Wanne watimuliwa CCM Bukoba kwa usaliti

October

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
2,145
91
SIKU chache baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, wanachama wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Bilele, Manispaa ya Bukoba
mkoani Kagera, wamefukuzwa uongozi na kunyang'anywa kadi za chama hicho kwa kudaiwa kukisaliti chama.

Katibu wa CCM wa Kata ya Bilele, Bw. Rashid Hassan alisema kuwa uamuzi huo ulichukuliwa na Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Kata hiyo, katika kikao chake kilichofanyika Novemba 12, mwaka huu.

Bw. Hassan alisema miongoni mwa tuhuma zilizothibitishwa kuwahusu wanachama hao ni pamoja na kukisaliti chama hicho kwa kushirikiana na wapinzani kufanya kampeni waziwazi, za kuwapinga wagombea wa CCM katika ngazi za udiwani, ubunge na urais kwa kutumia dhamana waliyopewa na chama hicho.

Aliwataja waliovuliwa uanachama pamoja na uongozi kuwa ni Bw. Uddi Miruko, ambaye ni Katibu Mwenezi wa Kata ya Bilele na Mwenyekiti wa Mtaa wa Uhuru.

Bw. Hassan alisema wengine ni Bw. Abdallah Kichwabuta ambaye ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi la Uhuru, Bw. Goodselda Rwitana ambaye ni Katibu wa Tawi la Uhuru na Bi. Fatma Ahmad ambaye ni Katibu wa UWT Tawi la Uhuru.

Alisema kuwa wanachama hao, mnamo Novemba 1, mwaka huu walikutwa kwa aliyeshinda kiti cha udiwani katika kata hiyo kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Ibrahim Mabruk wakishangilia ushindi alioupata katika uchaguzi huo.

Katika kikao hicho, wajumbe wameomba ngazi ya CCM wilaya ya Bukoba kumchukulia hatua Bi. Murungi Badru Kichwabuta, ambaye ni mwenyekiti wa UWT wilayani humo, kwa madai ya kushiriki kukihujumu chama wakati wa uchaguzi mkuu.

Wakati wa kampeni za chama hicho, Bi. Kichwabuta alikuwa miongoni mwa wanachama watano waliosimamishwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mjini kushiriki kampeni za chama hicho tangu Oktoba 20 kwa madai ya kukihujumu chama.

Pia wajumbe hao wamewaonya wajumbe wa kamati ya siasa ya kata hiyo, kuacha kutoa siri za vikao nje.

source >>here
 

October

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
2,145
91
Wanaanza kutafutana Uchawi ndani ya chama!!!
Na Bado, Watiana vidole machoni muda si mrefu...:smile-big:
 

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
Patamu hapo..... tumeanza sikia Arusha, mara Karatu, mara Songea, mara Bukoba na tutasikia zaidi ila hiyo ngoma ya watoto haikeshi, ngoma yenyewe ya wakubwa 2015 lazima ikeshe na watanyang'anyana kadi hadi makao makuu na huenda wakwanza akawa JK na Makamba maana ndio wameua chama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom