Wangapi wamepoteza imani kwa Serikali ya Muungwana....?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,350
29,170
Naanza kwa kujitetea kamba mie sio mwandishi nguli wa aina ya mzee mwanakijiji, ES, Mwafrika mwanamke n.k. I am just an artist and short talk reflecting way of art which i use to communicate to the community....

Tena, as heading above, sio nia yangu kuweka orodha ya depressed citizens hapa, ila just kuwachechemiza wenye machungu yao kuweka hapa ili tuone ni namna gani tumeguswa na matukio ya kifisadi yanayoendelea ndani ya nchi yetu..

Tangu nipigie kura serikali ya muungwana, niliamini kuwa mwarobaini wa matatizo ya mtanzania umepatikana. Nilikuwa naitetea kwa nguvu zote (mishipa ya shingo ikinitoka) serikali hii kuwa tumepata mkombozi. Kumbe nilikuwa brain washed kwa muda mrefu sana tena victim wa muda mrefu. Kuanzia kwenye media ambapo muungwana alikuwa anapata coverages hadi kwenye dini ambapo makasisi walituhakikishia kuwa mteule wa mungu ndiye huyu. Lakini maumivu ya kwanza ya kichwa yalinianza baada ya kutangazwa baraza kuuuubwa la mawaziri ambapo nilihisi kuwa hata wakurugenzi wa wizara watakuwa wameporwa baadhi ya majukumu na baraza hili. Pia nilikuwa napingana na nafsi yangu kuamini kuwa labda Mkapa alijua kitakachokuja Hughe cabinet) hivyo akasave much bucks ili kuhost this era. Mpaka leo nashangaa kuna baadhi ya wizara ambazo zina manaibu wawili ambapo labda hata waziri pekee angeweza shughuli hizo. Na pia mpaka sasa hatujaelezwa hizo added responsibilities zinazopelekea kuwa na baraza kubwa (linalonyonya hazina bila kuzalisha). Kingine kinachousonga mtima wangu ni kuwa pamoja na mkakati ambao pia umo ktk ilani ya uchaguzi ya CCM, ya kupambana na ufisadi na kuongeza tija, sijaona chochote kilichofanyika zaidi ya ngonjera na mipasho mbalimbali. Mfano kilio cha wakulima wa kada mbalimmbali haswa kuhusu upatikanaji wa pembejeo na masoko (hasa bei) imekuwa ni utata. Nimeambiwa kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa letu lakini nadhani nimedanganywa, tuna rasilimali ambazo kwa uchache na wingi wake tungeweza kuongeza tija.

Nadhani wengi mnafahamu lile shairi maarufu la yule baba na wanae ambapo aliwausia wanae kuwa mali watayapata shambani. Nadhani labda vijana wale kwa kutokufikiria mara mbili mmbili walianza kulima shamba right away. nadhani kama wangefikiria zaidi kuhusu ujumbe wa baba yao wangeligundua hazina ya madini iliyopo chini ya shamba lao na wangekuwa mbali zaidi. Nimejaribu kufikiria zaidi kuwa wengi wa vigogo wetu hawako creative ktk utawala wao (sio uongozi). Jaribu kufuatilia kuanzia hotuba zao hadi wanapojibu maswali bungeni wanakuwa hawana jipya. sana sana hawapendi kuambiwa ukweli.

Imani yangu kwa serikali yangu inazidi kupotea hasa kuhusiana na ahadi nyingi zisizotekelezwa. Tuliahidiwa kuwa hakutakuwa na uingiaji wa mikataba mipya ya madini mpaka baadhi ya vipengele vya kanuni kuboreshwa, Tuliahidiwa kuwa tetesi za ufisadi zingemwondolea mhusika sifa ya kuaminiwa tena ila duh! kumbe haikuwa kweli. Pamoja na yooote ahadi ya ufanisi na utendaji hatujaiona mpaka sasa. imefikia mahala kwamba kiongozi akifanya jambo fulani ambalo anapaswa kufanya, tutamsifia kuwa angalau anajali.

Bunge limeporwa haki yake ya kutunga sheria sanasana executives wameweka wizara ambayo ndiyo draftsman yupo huko... Na ole wake mbunge wa chama dume aihoji serikali ya chama bungeni... atashughulikiwa ndani ya chama. pamoja na kuwa nilichukia vyama vingi hapo awali lakini kwa ushawishi w Baba wa Taifa serikali iliridhia viwepo na cha kushangaza baada ya sie kuona faida za vyama tele bado serikali inakumbatia katiba ya zamani ya chama kimoja. Tume ya Nyalali iliona baadhi ya vipengele vya kubadilisha au kuboresha ktk katiba lakini mpaka leo ripoti ile inaozea kabatini.

Lakini naamini haya mambo ya ufisadi yalianzia pale ambapo viongozi walipogeuka kuwa watawala, na pale ambapo watawala hawa wakayapiga teke maadili na miiko ya uongozi. Kwa mfano, wengi wa watawala ni mabepari na wakati huohuo wanaitumikia nchi. Kama mtu anataka kuwa mtawala au kuongozi anapaswa kuikana nafsi yake kwanza na kukubali kuubeba msalaba wa taifa kuelekea kilimani. mabepari hawa wanahonga ili kupata kura, mabepari hawa hawajali wala kusikia kilio cha umma kuhusu masuala ya kimsingi kama vile nishati na miundombinu. mabepari hawa hawa wana hisa ktk makampuni makubwa yanayoinyonya nchi. walah nasema kuwa am soooo depressed.

Muungwana isafishe nyumba yako au la sivyo viroboto, papasi na mchwa wataendelea wataitafuna na kuiaibisha zaidi. Na ujue kuwa mchwa hatishiwi kwa maneno au maonyo, dawa ya mchwa ni kumwondoa...
 
..swali la kisanii kweli kweli!

..ila,watu hawaongei vizuri!sasa kama huko ndo kupoteza imani mi sijui!

..unajua,waswahili tushazoe kusemana vibaya,lakini kesho utatukuta tumekaa pamoja tunacheza bao!

..na usilogwe ukafikiri tumesalitiana...utashangaa na roho yako!
 
Kheee....nyi vipi...ndo mnaamka leo?
Mwenzenu sikuwa na imani naye hata kabla hajateuliwa kugombea...
Kwa sababu sikuona quality zozote alizokuwa nazo ambazo zinafaa mgombea uraisi awe nazo.
Ila kama kweli yeye ndo alikuwa chaguo pekee na hakuna mwingine alikuwa anastahili zaidi yake basi tuko doomed. Oh well.....
 
Nyani Ngabu
nadhani pia tatizo lingine ni kuwa mpaka sasa uwaziri ndicho kigezo cha uzoefu wa kuteuliwa kuwa mgombea uraisi, wengine ni wasindikizaji. kwani hakuna mtanzania au watanzania wanaoweza bila kuwa mawaziri??
 
Hata mi nshajiuliza hilo....
 
Nyani Ngabu
nadhani pia tatizo lingine ni kuwa mpaka sasa uwaziri ndicho kigezo cha uzoefu wa kuteuliwa kuwa mgombea uraisi, wengine ni wasindikizaji. kwani hakuna mtanzania au watanzania wanaoweza bila kuwa mawaziri??

Tena wawili walikuwa wizara inayonuka kwa ufujaji wa pesa, na balozi moja anakesi na mwingine kule Malawi au Zambia wakamsamehe kinyemela. Tuondoe hii taboo tupate mwingine ambaye hajawahi kuwa waziri hasa wa mambo ya nje.
 
Dua hapo umenena
pia tukumbuke kuwa wapo mafisi wa madaraka wamekaa madarakani mda mrefu wakisubiri huruma ya kuteuliwa. nadhani iwe mkakati wa kumsaka rais asiye na uzoefu wa ufisadi.
 
Mimi huyu Jakaya ananikatisha sana tamaa ninapomlinganisha na Mkapa. Ni kweli inaelekea Mkapa amekuwa na possession mania kiasi, lakini alijenga sana uchumi. Naomba nionyeshe kukatishwa tamaa kwangu na Muungwana kwa kulinganisha utendaji wa serikali yake na wa ile ya Mkapa, kama ifuatavyo:

1. Benjamin William Mkapa alipokea nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 30%. Hiyo ilikuwa 1995. Mfumuko wa bei wa juu ni kitu hatari sana kwa uchumi na usalama wa taifa. Mkapa alipambana nao kwa dhati, na wakati anang'atuka mwaka 2005, alishaushusha hadi 4.5%.

Jakaya Mrisho Kikwete akaanza na nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 4.5% mwanzoni mwa 2006. Miaka miwili tu baadaye, sasa tuna kasi ya mfumuko wa bei ya 10% (zaidi ya mara mbili ya ule alioridhi!). Hii takwimu imetolewa na IMF kwenye magazeti ya Tanzania ya wiki hii. Kama Jakaya ameweza kuongeza kasi ya mfumuko wa bei mara dufu kwa kipindi cha miaka miwili, itakuwaje akikaa miaka mitano? Naona tutarudi kule kwenye kasi ya mfumko wa bei ya 30% kabla hajamaliza miaka mitano madarakani.

2. Mwaka 1995, Mkapa alipokea uchumi uliokuwa unakua kwa kasi ya 3% kwa mwaka. Akaufanyia kazi, na wakati anatoka madarakani, alishaongeza kasi ya kukua kwa uchumi hadi 7.0% . Muungwana amerithi hiyo 7.0% na sasa ameshaishusha hadi 5%. Na bado anazidi kuharibu macroecononic stability ya nchi yetu. Inatisha sana!

3. Mkapa alipokea Hazina yenye fedha za kigeni kiasi cha US$267 million. Inaonekana ni kidogo lakini tunamshukuru Mzee mwinyi kwani yeye alirithi Hazina yenye US$0.0 million! Mkapa aliingia kazini kwa nguvu, na wakati anatoka mwaka 2005, Hazina ilikuwa na fedha za kigeni kiasi cha US$2,300 million. Hiyo ni mara tisa ya fedha alizokuta. Kikwete amerithi hizo fedha, na akaanzisha kitu anaita program yake ambacho kimezibugia haraka haraka, na sasa ziko chini ya US$2,000 million. Na anaendelea kuzidi kuzibugia mbiyo hivyo hivyo!

4. Mkapa ni mtu wa maneno machache, vitendo vingi. Kikwete ni maneno mengi, vitendo hakuna kabisa. Kuna miradi mingi ya maji mikoani aliyoanzisha Mkapa na kumwachia Kikwete amalizie. Badala yake, ameinyima fedha, na wabunge wamelalamika hovyo kwamba karibu miradi yote ya maji inakufa. Mabarabara ni hadithi hiyo hiyo!

We are in serious trouble!
 
Mheshimiwa augustine
naona uko deeeply depressed na data zako zimetisha hata mie. Nadhani kuna kosa limefanyika mahala ambapo labda tunaweza kurekebisha au tukawa too late.

Hivi unajua kuwa mpaka sasa viongozi wapo ktk fungate la ushindi?? maana hata bungeni utasikia mbunge anaipongeza serikali kwa kuchaguliwa kwa kishindo.

Kali ya yote ni kwammba naogopa kukopa zile bilion zake maana sijui zinatoka ktk bajeti ipi kwani nisije nikawa nashiriki ufisadi. Watu hatutaki fedha tnahitaji fursa na maboresho ya miundombinu ili tukuze uchumi.

Wataalam leteni data hapa...
 
Mimi huyu Jakaya ananikatisha sana tamaa ninapomlinganisha na Mkapa. Ni kweli inaelekea Mkapa amekuwa na possession mania kiasi, lakini alijenga sana uchumi. Naomba nionyeshe kukatishwa tamaa kwangu na Muungwana kwa kulinganisha utendaji wa serikali yake na wa ile ya Mkapa, kama ifuatavyo:

1. Benjamin William Mkapa alipokea nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 30%. Hiyo ilikuwa 1995. Mfumuko wa bei wa juu ni kitu hatari sana kwa uchumi na usalama wa taifa. Mkapa alipambana nao kwa dhati, na wakati anang’atuka mwaka 2005, alishaushusha hadi 4.5%.

Jakaya Mrisho Kikwete akaanza na nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 4.5% mwanzoni mwa 2006. Miaka miwili tu baadaye, sasa tuna kasi ya mfumuko wa bei ya 10% (zaidi ya mara mbili ya ule alioridhi!). Hii takwimu imetolewa na IMF kwenye magazeti ya Tanzania ya wiki hii. Kama Jakaya ameweza kuongeza kasi ya mfumuko wa bei mara dufu kwa kipindi cha miaka miwili, itakuwaje akikaa miaka mitano? Naona tutarudi kule kwenye kasi ya mfumko wa bei ya 30% kabla hajamaliza miaka mitano madarakani.

2. Mwaka 1995, Mkapa alipokea uchumi uliokuwa unakua kwa kasi ya 3% kwa mwaka. Akaufanyia kazi, na wakati anatoka madarakani, alishaongeza kasi ya kukua kwa uchumi hadi 7.0% . Muungwana amerithi hiyo 7.0% na sasa ameshaishusha hadi 5%. Na bado anazidi kuharibu macroecononic stability ya nchi yetu. Inatisha sana!

3. Mkapa alipokea Hazina yenye fedha za kigeni kiasi cha US$267 million. Inaonekana ni kidogo lakini tunamshukuru Mzee mwinyi kwani yeye alirithi Hazina yenye US$0.0 million! Mkapa aliingia kazini kwa nguvu, na wakati anatoka mwaka 2005, Hazina ilikuwa na fedha za kigeni kiasi cha US$2,300 million. Hiyo ni mara tisa ya fedha alizokuta. Kikwete amerithi hizo fedha, na akaanzisha kitu anaita program yake ambacho kimezibugia haraka haraka, na sasa ziko chini ya US$2,000 million. Na anaendelea kuzidi kuzibugia mbiyo hivyo hivyo!

4. Mkapa ni mtu wa maneno machache, vitendo vingi. Kikwete ni maneno mengi, vitendo hakuna kabisa. Kuna miradi mingi ya maji mikoani aliyoanzisha Mkapa na kumwachia Kikwete amalizie. Badala yake, ameinyima fedha, na wabunge wamelalamika hovyo kwamba karibu miradi yote ya maji inakufa. Mabarabara ni hadithi hiyo hiyo!

We are in serious trouble!

MWALIMU MOSHI SAFI SANA!!!ungekuwa karibu ningekupa kikombe... SIKATAI MKAPA SI MALAIKA ..lakini naaza kuamini kuna juhudi za makusudi za kutaka kufunika yoote mazuri aliyofanya....na wanaofunika hawafanyi lolote.....

njia pekee ya kumfunika mtu ni kufanya zaidi yake kwa vitendo..kama mwinyi alimfunika mwalimu ni haki mkapa amemfunika mwinyi na jk TUNAMTEGEMEA amfunike mkapa na si vinginevyo..hakuna kurudi nyuma..mtuelewe jamani!!!! kama nyerere alirithi madaktari 5., maengeer 2..na mchumi mmoja au wawili..leo kikwete anao wataalam ambao hata ajira hawana na nchi ina umoja...na amani ..tunataka kwenda mbele..si maneno,,,
 
BIG UP MOSHI
Nina wasiwasi urais wa JK umeanza kuwa unafanana na wa mzee Mwinyi. Kibaya zaidi waandishi wa habari hapa home ni kama karibu wote wamehongwa, sio siri uchumi Tanzania kwa sasa unakwenda ovyo, alisema Moshi hayapingiki kwa mtanzania mwenye elimu na anayejua mambo, atakayebisha ni yule ambaye hajui analosema. Lakini ajabu waandishi wa habari karibu wote(except wa THIS DAY) kazi yao ni kuwapongeza JK na Lowassa kila kukicha, na wahariri wengine ambao ndio waliotakiwa kuwa mstari wa mbele kuyasema haya, wanaanza kuwatetea kina Karamagi na kuwapiga madongo Kabwe na Slaa, lakini really issues zinazo matter kwa maendeleo ya nchi yetu wameweka kando.
Leo ukiuliza kwa mtanzania yoyote mwenye akili JK amefanya nini, jibu litakuwa ni hakuna cha maana alichofanya. Mimi binafsi kama angeweza kudhibiti mfumuko wa bei kwen ye asilimia 4.5 ningeona kuwa amefanya la maana, lakini hata hilo JK ameshindwa. Nadhani we are heading to a disaster kama ya Mwinyi. Tusubiri mungu tu atuokoe.
Nina hakika hata 2010 haya mambo kwa watanzania hayatakuwa issues za uchaguzi(si unajua tena aleimu ya watanzania wengi) unaweza kushangaa kuwa JK anapita tena. Really Sad.
 
Mimi huyu Jakaya ananikatisha sana tamaa ninapomlinganisha na Mkapa. Ni kweli inaelekea Mkapa amekuwa na possession mania kiasi, lakini alijenga sana uchumi. Naomba nionyeshe kukatishwa tamaa kwangu na Muungwana kwa kulinganisha utendaji wa serikali yake na wa ile ya Mkapa, kama ifuatavyo:

1. Benjamin William Mkapa alipokea nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 30%. Hiyo ilikuwa 1995. Mfumuko wa bei wa juu ni kitu hatari sana kwa uchumi na usalama wa taifa. Mkapa alipambana nao kwa dhati, na wakati anang'atuka mwaka 2005, alishaushusha hadi 4.5%.

Jakaya Mrisho Kikwete akaanza na nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 4.5% mwanzoni mwa 2006. Miaka miwili tu baadaye, sasa tuna kasi ya mfumuko wa bei ya 10% (zaidi ya mara mbili ya ule alioridhi!). Hii takwimu imetolewa na IMF kwenye magazeti ya Tanzania ya wiki hii. Kama Jakaya ameweza kuongeza kasi ya mfumuko wa bei mara dufu kwa kipindi cha miaka miwili, itakuwaje akikaa miaka mitano? Naona tutarudi kule kwenye kasi ya mfumko wa bei ya 30% kabla hajamaliza miaka mitano madarakani.

2. Mwaka 1995, Mkapa alipokea uchumi uliokuwa unakua kwa kasi ya 3% kwa mwaka. Akaufanyia kazi, na wakati anatoka madarakani, alishaongeza kasi ya kukua kwa uchumi hadi 7.0% . Muungwana amerithi hiyo 7.0% na sasa ameshaishusha hadi 5%. Na bado anazidi kuharibu macroecononic stability ya nchi yetu. Inatisha sana!

3. Mkapa alipokea Hazina yenye fedha za kigeni kiasi cha US$267 million. Inaonekana ni kidogo lakini tunamshukuru Mzee mwinyi kwani yeye alirithi Hazina yenye US$0.0 million! Mkapa aliingia kazini kwa nguvu, na wakati anatoka mwaka 2005, Hazina ilikuwa na fedha za kigeni kiasi cha US$2,300 million. Hiyo ni mara tisa ya fedha alizokuta. Kikwete amerithi hizo fedha, na akaanzisha kitu anaita program yake ambacho kimezibugia haraka haraka, na sasa ziko chini ya US$2,000 million. Na anaendelea kuzidi kuzibugia mbiyo hivyo hivyo!

4. Mkapa ni mtu wa maneno machache, vitendo vingi. Kikwete ni maneno mengi, vitendo hakuna kabisa. Kuna miradi mingi ya maji mikoani aliyoanzisha Mkapa na kumwachia Kikwete amalizie. Badala yake, ameinyima fedha, na wabunge wamelalamika hovyo kwamba karibu miradi yote ya maji inakufa. Mabarabara ni hadithi hiyo hiyo!

We are in serious trouble!

Hmmm! Mkapa ndiye huyu huyu aliyeleta Net Group Problems ili waindeshe TANESCO na pamoja na kulipwa mishahara mikubwa na management fees za hali ya juu kazi ikawashinda! Ndiye Mkapa huyu huyu aliyeng'ang'ania kununua rada pamoja na uamuzi huo kupingwa na idadi kubwa ya Watanzania. Rada ambayo ikaja kugundulika kwamba wakala wa huo ununuzi alilipwa $12 million? Ndiye huyu huyu aliyesimamia uuzwaji wa nyumba za sirikali kiholela kwa mawaziri? Ndiye huyu huyu aliyejipatia Kiwira Coal Mining katika mazingira ya kutatanisha? Ndiye huyu huyu aliyesaini mikataba ya uchimbaji wa madini ambayo hadi hii leo bado imefanywa siri? Ndiye huyu huyu anayesemekana alihusika katika mikataba ya ununuzi wa ndege ya Rais, helicopter na magari ya jeshi? Ndiye huyu huyu aliyekuwa busy akifanya biashara akiwa Ikulu?

Uchumi wa nchi unapokuwa ajira na kipato cha wananchi huwa kinaongezeka na wananchi wanaona tofauti kubwa katika hali halisi ya maisha yao. Hili halikutokea wakati wa Mkapa. Ni ukweli kwamba wakati wa awamu yake makusanyo ya kodi yaliongezeka kwa kiasi kikubwa sana, lakini Watanzania hawakuona mafanikio yoyote ya maongezeko ya makusanyo hayo. Mishahara bado ilikuwa hailingani na gharama halisi za maisha ya kila siku. Hospitali zetu bado zilikuwa hazina dawa, hazina vifaa muhimu na wagonjwa hata akina mama wajawazito ama walikuwa wanalala chini au kulalia kitanda kimoja wagonjwa wawili na kuendelea. Mashule ya msingi mengi yalikuwa katika hali ya kusikitisha ama wanafunzi walikaa chini kwa kukosa madawati na viti, kusomea chini ya miti kwa ukosefu wa madarasa na shule nyingi zilikuwa hazina vyoo. Hivyo pamoja na ongezeko hilo la ukusanyaji wa kodi, waliofaidika ni wachache sana.

Kwa kifupi pamoja na IMF na WB kumsifia Mkapa na kudai kuwa uchumi wa Tanzania ulikuwa unakuwa kwa asilimia 5 au zaidi, Watanzania wengi hawakuona ahueni yoyote katika maisha yao ya kila siku. Mkapa alikuwa busy kujilimbikizia mali yeye pamoja na familia yake, badala ya kutafuta namna ya kuboresha maisha ya Watanzania.
 
Hmmm! Mkapa ndiye huyu huyu aliyeleta Net Group Problems ili waindeshe TANESCO na pamoja na kulipwa mishahara mikubwa na management fees za hali ya juu kazi ikawashinda!

Nadhani nimesema Mkapa ameonyesha kuwa na possesion mania. Nasema alijenga uchumi; sisemi hakuwa corrupt.

Uchumi wa nchi unapokuwa ajira na kipato cha wananchi huwa kinaongezeka na wananchi wanaona tofauti kubwa katika hali halisi ya maisha yao. Hili halikutokea wakati wa Mkapa

Si sahihi. Hali ya uchumi wa wananchi ilionyesha kuboreka wakati wa Mkapa. Takwimu za kitafiti zilionyesha kukua kwa ajira na hali ya maisha ya wananchi kwa ujumla.

Ni ukweli kwamba wakati wa awamu yake makusanyo ya kodi yaliongezeka kwa kiasi kikubwa sana, lakini Watanzania hawakuona mafanikio yoyote ya maongezeko ya makusanyo hayo.

Hospitali karibu zote, kama sio zote kabisa za Wilaya, zilikarabatiwa. Mitambo ya X-ray ilifufuliwa kila mahali. Muhimbili ilifanyiwa ukarabati wa nguvu. Ofisi za serikali ambazo zilikuwa zimekuwa kama magofu wakati wa Mwinyi zilifufuliwa. Mishahara ya wafanyakazi serikalini ilipandishwa sana. Yalifanywa mapinduzi makubwa ya elimu, etc. Haya yote umepuuza? It is not fair. Give credit where credit is due.

Chini ya uongozi wa Mkapa, Tanzania ilipanda chati kiuchumi na kuwa na uchumi uliokuwa unaendelea kwa kasi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote ya Afrika Mashariki. Tulikuwa tunakimbia wakati wakitembea. Sasa JK ameturudisha kuwa tena wa mwisho.
 
Augustine Moshi,

Ndiugu yangu jaribu kumtazama JK kama JK bila kumweka Mkapa hapa maanake mtu kama mimi huwezi kabisa kunipa somo la Mkapa nikasimama hapa na kukubaliana nawe!..
Hata siku moja hatuwezi kuutazama mfumko wa bei nchini kwa darubini ya kawaida hasa ktk nchi ambayo Mkapa aliipokea dollar ikiwa Tsh 500 na kumaliza ikiwa Tsh 1100 na wananchi wakipokea mshahara kwa ongezeko lislozidi asilimia 5 kwa miaka 5 na nchi yetu kutegemea mikopo zaidi ya wakati wowote ule!
Yaani tuyaache tu haya maanake zijui ni mzani gani unaweza kupima ukweli wa hali ya uchumi wa Tanzania ikiwa Nchi inaweza kusifika kwa kuuza billioni 10 lakini kati ya pato hilo 50% (nusu) huenda ktk mifuko ya Watawala wachache!..
JK amefuata nyayo za Mkapa na itakuwa aibu kusifia Mtume hali Khalifa anafundisha kile alichoachiwa!
 
Mkandara
Nadhani hapa kinachosemwa ni kuwa Mkapa hakuwa msafi kwa asilimia 100. Unajua ukiwa na kitama cheupe chenye doa jeusi hilo doa ndio linaweza kuonekana sana kuliko huo weupe wote. Na huyo ndio Mkapa. Can you tell me kipi kinamnufaisha zaidi mwananchi wa kawaida wa Tanzania zaidi ya kudhibiti mfumuko wa bei kwa chini kabisa? Hapo lazima tumsifu Mkapa, lakini kwa hayo aliyosema Moshi mimi namuunga mguu kwa asilimia 101.
 
Hali ya uchumi wa wananchi ilionyesha kuboreka wakati wa Mkapa. Takwimu za kitafiti zilionyesha kukua kwa ajira na hali ya maisha ya wananchi kwa ujumla
Hapa kuna kiziwi na kipofu alitangulia kipofu na akamchagua kiziwi,kumrithi kuendelea kuongoza Taifa.Msingi Mama wa yanayojiri leo ndani ya Nchi YETU ni Huyo Mheshimiwa anayesifiwa hapa kwani alishiriki kuangamiza uchumi kwa kuvikwa kilemba cha ukoka na wahisani,Lakini hali halisi kwa walalahoi walibakia kuwa hivyo na kwa kundi la walichonacho ndiyo lilizidi kuwa nacho.Ajira zote wakati wa Mkapa silisitishwa serikalini isipokuwa madaktari tu ,NA ANAPOTAKIWA KUAJIRIWA MTU WA FANI NYINGINE MPAKA KIBALI KITOKE SERIKALI KUU na walijenga mwanya wa rushwa kwani vingi vilikuwa vinatoka kwa kundi lile la wanaojulikana la wenye navyo.

Hospitali karibu zote, kama sio zote kabisa za Wilaya, zilikarabatiwa. Mitambo ya X-ray ilifufuliwa kila mahali. Muhimbili ilifanyiwa ukarabati wa nguvu. Ofisi za serikali ambazo zilikuwa zimekuwa kama magofu wakati wa Mwinyi zilifufuliwa. Mishahara ya wafanyakazi serikalini ilipandishwa sana. Yalifanywa mapinduzi makubwa ya elimu, etc. Haya yote umepuuza? It is not fair. Give credit where credit is due.
Hospitali nyingi zilibaki kuwa hazina vitendea kazi vikiwemo ulivyovitaja na si za mikoani na wilayani tu hata Hospitali Kuu ya Taifa,Malipo Duni kwa wafanyakazi na mazingira magumu ya kiutendaji kwa watumishi wa afya.Ukarabati wa Hospitali ya Taifa ulianza wakati wa Mkapa hadi hii leo karibu mwaka wa tano haujakamilika na fedha ilitolewa na Benki Ya maendeleo ya Afrika na ukarabati haujakamilika na bado inakosa vitendea kazi muhimu kwa sehemu zilizokamilika.
Zilizokuwa Hospitali Kuu za Rufaa zenye kuwasaidia watu kwa kikanda kama KCMC Kanda ya kaskazini na Bugando Kanda ya ziwa aliwapa RC na Lutheran chini ya mgongo wa kwamba anawarudishia makanisa kwani ndiyo waliokuwa wakizimiliki kabla ya Uhuru, bila ya kuzingatia kwamba serikali bado inachangia uendeshwaji wa hospitali hizo na serikali iliwekeza fedha nyingi kuziendeleza hospitali hizo na kufikia hapo zilipofikia.Kwanini asingeendelea na ubia badala ya kuzirudisha na kusababisha gharama za matibabu kwa wagonjwa kwenye hospitali hizo kuzidi maradufu na wakati huo huo bado serikali inatoa Fungu la uwendeshaji wa hospitali hizo.
Tofauti ya wawili hawa ni kwamba Mkapa aliweza kupunguza idadi ya mafisadi kwa kuwa na kundi dogo la mafisadi ambalo aliweza kuwadhibiti mafisadi wadogo na kundi la kati Lakini Mrithi wake amekuwa na kundi kubwa ambalo hawezi kulidhibiti na lina mafisadi wa kila aina.
Chini ya uongozi wa Mkapa, Tanzania ilipanda chati kiuchumi na kuwa na uchumi uliokuwa unaendelea kwa kasi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote ya Afrika Mashariki. Tulikuwa tunakimbia wakati wakitembea. Sasa JK ameturudisha kuwa tena wa mwisho.
Ukiliwanganisha wawili hawa ni kweli mmoja ni bora kuliko mwenzake Lakini wote si bora kwa mwananchi wa kawaida na Taifa Letu kwa ujumla kwani msingi Mama ya tunayofanyiwa leo Mkapa ndiye mjenzi Mkuu.!
 
watanzania huchoshwa na serikali mapema sana, ila wanakumbukumbu kama ya kuku.
ikifika siku za kampeni, wakimsikia john komba na gari lake tu weshasahau kuchoshwa kwao.
 
Bongolander,
Nadhani hili somo la mfumko wa bei ni kubwa kuliko tunavyojaribu kulipamba. Na kibaya zaidi ni kwamba bado tunatumia cookbooks ambazo zimetengenezwa na serikali ili kuridhisha Umma...
katika Utawala wa Mkapa hapakuwa na doa ila kulikuwa na uchafu mkubwa ktk uchumi kama vile tunavyovaa mitumba. Ubora wa mitumba ni kwamba angalau tuna setiri uchi zetu lakini huwezi kunambia ama kuweka matumizi ya mitumba kuwa ni maendeleo wakati kabla ya mitumba watu hawakutembea uchi ila nguo zilikuwa adimu.

Mimi na wewe sote tumeishi ktk Utawala wa Mkapa na kwamwe tusitake kujidanganya kwamba kulikuwa na Nafuu ktk mfumko wa bei hali sote tunafahamu kwamba Mshahara wa mwananchi ulibaki palepale wakati thamani ya fedha yetu iliporomoka vibaya sana!..Sielewi kama wataalam wetu walichukua price level zipi kupima vitu hivi ikiwa kila mwaka kila mwaka shilingi yetu iliporomoka zaidi ya asilimia 10!
Ni sawa na lugha wanayotumia ktk mapato wakisema mwaka 2000 tuliweka kukusanya kodi za billioni 2 na mwaka 2005 billioni 3 kwa hiyo kulikuwa na ongezeko la asilimia blaaa blaa blaa hali kati ya mwaka 2000 na 2005 fedha yetu imeshuka kwa aslimia zaidi ya 50.
Usanii na Ufisadi wa JK haukuanza jana ila umeanza toka wakati wa Mkapa hasa kipindi chake cha pili. Kumbuka bomu lile la 2002 ktk mauzo ya Tanzanite duniani! ni Billioni ngapi zilipigwa mtama!...
Maisha ya wananchi yamezidi kuwa mabaya sana ktk kila mwaka tangu Mkapa alipoingia madarakani na kwa mara ya kwanza ktk historia ya Tanzania watu walikufa njaa. Uwezo wa wananchi kununua mali za nje ulikuwa mdogo sana hadi ilifkia wananchi kulishwa chakula ambacho kilikwisha kuwa expired.. this is a fact ambayo tunajaribu kuiwekea pazia.
Ni kujidanganya sisi wenyewe ikiwa tutakubali kwamba wakati Mwinyi akiwa madarakani tulisimama ktk asilimia 30 (1995) ya mfumko wa bei wakati hakuna data zozote zinazoonyesha jinsi gani mahesabu hayo yalifanyika ili kupata pungufu la mfumko huo kufikia 4.5 ktk mwaka 2005. Nipe bei za vitu ambavyo vilitumiwa ktk mahesabu hayo!
Ukweli ni kwamba kila kitu tunachokifahamu sisi wananchi kilipanda bei kwa zaidi ya mara mbili isipokuwa tu thamani ya ongezeko hilo ktk dollar lilionekana kuwa ni ndogo na pengine ndio wanachojaribu kutuburuza na data za namna hii.
Wananchi wanatumia fedha za madafu na kama kuna mahesabu yoyote yanayotumika ni bora zaidi ikiwa tutazingatia pia thamani ya fedha yetu na sio kupiga mahesabu kwa kutazama thamani ya dollar!
 
Mkandara
wakati wa utawala wa Mwinyi ni wajinga waliokuwa wanafurahia yaliyokuwa yanatokea, kwamba hela nje nje lakini thamani yake ilikuwa ikiporomoka kila leo. Bei za vituzilikuwa zinapanda kila kukicha na watu hawakujali kwa sababu kulikuwa na flow kubwa sana ya pesa. Thamani ya shilingi iliporomoka sana toka Mwinyi alipochukua nchi kutoka kwa Julius, mwelekeo huo uliendelea Mpaka alivyoingia madarakani Ben. Baada ya Ben kuingia na VAT na policies nyingine za udhibiti wa matumzi ya serikali na ukusanyaji wa mapato, thamani ya shilingi haikuongezeka ila ilikuwa stable na inflation haikuwa kubwa, ukiangalia jinsi bei ya bidhaa ilivyokuwa imetulia unaweza kuona wazi kuwa mfumuko wa bei ulikuwa umedhibitiwa sana, bei zilikuwa zinaongezeka kidogo sana, tofauti sana na sasa. Sasa hivi mfumuko wa bei uko wazi kabisa, ukiangalia bei za vitu unaweza kufeel kabisa ongezeko la bei.
Ukitaka nenda dukani leo nunua kitu weka kumbukumbu ya bei halafu nenda baada ya minezi sita uangalie kama bei itakuwa palepale au vipi. Hapo utaenlewa nini ninachosema.
Kwa ufupi naomba nitofautiane na wewe. Miaka miwili ya JK imeonesha kuwa Mkapa was far far better than JK kwa almost kila kitu. NI wazi kuwa kwenye second term Ben kuna mambo Ben alivuruga, lakini ukumbuke ni second term, lakini JK amevurunda kwa miaka miwili tu toka yuko madarakani na sasa hakuna hata dalili ya kurekebisha mambo. Sanasana naona ni kuwa ataacha legacy mbaya.
 
mwalimu mosha safi sana,
umenikumbusha habari za mzee mmoja,aliyeniambia bei za kupanga nyumba kwa sasa zimepanda tofauti na zamani,kwa mfano maeneo ya sinza nyumba ulikyokuwa unapanga kwa 150000 sasa ni 250000,sababu ya hii ni mfumuko wa bei umeongezeka mara mbili.

hivi ni nani wa kulaumiwa,Je ni watendaji wa serikali au Muungwana amejichukulia Maaamuzi yote na watendaji wamemdhilia nchi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom