Wangapi mlipitia huku? Tulipokuwa watoto tuliharibu sana miundo mbinu ya TTCL

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,487
2,344
Nakumbuka wakati nakua tulikuwa tunatengeneza magari ya waya za tairi na waya zile zenye rangi rangi za TTCl. Kipindi hicho tulikuwa tunazunguka mitaa ya wazito maarufu kama uzunguni ambako ndio kulikuwa na watumiaji wengi wa simu za mezani kipindi hicho, basi tunatafuta zile njia zilizopita ardhini. Tukifanikiwa kuzipata tunafukua tunakata pande la maana tunasepa.

Kuna kipindi TTCL walipiga mkwara kuwa wakimkamata mtoto anaendesha gari lenye waya zao atakula mbarati. Basi tukaona isiwe tabu tukawa tunazichuna maganda kupoteza ushahidi. Kipindi hicho TTCL walipata tabu sana na hasara za kutosha.

Leo naangalia wanangu wanavyopenda kushinda ndani kwenye udigitali hawaelewi kabisa mambo kama yale.
 
Miye nilikuwa natumia vzr Sana zile kadi za kupiga simu za ttcl, unabonyeza namba fulani ikiita unaongea pesa haishi. G tulikuwa tunasogoa weee mpk basi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom