Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,180
- 664
RAIA MWEMA: Wakati ukiwa Spika na mbunge ulijitahidi kujenga shule kwa manufaa ya wananchi wa Ukerewe, na ulichangiwa na baadhi ya watu. Watu walitarajia kuwa ungeimiliki, lakini kwa mashangao uliikabidhi serikalini. Kwanini uliamua kufanya hivyo?
MSEKWA: Nilikuwa na sababu nzuri sana ya kujenga shule ya sekondari, ya ngazi ya juu, high school. Ni shule ambayo nimeijenga katika kijiji nilichozaliwa. Ni kijiji kinaitwa Bugombe katika Wilaya ya Ukerewe. Ndiko nilikozaliwa mimi, nikaishi na wazazi wangu, hadi pale nilipohamia shule za bweni.
Lengo langu la kujenga shule hiyo lilikuwa ni kuwashukuru wazazi wangu na kuwasaidia wananchi wa wilaya yangu, waone kwamba mimi nimepata bahati ya Mwenyezi Mungu. Nimesoma nimefika kiwango cha juu sana wakati ule. Mimi ndiye niliyekuwa na digrii Ukerewe nzima, na siyo tu kwamba nimefika kiwango cha juu cha elimu, lakini Mwenyezi Mungu akanijalia nikafika kiwango cha juu cha utumishi wa umma. Nimekuwa katika ngazi za juu wakati wote, kiongozi wa shughuli mbali mbali, kwenye serikali, katibu mkuu kwenye chama.
Nimekuwa mbunge mpaka Spika. Kwa hiyo, ili watu wanufaike na uongozi wangu huo, na waweze kunikumbuka kuwa tulikuwa na mwenzetu hapa alijaliwa na Mwenyezi Mungu, na yeye akatujali sisi. Yaani si kwamba alijaliwa, akahodhi hiyo neema. Ninaona ni vizuri wakumbuke kuwa Mwenyezi Mungu alinijalia, na mimi nikawagawia wenzangu neema hizo.
Kwa hiyo, nikaona kumbukumbu ya kudumu itakayokaa miaka mia tatu, mia nne ijayo ni kuwajengea shule ili kusudi vizazi na vizazi vitakavyosoma katika shule hiyo waweze kukumbuka kwamba hii yote tumefaidika kutokana na mwenzetu aliyefanikiwa na sisi akatuwezesha tufanikiwe.
Kwa madhumuni hayo, kama ningeifanya shule kuwa yangu binafsi, ya private, ningewalipisha ada kubwa ya shule. Kama mnavyojua shule zinalipisha hadi shilingi milioni moja kwa mwaka au zaidi. Mimi lengo langu ni kuwasaidia vijana wa Ukerewe. Ukiwatoza shilingi milioni moja unakuwa bado hujawasaidia.
Ndiyo maana nikaikabidhi serikali ili waweze kulipa shilingi 20,000 kwa mwaka sawa sawa na shule nyingine zozote. Lengo langu lilikuwa ni hilo-kuwasaidia vijana wa Ukerewe, si kuwakamua kwa kufanya biashara mimi mwenyewe. Nilikuwa sitaki biashara. Niliijenga nikijua kwamba maslahi yangu ya ustaafu serikalini ni mazuri, yananitosha. Sihitaji tena mapesa mengine kwa kukamua wananchi kwa kufanya biashara ya elimu.
Tangu mwanzo niliwaeleza wafadhili wangu, kwamba mnisaidie, tujenge shule ya kuwasaidia vijana wa Ukerewe. Si kunisaidia kibiashara. Hapana. Kwa kweli wangesononeka sana kama wao wangenichangia halafu mimi nifaidike kwa biashara kutokana na fedha za wafadhili, ambao walitaka kusaidia vijana, si kunisaidia mimi.
Hayo ndiyo maelezo yangu, kwa nini niliikabidhi serikalini. Na ninafikiri kwa kuwa Mwalimu Nyerere alitufundisha kwamba kuongoza ni kuonyesha njia, ninafikiri mimi nimeonyesha njia. Na wewe ukipata mfadhili jenga shule uikabidhi serikali, usifanye biashara yako.
source raia mwema