Wangapi wamepoteza imani kwa Serikali ya Muungwana....?

Naam msanii ninapochoka zaidi JK ni mchumi by professional ingawa ni Political economy lakini nchi inayumba,hakuna discipline kama ulimwengu wa kambale yaani ata anayezaliwa leo ana ndevu.
Inflation imemshinda,economic growth ndo ivo na hata reserve ya nchi anaitafuna.Mind you ata nusu ya ngwe yake ya 5 years hatujaimaliza mambo yako ivo sijui uko Mbelle.
Jana nimeletewa barua nichangie elfu 20,000 za ujenzi wa shule ya kata.
Mbaya zaidi walizochangishwa wenzangu may mwaka huu zimeishia kujenga msingi tuu.
Maisha yanazidi kuwa magumu siku adi siku katika nchi yenye utajiri mkubwa wa maliasiri.
Nani atainuka kuwatetea watanzania wa leo?
 
Mimi huyu Jakaya ananikatisha sana tamaa ninapomlinganisha na Mkapa. Ni kweli inaelekea Mkapa amekuwa na possession mania kiasi, lakini alijenga sana uchumi. Naomba nionyeshe kukatishwa tamaa kwangu na Muungwana kwa kulinganisha utendaji wa serikali yake na wa ile ya Mkapa, kama ifuatavyo:

1. Benjamin William Mkapa alipokea nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 30%. Hiyo ilikuwa 1995. Mfumuko wa bei wa juu ni kitu hatari sana kwa uchumi na usalama wa taifa. Mkapa alipambana nao kwa dhati, na wakati anang’atuka mwaka 2005, alishaushusha hadi 4.5%.

Jakaya Mrisho Kikwete akaanza na nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 4.5% mwanzoni mwa 2006. Miaka miwili tu baadaye, sasa tuna kasi ya mfumuko wa bei ya 10% (zaidi ya mara mbili ya ule alioridhi!). Hii takwimu imetolewa na IMF kwenye magazeti ya Tanzania ya wiki hii. Kama Jakaya ameweza kuongeza kasi ya mfumuko wa bei mara dufu kwa kipindi cha miaka miwili, itakuwaje akikaa miaka mitano? Naona tutarudi kule kwenye kasi ya mfumko wa bei ya 30% kabla hajamaliza miaka mitano madarakani.

2. Mwaka 1995, Mkapa alipokea uchumi uliokuwa unakua kwa kasi ya 3% kwa mwaka. Akaufanyia kazi, na wakati anatoka madarakani, alishaongeza kasi ya kukua kwa uchumi hadi 7.0% . Muungwana amerithi hiyo 7.0% na sasa ameshaishusha hadi 5%. Na bado anazidi kuharibu macroecononic stability ya nchi yetu. Inatisha sana!

3. Mkapa alipokea Hazina yenye fedha za kigeni kiasi cha US$267 million. Inaonekana ni kidogo lakini tunamshukuru Mzee mwinyi kwani yeye alirithi Hazina yenye US$0.0 million! Mkapa aliingia kazini kwa nguvu, na wakati anatoka mwaka 2005, Hazina ilikuwa na fedha za kigeni kiasi cha US$2,300 million. Hiyo ni mara tisa ya fedha alizokuta. Kikwete amerithi hizo fedha, na akaanzisha kitu anaita program yake ambacho kimezibugia haraka haraka, na sasa ziko chini ya US$2,000 million. Na anaendelea kuzidi kuzibugia mbiyo hivyo hivyo!

4. Mkapa ni mtu wa maneno machache, vitendo vingi. Kikwete ni maneno mengi, vitendo hakuna kabisa. Kuna miradi mingi ya maji mikoani aliyoanzisha Mkapa na kumwachia Kikwete amalizie. Badala yake, ameinyima fedha, na wabunge wamelalamika hovyo kwamba karibu miradi yote ya maji inakufa. Mabarabara ni hadithi hiyo hiyo!

We are in serious trouble!


Hayo yote uliyoyaandika ya Mkapa, yanafutwa na ufisadi wake pamoja na pesa alizokomba yeye pamoja na marafiki zake.

Mkapa alikuwa anaminya wengine ili aibe yeye na rafiki zake.

Mkapa ni fisadi namba moja, hayo mambo ya kukua kwa uchumi ambao ulikuwa unanufaisha middle class kama laki moja tu hapo Dar huku mamilioni ya watu mikoani wanazidi kuwa maskini, naona kukua kama huko hakuna maana yoyote.
 
ni ora kipindi ch ache mkapa,kila mtu hakuwa mfanyabiashra,hii serikli ya Muunwagna kila mtu mfanyabisahara,usajili mpya wa kina karamagi,Msabaha,Masha,wassira ambao umewafunika kina mramba mungai na diallo ambao walikuwapo kipindi cha ben mpaka sasa.

katika mawazo yangu,Mkaba he still the best president ever in Tanzania on the party of economic policy
 
Kuna viongozi corrupt ambao wanajenga sana uchumi. Mfano mzuri ni Suharto wa Indonesia. Alikuwa thoroughly corrupt lakini aliinua sana uchumi wa nchi yake. Baadhi ya viongozi wa sasa wa Kenya ni corrupt lakini wamejenga sana uchumi wa Kenya

JK na mawziri wake ni corrupt through and through, na wanaangamiza uchumi wa Tanzania. Mkapa alikuwa corrupt, hasa katika miaka yake ya mwisho, lakini alijenga sana uchumi. Data tumeshatoa.

Nawasikitikia Watanzania wenzangu wanavyohadaika urahisi. Nashangaa hata marafiki zangu waalimu wa UDSM wengi wao walihadaika urahisi na kudhani JK angekuwa Rais mzuri.

Anyway, mtu huvuna alichopanda.
 
Anyway, mtu huvuna alichopanda.

Mkuu Moshi,

Heshima mbele, ndio maana tunavuna matunda ya Mkapa, aliyetuletea awamu hii ya nne ya kina Karamagi, good observation mkuu wangu!

Mti corrupt kama Mkapa, hauwezi kuwa na matunda mema, au?

Anyways, vipi unaionaje hii hapa chini ya Muungwana?


THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

PRESIDENT Jakaya Kikwete has made his first public statement on the state of corruption in Tanzania since the infamous 'List of Shame' was released last month, declaring that no one will be spared in the ongoing investigations into widespread graft allegations.

The president has asserted that the government will probe each and every corruption allegation and take appropriate legal action against anyone implicated, regardless of his or her position or authority in government.

According to a statement issued by State House in Dar es Salaam yesterday, Mr Kikwete made the remarks in Arusha on Tuesday night during a fund-raising event for the Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT).

He sought to answer critics of the government's effectiveness in fighting high-level corruption, saying the government could not rush into taking action before investigations are concluded.
 
Mzee wangu mwalimu Augustine Moshi,

Pleaseee na Mkapa tafadhali maanake naona hata kichefuchefu kusikia kwamba alikuza uchumi, hiyo +3-7 ama ndio hiyo 2+2= 22!
Nafikiri labda inabidi nirudishe ile hadithi ya maisha ya mama yetu Tanzania maanake naona kama unasahau vile!
Kumbuka hata hiyo reserve unayozungumzia ilitokana na kwamba hakuwa na kitu cha kufanya zaidi ya kuuza tu urithi wetu.
Mjomba nakupa picha ya karibu sana na maisha yetu sote kisha nambie kati ya watu hawa wawili ni nani ana maendeleo.
1. Kalubandike:-
Huyu jamaa hupokea kitu kama millioni 2 kwa mwezi lakini ukitazama account yake hana kitu kwa sababu fedha yote huipeleka ktk kujijenga. Kajenga nyumba nzuri, kanunua shamba ambalo ni urithi kwa wanawe, kawapeleka watoto wake shule, kifupi hana shida kulingana na mtazamo wake kwani fedha yake ka invest ktk mali.
2. Pedejee:-
Huyu mjomba hukusanya fedha kiasi hicho hicho ama zaidi lakini fedha yake yote huiweka benki na matumizi yake binafsi. Hana nyumba kapanga nyumba ya msajili, hakuanzisha mradi wowote zaidi ya kuuza mirathi na kuhakikisha fedha yote iliyokuwa ikidaiwa inakusanywa kisha kanunua gari la kifahari, Pombe na mabinti ndio starehe yake. Kutwa hutembea na mamillioni mfukoni na wapambe hawakosi kuunganisha behewa. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba amekuta tayari mirathi kinachotakiwa ni kukusanya na kuziweka benki. Watoto wake hawana elimu, hakuna maji safi na afya ya watoto wake sio hoja wakiumwa wanajua hospital iko wapi. Na kisha kwa nini wasitafute kazi?. Nae kwa mtazamo wake haoni shida ikiwa fedha za urithi bado zipo. Haya maisha ni sawa na baadhi viongozi wetu wakati wa Nyerere ambao leo hii wanakufa maskini pamoja na kwamba walitamba enzi zile na nyumba za O'bay. Huyu ndio Mkapa alivyoliweka Taifa ktk nyumba ya O'bay kama vile hakuna mwisho!

Ni hayo tu mkuu... Oooh samahani ktk swala la JK kusema kweli akiba yetu kaitumia ktk kujenga upya miundombinu ya Taifa ambayo Mkapa aliiacha akitegemea wageni na misaada inaweza jenga miundombinu maadam fedha ipo benki. Miaka 10 ilikwisha, miundombinu ya Taifa ilikuwa ktk hali mbaya sana kama vile Mwinyi alivyokuta viwanda baada ya Nyerere. Je, unakumbuka lakini kuwa tanzania tulikuwa hatuna maji wala madawa wala chakula watu wakifa hali yeye akijirusha na kina Blair! - Kumbuka Darwin's Nightmare mjomba hakuna mtu aliamini sinema ile hata JK mwenyewe hakuamini hadi alipotembelea Mwanza.
Wanapofanana Mkapa na JK ni kuhujumu uchumi wetu, huu wizi umeanza toka enzi za kina Yona, sema tu sisi Wadanganyika wepesi sana wa kusahau na ndio maana Jk hawezi kumhukumu Mkapa.
 
Naanza kwa kujitetea kamba mie sio mwandishi nguli wa aina ya mzee mwanakijiji, ES, Mwafrika mwanamke n.k. I am just an artist and short talk reflecting way of art which i use to communicate to the community....

Tena, as heading above, sio nia yangu kuweka orodha ya depressed citizens hapa, ila just kuwachechemiza wenye machungu yao kuweka hapa ili tuone ni namna gani tumeguswa na matukio ya kifisadi yanayoendelea ndani ya nchi yetu..

Tangu nipigie kura serikali ya muungwana, niliamini kuwa mwarobaini wa matatizo ya mtanzania umepatikana. Nilikuwa naitetea kwa nguvu zote (mishipa ya shingo ikinitoka) serikali hii kuwa tumepata mkombozi. Kumbe nilikuwa brain washed kwa muda mrefu sana tena victim wa muda mrefu. Kuanzia kwenye media ambapo muungwana alikuwa anapata coverages hadi kwenye dini ambapo makasisi walituhakikishia kuwa mteule wa mungu ndiye huyu. Lakini maumivu ya kwanza ya kichwa yalinianza baada ya kutangazwa baraza kuuuubwa la mawaziri ambapo nilihisi kuwa hata wakurugenzi wa wizara watakuwa wameporwa baadhi ya majukumu na baraza hili. Pia nilikuwa napingana na nafsi yangu kuamini kuwa labda Mkapa alijua kitakachokuja Hughe cabinet) hivyo akasave much bucks ili kuhost this era. Mpaka leo nashangaa kuna baadhi ya wizara ambazo zina manaibu wawili ambapo labda hata waziri pekee angeweza shughuli hizo. Na pia mpaka sasa hatujaelezwa hizo added responsibilities zinazopelekea kuwa na baraza kubwa (linalonyonya hazina bila kuzalisha). Kingine kinachousonga mtima wangu ni kuwa pamoja na mkakati ambao pia umo ktk ilani ya uchaguzi ya CCM, ya kupambana na ufisadi na kuongeza tija, sijaona chochote kilichofanyika zaidi ya ngonjera na mipasho mbalimbali. Mfano kilio cha wakulima wa kada mbalimmbali haswa kuhusu upatikanaji wa pembejeo na masoko (hasa bei) imekuwa ni utata. Nimeambiwa kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa letu lakini nadhani nimedanganywa, tuna rasilimali ambazo kwa uchache na wingi wake tungeweza kuongeza tija.

Nadhani wengi mnafahamu lile shairi maarufu la yule baba na wanae ambapo aliwausia wanae kuwa mali watayapata shambani. Nadhani labda vijana wale kwa kutokufikiria mara mbili mmbili walianza kulima shamba right away. nadhani kama wangefikiria zaidi kuhusu ujumbe wa baba yao wangeligundua hazina ya madini iliyopo chini ya shamba lao na wangekuwa mbali zaidi. Nimejaribu kufikiria zaidi kuwa wengi wa vigogo wetu hawako creative ktk utawala wao (sio uongozi). Jaribu kufuatilia kuanzia hotuba zao hadi wanapojibu maswali bungeni wanakuwa hawana jipya. sana sana hawapendi kuambiwa ukweli.

Imani yangu kwa serikali yangu inazidi kupotea hasa kuhusiana na ahadi nyingi zisizotekelezwa. Tuliahidiwa kuwa hakutakuwa na uingiaji wa mikataba mipya ya madini mpaka baadhi ya vipengele vya kanuni kuboreshwa, Tuliahidiwa kuwa tetesi za ufisadi zingemwondolea mhusika sifa ya kuaminiwa tena ila duh! kumbe haikuwa kweli. Pamoja na yooote ahadi ya ufanisi na utendaji hatujaiona mpaka sasa. imefikia mahala kwamba kiongozi akifanya jambo fulani ambalo anapaswa kufanya, tutamsifia kuwa angalau anajali.

Bunge limeporwa haki yake ya kutunga sheria sanasana executives wameweka wizara ambayo ndiyo draftsman yupo huko... Na ole wake mbunge wa chama dume aihoji serikali ya chama bungeni... atashughulikiwa ndani ya chama. pamoja na kuwa nilichukia vyama vingi hapo awali lakini kwa ushawishi w Baba wa Taifa serikali iliridhia viwepo na cha kushangaza baada ya sie kuona faida za vyama tele bado serikali inakumbatia katiba ya zamani ya chama kimoja. Tume ya Nyalali iliona baadhi ya vipengele vya kubadilisha au kuboresha ktk katiba lakini mpaka leo ripoti ile inaozea kabatini.

Lakini naamini haya mambo ya ufisadi yalianzia pale ambapo viongozi walipogeuka kuwa watawala, na pale ambapo watawala hawa wakayapiga teke maadili na miiko ya uongozi. Kwa mfano, wengi wa watawala ni mabepari na wakati huohuo wanaitumikia nchi. Kama mtu anataka kuwa mtawala au kuongozi anapaswa kuikana nafsi yake kwanza na kukubali kuubeba msalaba wa taifa kuelekea kilimani. mabepari hawa wanahonga ili kupata kura, mabepari hawa hawajali wala kusikia kilio cha umma kuhusu masuala ya kimsingi kama vile nishati na miundombinu. mabepari hawa hawa wana hisa ktk makampuni makubwa yanayoinyonya nchi. walah nasema kuwa am soooo depressed.

Muungwana isafishe nyumba yako au la sivyo viroboto, papasi na mchwa wataendelea wataitafuna na kuiaibisha zaidi. Na ujue kuwa mchwa hatishiwi kwa maneno au maonyo, dawa ya mchwa ni kumwondoa...

Tumetoka mbalu aisee...
 
Mimi huyu Jakaya ananikatisha sana tamaa ninapomlinganisha na Mkapa. Ni kweli inaelekea Mkapa amekuwa na possession mania kiasi, lakini alijenga sana uchumi. Naomba nionyeshe kukatishwa tamaa kwangu na Muungwana kwa kulinganisha utendaji wa serikali yake na wa ile ya Mkapa, kama ifuatavyo:

1. Benjamin William Mkapa alipokea nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 30%. Hiyo ilikuwa 1995. Mfumuko wa bei wa juu ni kitu hatari sana kwa uchumi na usalama wa taifa. Mkapa alipambana nao kwa dhati, na wakati anang'atuka mwaka 2005, alishaushusha hadi 4.5%.

Jakaya Mrisho Kikwete akaanza na nchi yenye kasi ya mfumuko wa bei ya 4.5% mwanzoni mwa 2006. Miaka miwili tu baadaye, sasa tuna kasi ya mfumuko wa bei ya 10% (zaidi ya mara mbili ya ule alioridhi!). Hii takwimu imetolewa na IMF kwenye magazeti ya Tanzania ya wiki hii. Kama Jakaya ameweza kuongeza kasi ya mfumuko wa bei mara dufu kwa kipindi cha miaka miwili, itakuwaje akikaa miaka mitano? Naona tutarudi kule kwenye kasi ya mfumko wa bei ya 30% kabla hajamaliza miaka mitano madarakani.

2. Mwaka 1995, Mkapa alipokea uchumi uliokuwa unakua kwa kasi ya 3% kwa mwaka. Akaufanyia kazi, na wakati anatoka madarakani, alishaongeza kasi ya kukua kwa uchumi hadi 7.0% . Muungwana amerithi hiyo 7.0% na sasa ameshaishusha hadi 5%. Na bado anazidi kuharibu macroecononic stability ya nchi yetu. Inatisha sana!

3. Mkapa alipokea Hazina yenye fedha za kigeni kiasi cha US$267 million. Inaonekana ni kidogo lakini tunamshukuru Mzee mwinyi kwani yeye alirithi Hazina yenye US$0.0 million! Mkapa aliingia kazini kwa nguvu, na wakati anatoka mwaka 2005, Hazina ilikuwa na fedha za kigeni kiasi cha US$2,300 million. Hiyo ni mara tisa ya fedha alizokuta. Kikwete amerithi hizo fedha, na akaanzisha kitu anaita program yake ambacho kimezibugia haraka haraka, na sasa ziko chini ya US$2,000 million. Na anaendelea kuzidi kuzibugia mbiyo hivyo hivyo!

4. Mkapa ni mtu wa maneno machache, vitendo vingi. Kikwete ni maneno mengi, vitendo hakuna kabisa. Kuna miradi mingi ya maji mikoani aliyoanzisha Mkapa na kumwachia Kikwete amalizie. Badala yake, ameinyima fedha, na wabunge wamelalamika hovyo kwamba karibu miradi yote ya maji inakufa. Mabarabara ni hadithi hiyo hiyo!

We are in serious trouble!
Mh kwahiyo mnataka kusenaje
 
Ama kweli watu walikuwa na analysis nzuri sana enzi hizo!!
Wako wapi hawa wazee
cc Augustino Moshi,Mukandara &etl!?
 
Back
Top Bottom