"Wanikumbuke kuwa nilikuwa rais niliyewatoa hapa nikawapeleka pale"

inols

JF-Expert Member
Sep 22, 2010
283
95
Ungependa wananchi wakukumbuke kwa yapi?

"Wanikumbuke kuwa nilikuwa rais niliyewatoa hapa nikawapeleka pale"
Kuna msemo mmoja katika vitabu vya dini unaosema kuwa "pasipo maono watu uangamia".
Ni kweli hatuwezi kupingana na uhalisia wa kuwa Mhe J. Mrisho Kikwete ni Rais wa watanzania wote, lakini tungependa sana akiwa anatoa hotuba yake ya kwanza ktk bunge jipya atueleze alitutoa wapi? na ametupeleka wapi? na atazamia kutupeleka wapi? Maelezo haya yasiyo ya blaaah blaaah bali yawe ni maelezo ambayo tutaweza kuya quantify.
 
Unajua hata yeye mwenyewe anaona ni ngumu kuelezea ukweli halisi wa mustakabari wa nchi yetu ukiondoa swala la miundombinu ambalo unaweza ukasema amejenga barabara kadhaa na madaraja na vinginevyo ambavyo vinaonekana kiurahisi.....Sasa tuje kwenye mfumuko wa bei,ukisema umewatoa hapa na kuwapeleka pale,na je kwenye kuporomoka kwa shillingi yetu je?
 
kutoka hapa na kutupeleka pale, je alikua na mtazamo huu?

YearInflation rate (consumer prices)RankPercent ChangeDate of Information20034.80 %73 2002 est.20044.40 %81-8.33 %2003 est.20055.40 %15422.73 %2004 est.20064.30 %126-20.37 %2005 est.20075.90 %14537.21 %2006 est.20087.00 %15818.64 %2007 est.200910.30 %14947.14 %2008 est.201011.60 %19712.62 %2009 est.
source: Tanzania Inflation rate (consumer prices) - Economy
 
Ndugu yangu sasa ulitarajia aseme nini! Ni kweli alitutoa hapa akatupeleka huku hata yeye hawezi kueleza na ndio ukweli, labda baada ya uchaguzi majuzi anaweza kusema ametuleta kwenye chumba cha kukata tamaa na kuanza kuulizana dini NA MAKABILA YETU!
 
yaah Tutamkumbuka, kwa Mengi
katutoa kutoka Mkate 250 mpaka 600
katutoa Mchele 600kg mpaka 1200kg
katutoa..................
 
Sukari 800 hadi 1,5000
katutoa kwenye utanzania - mpaka kwa udini
 
Back
Top Bottom