Wandugu tatizo uwizi Inyala/ iyunga Mbeya kamwe halitaisha

kasa boy

Member
Oct 1, 2017
8
1
Ndugu zangu, wanaharakati wenzangu napenda kuzungumzia suala hili kwa uchungu mkubwa sana hii ni kutokana wiki chache nyuma ulifanyika msako mkali kwa kushirikiana na polisi pamoja wana-mtaa wa Inyala na kufanikisha kuwakamata wezi wote kasoro mmoja tu ndo ambaye hakukamatwa. Cha kushangaza wezi walishataja walipoenda kuviuza vitu na kukili kuwa waliiba lakini cha ajabu zaidi ni palisi anaposema waliouziwa wamekimbia na sasa hivi wanaishi dar, kutokana na uchunguzi wa cm kupitia cm.

Kubwa zaidi linalonishangaza ni polisi wameanza kuwachia waarifu mmoja mmoja kurudi mtaani kwa mbwembwe na majigambo kitu ambacho uelewa wangu mdogo ni hatari ukizingatia hawa waarifu hawatakiwi katika Mtaa na M/kiti lishatoa taarifa hiyo kwenye vituo vya polisi jirani. Je! Suala lilofanya na polisi wetu tunaowaamini kabisa la kuwatoa watumiwa kurudi uraiani kwa kivuli cha udhamini ni sahihi?

Wadau mnasemaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo Inyara kama unaenda Uyole kuna mlima unaitwa mlima Nyoka haufai kabisa kupita na gari za mizigo kuanzia saa moja, yani kigiza kinavyoanza au alfajiri kabla hakuja pambazuka. Kuna faza wanamwita Tenende ana vijana wake hawafai hao wanashusha mzigo na gari inatembea chakushangaza hakuna ambaye anaibiwa na akafanikiwa kupata mzigo wake japo taarifa zinapelekwa vituo vya polisi.
 
Back
Top Bottom