Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,604
- 5,581
Kwa masaa machache sana ambayo nimekuwepo hapa, nimegundua ya kwamba, yule wanaesema WANAMPENDA na kumuamini HAWAMPENDI bali wanambomoa na KUMUANGAMIZA. Kwa sababu kama KWELI WANAMPENDA WATAMLINDA. Lakini wao hawako hivyo, Mwanakijiji aliwapa maneno mapana kwa marefu yake, hakuandika kama ambavyo nimekuwa nikiandika mimi. Alifafanua beti kwa beti na aya kwa aya ili hata wale wenzangu mimi ambao uelewa wetu lazima tuulize taarifa tuliyotazama wote waweze kuelewa. Lakini bado. Ni hali ambayo inasababisha kwamba sote wageni humu ndani tuonekane kuwa watuhumiwa, ila ikumbukwe kwamba mara nyingi wahalifu ni WAGENI WENYEJI. hivyo basi ni vema IP addresses zichunguliwe-chunguliwe, ili chanzo cha tuhuma kijulikane. (KWANI MWIZI KWENYE SHAMBA LA KARANGA HUJIFICHA KWA KUJILAZA-AKIDHANI MGONGO HAUONEKANI)
Kwanini nasema hivyo;
MBWA MWENYE KUKUUMA MKONO NI YULE UNAYEMPA CHAKULA.
Kwanini nasema hivyo;
- WENGI WA WATANZANIA HATUUJUI UHURU WETU UNAKOMEA WAPI, KISA UHURU WA KUJIELEZA.
- WENGI WETU HATUJUI MAMLAKA YA SERIKALI YANAANZIA WAPI
- WENGI HATUJUI MACHAFUKO HUANZIA WAPI
- WENGI HATUFAHAMU UJUMBE HUWA UNA ATHARI GANI KWA WANAOUPOKEA
- WENGI NI WAVIVU KUFIKIRI YAJAYO KWA TAMAA YA WANAYOFIKIRI YATAKUWEPO
- WENGI WANADHANI SERIKALI INAWEZA KULETA MAENDELEO BILA BIDII ZAO.
- NINA HAKIKA 85% NI WANAOSOMA KWA MKOPO WA SERIKALI NDIO HAOHAO WACHOCHEZI, SIWACHUKII ILA SHAKA YANGU IKO HAPO.
- TUNACHOJADILI HAPA (KWA MUONO WANGU) NI NINI KIFANYIKE ILI TUWE NA MUSTAKABALI MWEMA KWA TAIFA LETU.
- NI WATU WAJINGA PEKEE WANAOWAZA KUBOMOA BADALA YA KUJENGA, NI WATU WAPUMBAVU PEKEE WANAOSHABIKIA NYUMBA WANAYOISHI IKIVUNJWA, WAKATI HAWATOKUWA NA PENGINE PA KWENDA.
- TUNASOMA ILI TUPATE MAARIFA, HATUSOMI ILI KUWA WENDAWAZIMU.
MBWA MWENYE KUKUUMA MKONO NI YULE UNAYEMPA CHAKULA.