wangapi kati ya viongozi wetu wanafanya haya!!!!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
RAIA MWEMA: Wakati ukiwa Spika na mbunge ulijitahidi kujenga shule kwa manufaa ya wananchi wa Ukerewe, na ulichangiwa na baadhi ya watu. Watu walitarajia kuwa ungeimiliki, lakini kwa mashangao uliikabidhi serikalini. Kwanini uliamua kufanya hivyo?
MSEKWA: Nilikuwa na sababu nzuri sana ya kujenga shule ya sekondari, ya ngazi ya juu, high school. Ni shule ambayo nimeijenga katika kijiji nilichozaliwa. Ni kijiji kinaitwa Bugombe katika Wilaya ya Ukerewe. Ndiko nilikozaliwa mimi, nikaishi na wazazi wangu, hadi pale nilipohamia shule za bweni.

Lengo langu la kujenga shule hiyo lilikuwa ni kuwashukuru wazazi wangu na kuwasaidia wananchi wa wilaya yangu, waone kwamba mimi nimepata bahati ya Mwenyezi Mungu. Nimesoma nimefika kiwango cha juu sana wakati ule. Mimi ndiye niliyekuwa na digrii Ukerewe nzima, na siyo tu kwamba nimefika kiwango cha juu cha elimu, lakini Mwenyezi Mungu akanijalia nikafika kiwango cha juu cha utumishi wa umma. Nimekuwa katika ngazi za juu wakati wote, kiongozi wa shughuli mbali mbali, kwenye serikali, katibu mkuu kwenye chama.

Nimekuwa mbunge mpaka Spika. Kwa hiyo, ili watu wanufaike na uongozi wangu huo, na waweze kunikumbuka kuwa tulikuwa na mwenzetu hapa alijaliwa na Mwenyezi Mungu, na yeye akatujali sisi. Yaani si kwamba alijaliwa, akahodhi hiyo neema. Ninaona ni vizuri wakumbuke kuwa Mwenyezi Mungu alinijalia, na mimi nikawagawia wenzangu neema hizo.

Kwa hiyo, nikaona kumbukumbu ya kudumu itakayokaa miaka mia tatu, mia nne ijayo ni kuwajengea shule ili kusudi vizazi na vizazi vitakavyosoma katika shule hiyo waweze kukumbuka kwamba hii yote tumefaidika kutokana na mwenzetu aliyefanikiwa na sisi akatuwezesha tufanikiwe.

Kwa madhumuni hayo, kama ningeifanya shule kuwa yangu binafsi, ya private, ningewalipisha ada kubwa ya shule. Kama mnavyojua shule zinalipisha hadi shilingi milioni moja kwa mwaka au zaidi. Mimi lengo langu ni kuwasaidia vijana wa Ukerewe. Ukiwatoza shilingi milioni moja unakuwa bado hujawasaidia.

Ndiyo maana nikaikabidhi serikali ili waweze kulipa shilingi 20,000 kwa mwaka sawa sawa na shule nyingine zozote. Lengo langu lilikuwa ni hilo-kuwasaidia vijana wa Ukerewe, si kuwakamua kwa kufanya biashara mimi mwenyewe. Nilikuwa sitaki biashara. Niliijenga nikijua kwamba maslahi yangu ya ustaafu serikalini ni mazuri, yananitosha. Sihitaji tena mapesa mengine kwa kukamua wananchi kwa kufanya biashara ya elimu.

Tangu mwanzo niliwaeleza wafadhili wangu, kwamba mnisaidie, tujenge shule ya kuwasaidia vijana wa Ukerewe. Si kunisaidia kibiashara. Hapana. Kwa kweli wangesononeka sana kama wao wangenichangia halafu mimi nifaidike kwa biashara kutokana na fedha za wafadhili, ambao walitaka kusaidia vijana, si kunisaidia mimi.

Hayo ndiyo maelezo yangu, kwa nini niliikabidhi serikalini. Na ninafikiri kwa kuwa Mwalimu Nyerere alitufundisha kwamba kuongoza ni kuonyesha njia, ninafikiri mimi nimeonyesha njia. Na wewe ukipata mfadhili jenga shule uikabidhi serikali, usifanye biashara yako.

source raia mwema
 
..............nonsense,

ubunge ni kuwakilisha wananchi bungeni ili serikilai ifanye maamuzi yatakalyowanufaisha; siyo kuchangisha wafanya biashara (wafadhili) wajenge shule wilayani kwako.
 
..............nonsense,

ubunge ni kuwakilisha wananchi bungeni ili serikilai ifanye maamuzi yatakalyowanufaisha; siyo kuchangisha wafanya biashara (wafadhili) wajenge shule wilayani kwako.

Kichunguu

Ukiondoa hilo nonsense hapo juu, kwa ujumla na kubaliana na maneno yako. Sijui lini wapiga kura wataelewa ukweli huu? Mtazamamo huu wa baadhi ya watu kwamba wabunge ni "Mama Theresa" kwa kugawa 'biskuti na pipi kwa wananachi" iko siku itapelekea kuwa na bunge la vibaraka wa wafadhili ama wabunge-wafadhali- mabwanyenye ambao ubunge wao si kutumikia bungeni bali kupata ukuu wa kuonyoosha madili yao na kuwatuliza mzuka wananchi kwa kuwafadhili sabuni za kuogea! Laiti watu wangekujua kwamba 'pipi na biskuti' ni matokeo ya kuwa na wabunge wenye kupitisha sheria zilindazo maslahi ya na kuhasimamia serikali itekeleze sera bora hapo ndipo tungepata bunge lenye nguvu ya kuwajibisha! Tunahitaji wabunge wenye kutoa dira kwa taifa, kupinga ufisadi na kutetea rasilimali za Tanzania. Ukitujengea shule moja na kuruhusu fedha za shule elfu moja zikavufujwa tutakusuta badala ya kukupongeza. Aulizwe, katika kipindi cha uspika wake, taifa limepoteza fedha kiasi gani kwa bunge alilokuwa akiongoza kushindwa kulinda rasilimali zetu? Je, kwa fedha hizo tungejenga shule ngapi? Kama waliongoza vikao vya kupitisha sheria ambazo sasa zinapitiwa upya kwa kweli wanapaswa kujieleza. Ni vizuri watoto wa ukerewe wamepata shule lakini tutazame picha pana zaidi.

JJ
 
Mtu wa Pwani,

hata mimi najiuliza maswali hayohayo unayojiuliza. yuko jamaa hapa alilamika kwamba wawekezaji ktk gesi mkuranga wameenda kuchangia ujenzi wa shule rombo. mbunge wa mkuranga kwa vyovyote vile amelala usingizi.

suala lingine ni sisi watanzania kuwaachia/kuwasusia shughuli za maendeleo wabunge wetu. yaani kuchangia/kuhamasisha maendeleo ya kule tunakotoka tunasubiri mpaka mbunge aitishe vikao.

badala ya kuuliza wabunge wangapi wamefanya kama Mzee Msekwa, tupanue uwigo na tuulize watanzania wangapi wenye uwezo wamechangia maendeleo mahali popote pale?

Mwekezaji mkubwa ktk viwanda vya chuma nchini Marekani alianzisha chuo kikuu cha Carnegie Mellon. Yeye aliamua sehemu ya utajiri wake iende ktk kuelemisha wananchi wenzake ktk masuala ya Ufundi.

Mimi ningependa hawa kina Bakhresa,Mohamed Dewji,Reginald Mengi,Gachuma,...wajitolee kuanzisha private institutions za maana ktk masuala ya kijamii kama elimu au afya.

NB:
serikali ina wajibu wa kujenga mashule,vyuo,hospitali. mara nyingi serikali inachangisha wafanya biashara halafu inajizolea sifa ya kupeleka maendeleo kwa wananchi.

juhudi za serikali zitofautishwe na juhudi na michango ya watu binafsi.
 
attitude za namna hii ndio zimewaweka watz wengi kuwa ombaomba, hata tukienda kwenye research wanatuulizia habari za ufadhili, sijui ni nini hii. Yaani hayo mawazo yako Kichuguu ukiongea kwa watz wenzetu huku vijijini watakucheka sana.Ndio maana Dewji kule kwetu Singida hahangaiki, yeye anapeleka unga tu wakati wa njaa na kura anapata. Yule bwana Harusi wa juzi Nyalandu yeye anaenda zake Marekani anaokoteza machine fake za maji anapeleka Singida kaskazini basi wanyaturu wote meno nje wanampa kura na wanamuona bonge la mbunge. Ndivyo tulivyo, tumekaa mkao wa kupewa msaada kuanzia Rais wetu hadi wananchi huko chini kabisa. Sasa kubadilika sijui tuanzie wapi-aanze Rais then wananchi au wananchi then Rais?

Tumekuwa tukijadili ilikuwaje Tanzania ikashika nafasi ya mwisho katika mataifa ya watu wenye furaha (happiness index) kiasi cha kuzidiwa na Rwanda ambayo bado wamezungukwa na mauaji ya 1994-Tulikutana na one of the interviewers, yeye anasema wakati wakusanya takwimu watz wengi walijiweka kinyonge ili wahurumiwe wapatiwe msaada, tena walipokuwa wakiulizwa wanayaonaje maisha karibu wote walikuwa wanalia vibaya mno, tena wakiomba wasaidiwe: conclusion a very unhappy nation!

So, the repurcations here are far reaching! We need to change our attitudes kwamba maendeleo yetu ni jukumu letu na sio la mtu mwingine na kwamba kazi ya mbunge sio kutugawaia mahindi au kutuchimbia visima vya maji. Haya mtu anaweza kuyafanya bila hata kuwa mbunge, na wala hayampi sifa ya kuwa mbunge.
 
Mimi pamoja na kuwa ni maskini wa pesa- huwa nina furaha tu sana saa zote- ni mcheshi na mchangamfu sana! Sijui wengine kama mna donge hata mnashindwa kutabasamu- kisa eti kuna mafisadi! Mimi saa ingine siwaelewi vizuri Watz!
 
Ndugu!
Ni ngumu kulazimisha furaha- ni heri tu kununa- hadi kieleweke!
 
Angalieni mfumo wetu wa elimu ,mambo yote yapo hapo japo hatutaki kuukubali ukweli huo.
 
..............nonsense,

ubunge ni kuwakilisha wananchi bungeni ili serikilai ifanye maamuzi yatakalyowanufaisha; siyo kuchangisha wafanya biashara (wafadhili) wajenge shule wilayani kwako.

Prof. Kichuguu,

Kazi ya mbunge pia ni ku organize resources mbalimbali kwa lengo la kusaidia kuendeleza maendeleo ya wilaya yake.

Kwa hilo nampongeza Msekwa maana angalau kasaidia kuendeleza elimu jimboni kwake.

Labda kitu ambacho wanasiasa wengi wanafanya ni kutokuwahusisha wananchi moja kwa moja. Miradi yote ya maaana na inayodumu ni ile ambayo wananchi husika wanashirikishwa na pia kuchangia ili wawe na aina fulani ya ownership kwenye hizo projects na hivyo kuwa tayari kuzilinda na kuendeleza.

Hii miradi ya kujengwa na wafadhili bila nguvu ya wananchi huwa inakufa haraka sana hao wafadhili wakiondoka.

Naamini mbunge makini yuko katikati, yaani analiwakilisha jimbo lake vizuri bungeni kuhakikisha sheria za maana zinatungwa na kuiwajibisha serikali lakini pia anatumia ubunifu wake na resources mbalimbali zilizopo wilayani kwake kuendeleza jimbo lake. Shule, huduma za afya na kilimo ni katika miradi ambayo inatakiwa ipewe kipaumbele.
 
Mtanzania,

nakubaliana na wewe 100%. wananchi lazima washirikishwe ktk shughuli za kujiletea maendeleo. hii tabia ya kusubiri kila kitu serikali imesababisha wananchi wawe wategemezi mno.
 
Back
Top Bottom