Wandugu okoeni ndoa ya kijana mwenzenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wandugu okoeni ndoa ya kijana mwenzenu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NGULI, Mar 31, 2010.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Amepatwa na ugonjwa unaoitwa PANGUSA;-nia aina ya ugonjwa unaopata wanaume sehemu za siri za mbele unakuwa kama umepata mmba kali ukifuta inazidi kulika kama kifuto cha pencil mwishowe inakuwa ndogo na dhaifu.

  Ameupata kwa kutumia mataulo ya gym hapa dsm. Amenihakikishia kuwa hajatoka nje ya ndoa yake na anampenda sana mke wake. Ila dr. wa hospitali moja kubwa ya binafsi amemwambia lazma aende na mke wake ili watibiwe Je? mke wake atamwamini? na aliwahi kumkanya kuhusu kwenda gym akihofia ndio njia ya kutoka nje ya ndoa.

  Anaomba ushauri wenu na yuko hapa anasoma posti zenu tafadhali msaidieni rafiki yetu huyu.
   
 2. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama alichoambiwa na daktari hataki.....atasikiliza vipi tutakachomwambia sisi? Muache kitu kikatike watu wengine wamsaidia kulea mama watoto..!
   
 3. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  anasema yeye haogopi kwenda kwa matibabu ila anaogopa mkewe atareact vp anaweza ku respond kwa talaka. Anasema ana wivu kupindukia na hataki kuteteresha familia yake.
   
 4. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu huwa sihangaiki na mtu asiyejali afya yake! Usipojipenda mwenyewe unataka nani akupende? Muache kibamia kikatike.......aone huyu mke atakaa nae vipi!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,168
  Trophy Points: 280
  Huo ugonjwa mbaya sana,
  asipowahi matibabu atakatika umbile la jinsia yake.
  Bora lawama kuliko fedheha, amwambie tu mkewe wakapate tiba sahihi wakati muafaka. Kuliko kijibanza halafu apatwe na kilema cha maisha.
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Yote mliyoyasema mliotangulia... mbona ya mbolea...
   
 7. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Aje hapa JF tumlishe nasaha mbichimbichi mwenyewe.......! Why using an agent? Let him, or all come to this ground for the vigin advices.
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Kwanza nampa pole kijana mwenzangu huyo.Ila hakuamakini kuzingatia suala la afya hasa pale ambapo alitumia vifaa vya public kujiswafi

  Pili,sasa akisema anaogopa kwa sababu familia itavunjika inabidi ajue kwamba asipofuata ushauri wa daktari hata hiyo familia anayotaka kuilinda itaangamia.

  Ushauri:

  Ni bora akae na mama watoto wake atumie muda mwingi kumshawishi kuhusu hilo tatizo.Pia sasa inaonekana kijana hajaweza kumfanya mke wake amwamini ktk kipindi alichoishi nae ndiyo maana hata anafikia hatua ya kumkataza kwenda Gym kwa kuogopa jamaa anaweza kutoka nje.

  Ndiyo mana nasema kujenga uaminifu kuna faida kubwa sana,sasa hapa kazi imekua nzito zaidi kwa kuwa bibie hamuamini.Akae chini tu amueleze mke wake kwa upole,utulivu na upendo wa hali ya juu.Ikiwezekana hata kama alikua hamuonyeshi mapenzi ya kutosha basi aanze mara moja halafu apage siku soon amweleze.
   
 9. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Yupo hapa JF kama guest
   
 10. RR

  RR JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Jamaa anaanza kujiona mwenye hatia wakati hana hatia? Jamaa ajiamini (kwamba hana hatia/hajafanya kosa), amwambie ukweli mkewe!
  Akijihukumu mwenyewe hakuna msaada wa nje utakaomfaa.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  maradhi aina ya STD yote hospitalini unaambiwa ukatibiwe pamoja na mke wao kwa sababu hata akitibiwa yeye tu, labda mkewe tayari ameshapata, atamuambukiza tena na tena

  sasa kwa ushauri wangu tu, angetengeneza mazingira ya kuzungumza na mkewe. lazima mkewe atakasirika na anaweza pia asimuamini awali, lakini mwanamke anaweza kujua pale anapodanganywa na anapo ambiwa kweli ( japo kuwa wakati mwengine tunajua kuwa tunadanganywa but tunajifanya hatuoni)

  wapeleke watoto kwa bibi yao kutembea, mwite mama watoto pembeni, mwambie ukweli uliotokea.......atakasirika lakini lazima atakwenda hospitali. hakuna anaetaka kuuguwa
   
 12. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Taulo za gym?................ hivi hushauriwi kutochangia vitu kama hivi?
   
 13. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Anakushukuru sana kwa ushauri wako, amekuja kwangu kwa ushauri nikwambia wapo wenye nguvu kuliko mimi ambo sithubutu hata kuinama na kushika gidamu ya viatu vyao.
   
 14. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dr. amempa ushauri mzuri sana maana hata akiamua kumtibu akapona je si atapata tena kwa mkewe? so ni bora wote watibiwe! mwambie aache ubishi!!
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Too Bad!
  Kimsingi namsikitikia kwa ugonjwa, lakini masuala ya hofu ya mke/familia ni minor sana kulinganisha na risk au changamoto ya kiafya anayoikabili...Inapofikia hivi kawaida , ni kuwa bold tu, unamkalisha mama chini na kumwambia ukweli, then mnafika muafaka, hawezi kujitibu kwa ujanjaujanja, ugonjwa mkubwa huu!
  Sasa akikaa kimya kumhofia mke, then ataweza kuficha hiyo hali?..Au atatembea naye tu ..potelea mbali?
  Mi naona suala hili linazungumzika tu, ni matter ya uelewa wa mke zaidi, na kulinda heshima ya nyumba!
  Akae na huyo mywife waweke wazi, hakuna longolongo-mbadala!
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  vitu vinne vinavyokatazwa kuchangia pamoja ni
  1) Kiwembe
  2) Mswaki
  3) Taulo
  4) Shanuo/kitana/ brush ya kuchania nywele ......
   
 17. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2010
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Thats the point mkuu. Nadhani ni uwoga tuu. Maana hata Dr kama ni mtaalamu anaweza kuprove kwamba source ilikuwa ni gym. Na kama wanaaminiana, kwanini kuogopa kumwambia ukweli? Tunasema hapa daily ndoa nyingi zinavunjika coz of lack of communication. sasa akitibiwa, hayo madawa atanywea wapi? na Vipi mkewe aikigundua kwamba amewahi kuugua ugonjwa wa namna hiyo na kutibiwa, si ndio atakuwa ameamsha na kuaminisha anachokikataa sasa?
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Cha msingi rafiki yako aende Hospital kuna wataalam wengi na huduma zote zinapatika huko
   
 19. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Amejaribu maji ya betri? mara nyingi haya huponesha na kukausha kabisa ugonjwa wa pangusa. Kwa wale mnaoanza kuhisi ataungua yes ni kweli kwa sababu ni acid but after a few hours ugonjwa unatoka, wadudu wanakufa halafu anauguza kidonda kwa siku 3 anapona kama atapaka GV.

  Surely hii ndo namna pekee ya kupata tiba bila kuripoti nyumbani na kama chakula cha mama kitakuwa kinapungua ukubwa si afadhali maumivu ya siku 3 kuliko maumivu ya maisha yote?

   
 20. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Ana lake jambo huyo..
  Anataka kuiondoa na oho ya mkewe pia.
   
Loading...