ya wale madiwani kadhaa wa Arusha waliovuliwa udiwani kuna Rasta mmoja aliyejipatia umaarufu kwa jina la Charles David Mpanda. Jamani diwani rasta wa Arusha kata ya Kaloleni kwa tiketi ya chadema ila kwa sasa amevuliwa uanachama na udiwani CDM na anatafutwa na jeshi la polisi mkoani Arusha kwa wizi wa fedha tathlim USD 16,400/= alioufanya kwa dada Magreth ambaye alikua ni mchumba wake kabla na baada ya kuukwaa na kutoswa kwenye udiwani kata ya Kaloleni kupitia Chadema Arusha mjini.
Diwani Rasta aliyekua akiwakilisha kwa tiketi ya CDM kaloleni Arusha alikua ni mmiliki wa kampuni ya utalii jijini arusha kwa jina la AFRICAN ZOOM , Na dada Magreth ambaye alikua ni mchumba wa Rasta naye alikua akimiliki kampuni yake ya utalii kwa jina la TANGANYIKA ACCENT ROOT.
Baada ya kuanza uhusiano wa kiuchumba baina ya diwani Rasta na dada Magreth waliamua kuunganisha kampuni zao zote na kuifanya kampuni kuwa moja na kuitwa AFRICAN ZOOM & TANGANYIKA ACCENT ROOT na Diwani Rasta ndiyo aliyekua mteule wa kusign Cheque zote na kutoa pamoja na kupokea fedha zote ktk matumizi ya kampuni hii kupitia bank .
Baada ya diwani rasta kupigwa chini katika kiti cha udiwani wa Chadema kata ya Kaloleni Arusha hivi majuzi amemuibia mchumba wake USD 16,400 kwenye kampuni yao na amekimbilia Marikani leo hii. Dada Magreth amegundua kuwa diwani rasta ambaye alikua ni mpenzi wake kamuibia na ametorekea marekani na kimada wa kizungu baada ya kusikia kua jamaa alikua anaranda mitaani kumtafuta mtu wa kumkabithi gari ili asepe tena gari ambalo alipewa kwa ajili ya kutembelea na Dada Magreth kipindi cha kazi yao ya pamoja ya utalii. Nawakilisha .
N.B kama kuna muandishi wa habari mwenye shida ya kuwasiliana na Mchumba wa Diwani Rasta wa kaloleni Arusha na kumuhoji zaidi juu ya hili na kujua undani wa tukio hili la uwizi wa USD 16,400/= ani- PM.
Mpaka naondoka mitamboni mtaa wa SOWETO mkoani Arusha, dada Magreth aliyeibiwa pesa za kampuni na diwani rasta kwa sasa yupo safarini kuelekea Marekani kumkamata Rasta uyu aliyekimbilia huko baada ya kupata dada wa kizungu kwa jina la Pamela mkazi wa America .