WANNE WAFA Wakichoma Bomu Wakifikiri Kiazi!!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Jamani! Masikini.....

Habari ifuatayo inasikitisha; wanne wafa wakioka bomu la kurusha kwa mkono wakifikiri ni kiazi.

Bomu laua wanne wa familia moja

Meddy Mulisa, Bukoba
HabariLeo; Wednesday,October 17, 2007 @00:06

WATU wanne wote wa familia moja wamefariki dunia baada ya kulipuliwa na bomu la kutupwa kwa mkono.

Bomu hilo liliokotwa porini na mtoto wa miaka 10 aliyelipeleka nyumbani, ambako inadaiwa alilichoma kwenye moto akidhania ni kiazi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Adihaki Rashid aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mtoto huyo, Chacha Juma (10) alikuwa akichunga mbuzi porini ambako aliokota bomu hilo.

Alisema mtoto huyo alilipeleka bomu hilo nyumbani kwao juzi akidhani ni kiazi kitamu na akaliweka kwenye moto huku wadogo zake wawili na mama yake wa kambo wakiangalia.

Baada ya muda mfupi, bomu hilo lililipuka na kuwaua wote, alisema.

Aliwataja waliokufa kuwa ni Mbusilo Issa (27), Juma (10), Jane Issa (10) na Peter Issa (4), wote wakazi wa Kijiji cha Mabare, Kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo.

Adihaki alisema mwanamke mwingine, Mungushi Nyamhare (60) ambaye alikuwa akipita kando ya nyumba hiyo wakati bomu hilo lilipolipuka saa 11:00 jioni, alijeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya Biharamulo na hali yake ni mbaya.

Alisema Polisi inachunguza chanzo cha bomu hilo.


Wakati huo huo, mkazi wa mjini Bukoba, Hamis Juma (32) amejinyonga kwa kutumia kipande cha shuka akiwa kwenye nyumba ya wageni ya Ombamungu.

Adihaki alisema Juma aliondoka nyumbani kwake mwishoni mwa wiki na akapanga chumba kwenye nyumba hiyo ya wageni, kabla ya juzi kuamua kujinyonga.

Kamanda alisema karatasi inayodhaniwa kuwa aliiandika Juma kabla ya kujiua, ilionyesha kuwa alikuwa akidaiwa deni la Sh milioni moja na Benki ya NMB na kwamba alishindwa kurejesha mkopo huo ndipo alipoamua kujinyonga.
Source: HabariLEO.

4 perish roasting hand grenade

Meddy Mulisa Bukoba
Daily News; Wednesday,October 17, 2007 @00:06

FOUR members of the same family roasting a hand grenade mistaken for a sweet potato were blown to pieces when the device exploded as they circled an open cooking fire in Biharamulo District yesterday.

Acting Kagera Regional Police Commander Adihaki Rashid, told reporters that the lethal weapon had been picked earlier from a nearby bush by Chacha Juma (10), who took it home to cook thinking it was a potato. Their house was also severely damaged.

Commander Rashid said the explosion was so intense that the heads of two of the bodies were blown off while the other two were shredded into pieces, with an arm here and a leg there. A 60 year-old woman, Mungushi Nyamhare, who happened to be passing nearby, sustained severe head injuries and was admitted to hospital in serious condition.

Mr Rashid identified the dead as the boy, Chacha Juma (10), Jane Isa (10), Peter Isa (4) and their step mother, Mbusilo Isa (27), all residents of Mabare village in Nyakahura Ward. The village is near a closed camp formerly used by Rwandan refugees.

The identity of the device was confirmed by military personnel from a nearby Tanzania People’s Defence Forces (TPDF) camp, Commander Rashid further said.

This was the second incident this year involving deaths caused by unexploded ordinance in the area. Two people were killed earlier this year when a hand grenade also exploded as curious villagers toyed with it. Police have warned people to handle strange metal objects with caution.

Other deaths traced to unexploded devices left behind by military combatants, also occurred at Lunazi near the border with Uganda. The device was suspected to have been left behind during the Uganda war against Dictator Idd Amin nearly thirty years ago.

Meanwhile, Hamis Juma (27) allegedly hanged himself because he had failed to repay a loan for 1m/- he took from the National Microfinance Bank (NMB), Commander Rashid said quoting a note the man left behind.

Source: Daily News.

SteveD.
 
Back
Top Bottom