Wangekuwa na speed kama hii kuwashughulikia mafisadi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wangekuwa na speed kama hii kuwashughulikia mafisadi...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 2, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,204
  Trophy Points: 280
  ...basi ufisadi ungetokomezwa Tanzania

  Date::9/2/2008
  Televisheni bandia za Sh500 milioni zateketezwa na serikali Dar
  Na James Magai
  Mwananchi
  TUME ya Ushindani Huru Kibiashara jana iliteketeza bidhaa bandia aina ya runinga zipatazo 2829 zenye thamani ya Sh500 milioni katika dampo la Pugu Kinyamwezi wilayani Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kukanyagwa na katapila.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio Mkurugenzi wa Mambo ya Walaji na Utawala Michael Shilla alisema runinga hizo zilikuwa zimeagizwa na wafanya biashara watatu tofauti kutoka nchini China na kwamba zilikamatwa kwenye bandari ya Dar es Salaam kabla ya kuingizwa sokoni.

  Shilla alisema runinga hizo ziliingizwa nchini na Kampuni ya Shuangao Imports & Export, iliyokuwa na makontena matatu yenye runinga 1950 yote kwa pamoja zikiwa na thamani ya Sh.110 milioni.

  Alisema Kontena moja lenye runinga 650 zenye thamani ya Sh.40 milioni ziliingizwa nchini na Mfanya biashara Frank Sindato Mrisho,wakati runinga 229 zenye thamani ya Sh.12 milioni ziliingizwa nchini na mfanyabiashara Beda Massawe wa jijini Dar es Salaam.

  “Ingawa wamiliki wa mizigo hiyo walidai hiyo ndio thamani ya mizigo hiyo lakini katika thamani ya sokoni bidhaa hizo zina thamani ya Sh.500milioni,”alisema Shilla.

  Alisema baada ya kukamatwa wafanyabiashara wote walikubali kosa na Mkurugenzi wa FCC akawatoza faini ya Sh.5 milioni kwa kila kontena na mujibu wa mamlaka anayopewa na sheria, kulipia Sh.2 milioni kwa kila kontena kama gharama za kuharibu bidhaa hizo.

  Shilla alisema kwa sasa bidhaa bandia za aina mbalimbali zenye thamani ya Sh 1 bilioni zimekwisha kuteketezwa katika kipindi cha amwaka mmoja.

  Alisema hivi sasa FCC imepewa meno ya kisheria baada ya kuifanyia marekebisho sheria ya bidhaa bandia ya Mwaka 1963, ambapo kwa sasa wana uwezo wa kwenda kusaka bidhaa bandia hadi sokoni tofauti na awali walipokuwa na uwezo wa kusaka bidhaa hizo bandarini tu.

  “Hivyo ninawatahadharisha wafanya biashara kwamba kwa sasa tuko makini hivyo tutawashughulikia kikamilifu ili kuhakikisha kuwa nchi yetu haigeuki kuwa dampo la bidhaa bandia,”alisema Shilla.
   
Loading...