Wangwe: "Rais angevunja Bunge"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,422
39,670
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bw. Chacha Wangwe amedai kuwa kama angepata nafsi ya kumpa ushauri Rais basi angemshauri Rais "avunje bunge ili sote turudi kwa wananchi na kuwapa wananchi nafasi ya kuchagua upya viongozi wao". Sasa miye najiuliza, hivi Wangwe anafikiri Rais anaweza kukurupuka tu na kuvunja Bunge? Jamani someni Katiba mnajidhalilisha!
 
hawa ndio wapinzani wanaotaka tuwapishe waongoze nchi.

mie nnaamini mbali ya kuwa wananchi wana kiu ya mabadiliko lkn wapinzani bado hawajawa tayari kupewa dhamana kubwa kama hiyo. si suala la kujaribu tukifanya mchezo tutafika walipofika wenzetu kwani wao walikuwa makini zaidi kuliko hawa.

CCM endelea kuweka misingi imara na walee hawa wapinzani alau tuanze kuwafikiria baada ya miaka 20

ila kwa sasa kuchagua machafuko kuwapa urais upinzani
 
Hodi jamani.

Then, kweli ndugu kakurupuka, sijui alikuwa anawaza nini?
 
Hodi jamani.

Then, kweli ndugu kakurupuka, sijui alikuwa anawaza nini?

karibu Lizy.. yaani angalau wewe umepisha hodi... jisikie uko kwenye baraza huru kupita yote duniani ambapo watu wanakesha kumkoma nyani giledi.. (baada ya muda utaelewa ni nini hicho kama hujaelewa bado).

Karibu.
 
hawa ndio wapinzani wanaotaka tuwapishe waongoze nchi.

mie nnaamini mbali ya kuwa wananchi wana kiu ya mabadiliko lkn wapinzani bado hawajawa tayari kupewa dhamana kubwa kama hiyo. si suala la kujaribu tukifanya mchezo tutafika walipofika wenzetu kwani wao walikuwa makini zaidi kuliko hawa.

CCM endelea kuweka misingi imara na walee hawa wapinzani alau tuanze kuwafikiria baada ya miaka 20

ila kwa sasa kuchagua machafuko kuwapa urais upinzani

Mzee mwanakijiji na Mtu wa Pwani:
Jana nilibahatika kumuona huyu bwana akihojiwa na TV za hapa nyumbani,alichokieleza pale akanifanya maumivu ya kufungwa kwa Cameroun yawe mara mbili! Huyu jamaa anasema yeye haoni tatizo la ukubwa wa baraza la mawaziri,kwake tatizo ni utendaji? Hajiulizi utendaji wenye mafanikio unaletwa na nini huyu bwana! Siamini pia kuwapo kwa baraza dogola wizara 10 bali lile la kati 15 .

Ila kilichonifanya ninune ni kutambua huyu ni Makamu wa Mbowe, Mbowe siku ile mbele ya Butiku na Warioba alilalamikia ukubwa wa baraza sasa Makamu anapingana naye !!!! Hiki ni chama gani ambacho hata misimamo midogo kama hii wanasigana sasa kwenye mazito ya kitaifa wataweza hawa? Thubutu yao. Haya wazee wangu tumwache JK akamilishe kazi.

Mwanakiji na Mtu wa Pwani: JK alishasema hana mbia ktk urais wake tumeyaona wazee.
 
Siwezi kumchukulia Wangwe serious baada ya hizi comments.He exists and reason in utopialand.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bw. Chacha Wangwe amedai kuwa kama angepata nafsi ya kumpa ushauri Rais basi angemshauri Rais "avunje bunge ili sote turudi kwa wananchi na kuwapa wananchi nafasi ya kuchagua upya viongozi wao". Sasa miye najiuliza, hivi Wangwe anafikiri Rais anaweza kukurupuka tu na kuvunja Bunge? Jamani someni Katiba mnajidhalilisha!

Nafikiri ni kutafuta UMaarafu kwani naye huyu anapenda kusikika kwenye siasa za bongo mara kwa mara hata kama hana cha kusema. Sasa subiri baada ya baraza jipya kutangazwa atasema nini.
 
msishangae Bw. Mdogo akaingizwa Bungeni.. nasikia mtu mmoja wa Chadema aliombwa na Rais kuingia kwenye baraza.. na siamini kama ni Chacha, na ikiwa yeye basi tuna kazi, ila kama si yeye akawa mtu mwingine (dada) basi kuna mtu kitamuuma kweli..
 
hawa ndio wapinzani wanaotaka tuwapishe waongoze nchi.

wapinzani bado hawajawa tayari kupewa dhamana kubwa kama hiyo. si suala la kujaribu tukifanya mchezo tutafika walipofika wenzetu kwani wao walikuwa makini zaidi kuliko hawa.

ila kwa sasa kuchagua machafuko kuwapa urais upinzani

Nadhani tumeeaca Hoja ya msingi na sasa tumeingia katika mtego wa ushabiki wa vyama.Awapishe waongoze nchi akina nani? kwani katiba ya Tz inasema nchi iataongozwa na nani?

Nasikitika tunapoleta ushabiki wa vyama kama ambvyo wabunge wetu wameacha kueleza namna amabavyo Pinda ataisaidia nchi wamekazana amelelewa na chama. Lakini si hata hao tunaowaondoa walilelewa na chama?
alafu Hoja hizi zilizotumika kuwadanganya watanzania kuwa kuchagua upinzani ni kuchagua machafuko zimepitwa na wakati. Labda mchangaiaji alete Mifano hai na uthibitisho ni vipi itakuwa macahafuko?

Swala la nchi Jirani wote tunaelewa lina elemnt nyingi, ambazo ni ukabila toka enzi za ukoloni, mgawanyo wa njia za uchumi, Ubadhirifu uliokuwa umekithiri toka enzi Kanu.

Nadhani tuwe tunajadili faida na hasara za kuvunja Bunge ili watu wajifunze hapa, wapate mwanga, tupate kuelewa tunaoanza leo siasa.
 
Nakubaliana na wajumbe kuwa Chacha hakuwa makini, katiba inasema ni wakati gani ambapo Rais anaweza kuvunja Bunge. Mathalani kama wabunge wangempigia kura ya No Confidence Bwana Lowassa na Rais akawa na msimamo kuwa haoni shida yoyote kwa lowassa ingefika wakati ambapo either Raisi akajiuzuru au kuvunja bunge au yote mawili. :confused:
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom